Kila mara nimekuwa nikisisitiza juu ya umuhimu wa kuwa na ratiba. Ukiamka asubuhi pangilia siku yako kwa namna ambavyo ungependa iwe. Andika vitu ambavyo utafanya na hata vile ambavyo hutafanya.
Lakini pia kuna vitu ambavyo vinajirudia kila siku katika ratiba yako. Na hapo ndipo unapaswa kuwa na mfumo fulani ambao unaufuata. Mfumo huu utakuwezesha wewe kuchomeka majukumu ya kazi kwenye ratiba yako ambayo yanajitokeza mara moja.
Moja ya ratiba ya siku ambayo imekuwa maarufu mtandaoni ni ratiba ya Benjamin Franklin. Bwana Franklin alikuwa na ratiba maalumu aliyokuwa anaifuata kila siku ya maisha yake na pale ambapo kuna majukumu mapya ambayo yangejitokeza basi alikuwa anayaweka humo katikati kwenye ratiba iliyopo
Ratiba yake ilikuwa hivi:
Alikuwa anaamka saa 11 asubuhi na kitu cha kwanza alikuwa ananiuliza. Ni kitu gani kizuri ambacho ninaenda kufanya siku ya leo?
Benjamin Franklin ni mmoja watu ambao walikuwa wanaamka mapema sana na usemi wake wa Early to bed , early to rise makes a person healthy wealthy and wise. Umekuwa ni usemi maarufu sana kwenye ulimwengu wa leo. Kuna makala nzima kwenye blogu hii inayoeleza sanaa ya kuamka asubuhi na mapema.
Baada ya hapo alikuwa anahakikisha amepangilia ratiba yake ya siku hiyo. Baadaye alikuwa anasoma kitabu na kupata kifungua kinywa.
SOMA ZAIDI: Sababu Tano Kwa Nini Unashindwa Kuamka Asubuhi Na Mapema Na Kitu Gan Unaweza Kufanya Sasa Hivi
Ukiangalia vizuri ratiba ya Benjamin Franklin unatoka na vitu vifuatavyo.
Moja kulala mapema na kuamka mapema. Hiki kitu ni kigumu kwenye ulimwegu wa leo hasa uliojazana intaneti na mitandao ya kijamii na tamthiliya. Ila unapaswa kama unataka kufika mbali.
Anza kujenga utaratibu wa kulala na kuamka mapema kuanzia leo.
Pili ni kusoma vitabu. Inaonekana wazi kuwa Benjamin Franklin alikuwa msomaji mzuri wa vitabu, kwenye ratiba yake kuna vipengele vya kusoma mara mbili. Na wewe jiwekee utaratibu wa kusoma kila Mara. Kiufupi kusoma kupe kipaumbele kwenye maisha yako sawa na ambavyo unatoa kipaumbele kwenye kula na kuoga.
ANZA KWA KUSOMA KITABU HIKI CHA BURE
Tatu kufanya kazi kwa bidii. Hiki Ni kitu kingine muhimu kwenye ratiba ya Franklin. Jamaa anaonekana alikuwa anathamini kazi kazi kwelikweli na alikuwa anafanya kazi kwa bidii. Na hiki linaweza kuthibitishwa kupitia nukuu zake pia;
Kama uko huru kufanya kazi, basi fanya kazi kwa bidii na kamilisha majukumu ya muhimu.
kila mtu anaweza kuwa na utajiri, afya njema na busara kupitia kufanya kazi kwa bidii, kujituma na nidhamu
Benjamin Franklin
Nne kujitathimini. Kila siku jioni alikuwa anajiuliza ni kitu gani kizuri nimeweza kufanya ndani ya siku ya leo chenye manufaa kwa watu wengine.
Wewe pia unapaswa kuwa na utaratibu kama huu. Ikifika jioni jiulize ni kitu gani kizuri nimefanya leo? Ni mchango gani nimeweza kuleta kwa jamii yako. Ukigundua kwamba hakuna kitu cha maana umefanya usilale kwanza. Amka walau ufanye kitu kimoja tu kwa siku hiyo.
Tano, chakula na ulaji. Hiki ni kitu kingine ambacho kinaonekana kilikuwa kinafuatiliwa kwa ukaribu sana na Benjamin Franklin.
Watalaam wanashauri kuhakikisha kuwa walau upate kifungua kinywa hata kama hutapata mlo wa mchana.
Na ushauri mwingine maarufu ni ule unaosema;
Pata kifungua kinywa kama mfalme, chakula cha mchana kama mwana wa mfalme na chakula cha jioni kama ombaomba.
Hayo ndiyo Mambo muhimu ya kujifunza kwa leo kutoka kwa Benjamin Franklin. Naamimi umepata hata kitu kimoja cha kufanyia kazi.
[mailerlite_form form_id=1]
One response to “Nguvu Ya Kuwa Na Ratiba Na Mambo Matano Ya Kujifunza Kutoka Kwa Benjamin FranklinKila Mara nimekuwa”
Spectacular