Aina Tano Za Ujuzi Unaouhitaji Ili Uweze Kufikia Malengo Yako


Watu wengi wanadhani kuwa ukiweka malengo tu basi kinachofuata inakuwa ni tiketi ya wewe kuyafanikisha. Siyo hivyo. Kuna vitu vinahitajika ili kukusaidia wewe kufanikisha malengo yako. Na kwa leo nitakushirikisha aina tano za ujuzi unaouhitaji ili uweze kufikia malengo yako.

1. Unahitaji ujuzi wa kuweka malengo sahihi. Siyo kila lengo ni sahihi kwako. Na siyo kila njia unayoitumia kuweka malengo ni sawa.

Malengo mazuri yanapaswa kueleweka.
Yanapaswa kuwa yanapimika
Yanapaswa kuwa yanafikika
Yanapaswa kuwa yanaendana na ndoto au kusudi lako la maisha.
Yanapaswa kuwa na ukomo au muda ambapo yatakamilika.

SOMA ZAIDI: Hatua Muhimu Katika Kuweka Malengo

2. Unahitaji ujuzi wa kuchukua hatua.
Baada ya kuweka malengo haitoshi tu wewe kuendelea kushikilia kuwa una malengo badala yake unapaswa kuchukua hatua ili uweze kuyafikia hayo malengo yako.

3. Unahitaji ujuzi wa kuyaandika malengo yako kila siku.

Kila siku na kila Mara jikumbushe malengo yako, Kisha tafuta namna ambavyo utafanya kitu kuhakikisha lengo au malengo uliyoweka, unayafikia.

4. Unahitaji ujuzi wa kuwashawishi watu washirikiane na wewe au wakusaidie kufanikisha lengo lako. Ni wazi kuwa katika safari  ya kufanikisha malengo yako, huwezi kutembea peke yako, unahitaji watu na hapo ndipo unahitaji kuwa na ujuzi wa kuwashawishi watu ili waweze kukusaidia kwenye Safari yako.

5. Unahitaji ujuzi wa kunga’ang’ania kile unachofanya mpaka pale utakapokikamilisha au kukipata.

Kila la kheri.

 

Najua kuwa ungependa kupata ushauri wa karibu zaidi moja moja kwa moja kutoka kwangu. Nitafute tuone ni lini nitakuwa na muda, ili nikupangie ratiba ya kuongea na wewe. Utalipia kiasi kidogo tu.

Saa moja ni laki moja mazungumzo kwa njia ya mtandao.

SAA MOJA NI LAKI MBILI NA NUSU MAZUNGUMZO YA ANA KWA ANA. Malipo yanafanyika kwanza, kisha unapewa tarehe (appointment) tutakapoweza kuongea

Tumia namba ya simu +255 755 848 391 kuwasiliana nami.

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.

Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa

Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com

Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana naye kwa +255 684 408 755 na orodha ya vitabu vyenyewe unaweza kuiona HAPA. Chagua unachopenda, kisha twanga,  +255 684 408 755

Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396

For Consultation only: +255 755 848 391  au godiusrweyongeza1@gmail.com

Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza

Hakikisha Umesuscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

kila la kheri


4 responses to “Aina Tano Za Ujuzi Unaouhitaji Ili Uweze Kufikia Malengo Yako”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X