Kuna nyakati ndoto na malengo yako yanahusisha watu wa nje. Yanahusisha taasisi za serikali, makampuni fulani au hata mataifa mengine ambayo yana taratibu zake, utendaji kazi wake na kila kitu cha kwake. Watu hawa utakuta kwamba wana njia zao kutenda na kushughulika na vitu vyao katika namna ambayo inaweza isiwe rafiki kwako. Kwa mfano, unaweza kuwa na haraka ya kusajili kampuni yako au chuo chako, ila ukakuta kwamba taasisi inayo husika haioni umuhimu wa kukufanyia kile unachohitaji kwa wakati na wakati mwingine ukasumbuliwa bila ulazima wowote.
Unaweza ukawa unahitaji leseni yako ya udereva ili ikusaidie kutimiza jambo fulani ulilonalo kwenye mpango wako na malengo yako, ila ukakuta kwamba watu wanaohusika hawana haraka na wala hawajali kukupatia leseni yako kwa wakati hata kama umekidhi viwango vyote ambavyo unastahili kuwa navyo.
Katika hali ya kawaida watu wa aina hii wanakukwamisha na hata kukufanya ushindwe kufanikisha vitu vyako kwa wakati. wakati mwingine unaweza kuwa hata na watu ambao umewaajiri ila wakawa pia hawaelewi kile unachotaka na hivyo kuzidi kukudidimiza. Sasa zifuatazo ni njia za kukusaidia wewe kuwasiliana na watu wa aina hii ili wakufanyie mpango wako kwa wakati;
Kwanza, waeleze watu hao mpango wako mkubwa ambao unataka kuufanyia na muda ambao ungependa mpango huo uwe umetimia.
Ukiwaeleza watu mpango wako ambao ungependa ufanyiwe kazi ni wazi kuwa watu hao wanakuwa tayari kusaidia na kushirikiana na wewe. Muda mwingine badala ya kuonesha kwamba ndoto au lengno ni la kwako binafsi, unapaswa kulionesha kama vile lipo kwa ajili ya wakusaidia awao pia. Wape na wao lengoambalo watashirikiana na wewe kulifanyia kazi.
Hiki kitu kimenifanya nikumbe stori moja ya namna watu walivyopunguza idadi watu waliokuwa wanakojoa juu chooni. Ni kwenye uwanja wa wakimataifa wa…
Kulikuwa na tatizo kubwa hasa kwenye choo cha wanaume, ambapo mara nyingi walikuwawnakojjoa juu ya choo obadala ya kukojoa ndani. Sasa kilichofanyiaka ilikuw ani kuchora kitu kilichoonekana kama nziri kwenye sinki la choo.
Kila aliyekuwa anaingia kwenye kile choo alikuwa anatamani kumwongooa yule nzirr kwenye sinki na hivyo aakawa anamlenga. Baada ya muda idadia ya wtu waliokuw wanakojoa juu ya choo walikuw wamepungua.
Pili fahamu kuwa hauko kwenye mchezo huu kwa muda mfupi, ni mchezo ambao unaenda kuucheza kwa muda mrefu. Hivyo wewe kama wewe utapaswa kwenda vizuri, usibabishe fujo, usimdhuru mtu wa kudhulumu mtu kwa maana haufanyii hiyo ndoto kwa ajili ya kupata hela ya kula leo hii na kesho yake utaenda eneo jingine. Kwa ko hicho ni kitu ambacho unakifanya kama sehemu ya au kifanikiwe au ufe ukiwa unapambana nacho.
Nne, fahamu kuwa watu wote wanaostahili kulipwa stahiki zao, utapaswa kuwalipa stahiki zao kwa wakati bila ya kuchelewa. na hawa watu ni wazi kuwa siyo tu kwamba utataka wakufanyie kazi kwa siku moja au mbili, hawa watu unaweza utawahitaji leo na kesho.
Tambua mchango wa kile mtu ambaye anahusika kwenye kufanyia kazi ndoto yako na hakikisha huyo mtu anajua kwamba, yeye yana mchango kwako. hata hivyo, uwe makini watu wasije wakatumia hicho kipengele kwa ajili ya kukunyanyasa hasa wakijua kwamba mchango wao ni wa kipekee.
Wafanyakazi wako wajue kuwa ni watu wa muhimu kwenye kazi au biashara yako, ila pia wajue kuwa wakienda kinyume na taratibu hutaweza kuwavumilia.
Fahamu kuwa wewe unaweza kushinda kwa kufanyia kazi ndoto yako na mwingine akashinda kwa kuifanyia kazi ndoto yake. Usitake kabisaa kumuumiza mtu ili wewe uende mbali zaidi. badala yake penda kuwainua wengine maana kadiri wengine wanavyoinuka na wee unazidi kuinuka. Ndio maana mimi napenda nikuelimisha haya mabo uyafahamu maana nafahamu kuwa wewe ukiinuka, na mimi nitaweza kuinuka.
Tafuta mtu wa kushughulika na changamoto nyingine ili wewe uwekeze nguvu zako kwenye mambo ya maana zaidi.
Pia wenye ulimwengu wa sasa hivi ndoto yako inapasawa kuwekwa mtandaoni, sasa unapaswa kupambana na kuiweka
umekuwa nami rafiki yako wa ukweli
Godius Rweyongeza
0755848391
morogoro-Tz
One response to “Kitu Cha Kufanya Ndoto Yako Inapohusisha Watu Wa Nje”
[…] KWANZA UNAPASWA KUIJUA NDOTO YAKO KWA KINA […]