KUTOKA KWENYE AJIRA MPAKA KUJIAJIRI


Nakumbuka juzi nilikushirikisha safari ambayo unapaswa kuifuata ili uweze kujiajiri kama umeajiriwa kwa sasa. leo hii naomba kuendelea tena kwa kukushirikisha vitu zaidi kwenye suala zima la ujasiriamali na kujiajiri.  Na leo ninakushirikisha machache niliyopata kutoka kwenye kitabu cha Employee To Entrepreneur

Moja ya ushauri ambao umekuwa unatolewa kwa watu wengi ni ushauri wa kwamba unapaswa kwenda shuleni, kusoma kwa bidii ili hatimaye uweze kuajiriwa kwenye kampuni au serikalini ambapo utaajiriwa na kulipwa vizuri.

Ushauri huu umefanya vizuri hasa kwenye karne ya 20 ambapo nguvu kazi ilikuwa ikihitajika zaidi kwenye viwanda na maeneno mengine. Hata hivyo kwenye zama hizi kuna mabadiliko kidogo.

Kuna kazi ambazo zilikuwa zikifanywa na watu sasa hivi hazifanywi na watu tena. Lakini bado ushauri wa kwamba unapaswa kwenda shuleni na kusoma kwa bidii ili hapo baadaye uweze kuajiriwa umekuwa ukiendelea kutolewa.

Japo ujasiriamali unaonenaka ni njia nzuri na ambayo naweza kubadilisha maisha ya watu wengi, ila sasa wengi wanashindwa kuufanya. Na moja ya sababu  kubwa inayowafanya watu washindwe kujihusisha na ujasiriamali ni kwa sababu ili uwe mjasiriamali unahitaji mabadiliko kwenye akili yako.  Ebu fikiria hili. Tangu umezaliwa ulikuwa ukiambiwa kwamba ili uweze kuishi maisha mazuri unapaswa kuwa na kazi ambao itakulipa vizuri. Lakini sasa cha kushangaza ni kwamba unapohitimu chuo unakuta kwamba ajira hamna.

Kwa wengi ni vigumu sana kubadili akili zao na kujiingiza kwenye ujasirimali na hilo linafutanya tuje kwenye pointi yetu ya kwanza kwa siku ya leo ambayo

#1. ILI UWE MJASIRIAMALI UNAPASWA KUBADILI FIKRA ZAKO

Unapaswa kubadili fikra zako ili uweze kujiingiza kwenye ujasiriamali. Watu wengi hawapendi ujasirimali kwa sababu ujasiriamali unahusisha kuanguka na kushindwa. Hakuna mtu ambaye anapenda kushindwa na kuanguka.

Na watu wanaogopa kushindwa kutokana na fikra zao walizonazo. Linapokuja suala zima la fikra kuna watu wa aina mbili. kuna watu wenye fikra mgando na kuna watu wenye fikra za ukuaji.

Watu wenye fikra mgando ni wale ambao wanafikiri kwamba haiwezekani kufanyika  kitu chochote kipya. Ndio wale utakaowasikia wakikwambia hakuna jipya chini ya jua au kila kitu kilishagunduliwa.

Hata hivyo watu wenye fikra za ukuaji wenyewe wanaangalia ni kwa namna gani ambavyo wanaweza kukua zaidi kutoka hapo walipo. Wapo tayari kujifunza na kuchukua hatua. Wakianguka wanaona hilo kama somo ambalo wanaenda kulifanyia kazi kwenye maisha.

Ujasiriamali unahitaji fikra za ukuaji. Kwa sababu kwenye ujasirimali kuna kuna vitu vingine ambavyo mwanzoni unaweza kuwa unafikiri kwamba ukivifanya mara moja tu vitafanikiwa, ila ukienda kuvifanyia kazi kwenye uhalisia ukakuta kwamba mambo ni tofauti.

Ndio maana watu wengi huwa wanaanza kufanya vitu vipya lakini baadaye wanaishia njiani. Unajua kwa nini?

Kwa sababu ujasirimali unahitaji kujitoa kwelikweli. Na unapaswa kuwa tayari kupokea mabadiliko ambayo yanatokea kwenye ulimwengu wa leo.

#2 JUA KUSUDI LINALOKUFANYA UINGIE KWENYE BIASHARA

Huwa napenda sana kutolea mfano wa wachezaji wampira wa miguu. Kuna baadhi ya vyakula hawawezi kula hata kama vinapendwa na watu wengi kwa sababu tu wao ni wachezaji wa mpira wa miguu. Wanajua kabisa sili hiki chakula kwa sababu nataka nitimieze kusudi langu ambalo ni hili.

Usipokuwa na kusudi kwenye biashara unayumbishwa. Wewe pia unapoingia kwenye ujasiriamali unapasaw kuwa na kusudi kubwa ambalo linakusukuma wewe.

Ni kitu gani kinakusukuma kuanzisha biashara. Kama lengo kubwa ni fedha utajikuta kwamba unakwama kwa sababu msukumo wa fedha peke yake hautoshi kukufanya uweze kusonga mbele na kufanya makubwa zaidi.

Msukumo kama

Kupata uhuru binafsi

Uhuru wa kifedha

Familia

Kuwasaidia wazazi

Hii inaweza kuwa ni msukumo mzuri wa kukufanya uzidi kusonga mbele.

Kwa hiyo ni muhimu kwako kujiuliza hivi ni kweli nina msukumo mzuri kutoka ndani ambao unanisukuma

#3. KUSANYA MAWAZO MBALIMBALI KISHA TENGENEZA WAZO LAKO

Najua kuna nia mbalimbali za kupata mawazo ya bisahara, ila kwa leo nataka nikueleze hii njia ambayo unaweza kuitumia kama unataka kutengeneza wazo la kipekee kwenye biashara. Njia hii ni kuangalia vitu ambavyo tayari vipo kisha kujenga kitu kipya na cha tofauti kutokana na hivyo vitu ambavyo vipo.

Siyo lazima mara zote uje na wazo jipya na la kipekee sana. ila unaweza kutumia vitu ambavyo vipo kwa sasa kujenga wazo jipya na la kipekee

#4. JARIBU WAZO LAKO KWA WACHACHE WA MWANZO KABLA YA KUWEKEZA FEDHA NYINGI

Badala ya kuwekeza fedha zako kutengeneza bidhaa na kuileta sokoni. Anza na kuleta bidhaa yako kwa watu wachache wa kwanza, kisha baada ya hapo utawekeza zaidi.

#5. UTUMIE MUDA WAKO VIZURI

Kwa siku mtu wa kawaida anasemekana kugusa simu mara 2617. Na mara nyingi sio kwamba kunakuwa na kitu cha maana ambacho mtu huyu anafanya, badala yake unakuwa ni upotezaji wa muda tu mtandaoni kwenye makundi ya whatsap na maeneo mengine.

Sasa unachopaswa kufanya wewe ni kuhakikisha kwamba unautumia muda wako vizuri. Usitumie muda wako mwingi kwenye mambo ambayo hayana manufaa. Wekeza muda wako na hasa unapouwa kwenye hii safari ya kutoka kwenye ajira kwenda kwenye kuajiriwa.


5 responses to “KUTOKA KWENYE AJIRA MPAKA KUJIAJIRI”

  1. Ni somo zuri hakika. Ahsante sana kaka kwa kuleta majibu ya maswali ambayo wasomi wengi yanatuumiza vichwa. Yeyote atumiae maarifa haya, ni hakika atabadirisha maisha yake kwa kuwa bora zaidi kila iitwapo leo. Hongera sana.

  2. Mungu akubari kwakuumiza kichwa ilikusaidia wengine nimim rafikiyako Omar Hussein hassain ambae unanitumianga vitabu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X