Maisha Ni Wajibu Wako


Kama kila mtu akijenga utaratibu wa kuona maisha Kama wajibu wake tutafika mbali unajua kwa nini? Kwa sababu, ukianza kuona maisha kama wajibu wako utapambana kwa hali na mali kuweka kila Kitu sawa. Hutakuwa tena na muda wa kumlalamikia mtu KUWA Kitu fulani hakijakaa sawa au hakijafanyika.

Unatumia mitaji hii kupata fedha, ambayo baadaye unaweza kuitumia kufanya kitu Cha maana.

Napenda sana ule usemi wa Martin Luther King Jr. Anaosema kuwa kama kila mtu akifangia barabara dunia hii itakuwa safi Sana. Yaani, ebu fikiria hivi, kama kila mtu mtaani mwake akifagia mazingira yanayozunguka ya nyumba yake tu. Si mtaa wote utapendeza ndani ya siku moja? Si ndio?.

Sasa na kwenye hili suala zima la ajira. Kama kila mtu akisema ngoja kwanza nipambane na hali yangu. Nifanye kile kinachoweza tu. Niamini mimi, ndani ya miaka mitano mpaka kumi tuna uwezo wa kutatua tatizo hili la ajira.

Bado huamini tu? Sikiliza, kama kwa mfano wewe ulisema kwamba kuanzia leo, nitapambana nipate elfu mbili, elfu tatu, nne au tano na kuiweka akiba. Kila siku. Naamimi, kuwa baada ya miaka mitano, akiba yako hii ya elfu 2 kila siku. Itakuwa imekufikisha mbali. Tena siyo mbali kidogo, mbali sana tu.

Hii ndio Dhana nzima ya kuona maisha Kama wajibu wako. Na siyo wajibu wa MTU mwingine. Siyo wajibu wa mjomba au babu!

unahusika wewe mwenyewe bila kumtulia mtu lawama au kumtegemea mtu.

Sikiliza, kuanzia leo hii, Anza kujitegemea.

Usilalamike wala kumtupia mtu yeyote yule lawama. Kukitokea tukio. Jiulize ninahusikaje hapa kulitatua. Kama lipo nje ya uwezo wako achana nalo. Pambana na kile kilicho ndani ya uwezo wako.

SOMA ZAIDI: Hivi Ndivyo Unaweza Kufanya Mishale Inayolenga Kukuangamiza Kuwa Baraka

Kama umependa makala hii, utapenda pia Makala ninazotuma kwa njia ya baruapepe. Jiunge na mfumo wetu wa kupokea Makala kwa njia ya baruapepe kwa kujaza taarifa zako hapa chini


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X