Kwa nini hufikii ndoto zako


Umekuwa na ndoto kubwa Ila bado hazifanikiwi? Unajua kwa nini?

Najua kwa asili sisi ni viumbe wenye ndoto kubwa. Ndio na hili naweza kuliona kwa watoto wadogo. Maana mtoto mdogo haogopi kusema waziwazi kuwa siku moja atakuwa daktari au kuwa siku moja atakuwa rubani. Mtoto akiona ndege anasema ni ya kwangu au ya baba yangu kwa sababu yeye kwa asili ni mtu AMBAYE ana ndoto kubwa. Anafahamu kuwa hakuna kitu chochote kile kinaweza kumzuia kufikia ndoto zake. Anajua kwamba anaweza kuwa anachotaka.

Wewe pia najua una ndoto kubwa. Unaweza kuwa umezikatia tamaa, ila najua unazo. Si ndio? Walau ndoto ya kuwa fedha nyingi utakuwa nayo.

Ila tu tofauti na watoto wadogo ambao wao wanatamka waziwazi kuwa wanataka kufikia ndoto fulani, wewe unaogopa kusema ndoto yako mbele ya watu.

Kwani uongo? Wewe mara ya mwisho kusema mbele ya watu juu ya ndoto yako kubwa ni lini?

Kama tu unaogopa kuwaambia watu kuwa una mpango wa kujiajiri na kutoka ajirani, unadhani utawaambia hizo ndoto nyingine?

Kama tu unaogopa kuwaambia kuwa unataka kujiajiri baada ya chuo na hutaki kusikia kabisa habari ya ajira. Unadhani Sasa utadhubutu kuwaambia kuhusu hiyo ndoto nyingine?

Halafu mimi, niache uchokozi! Kwa nini nakuchokoza hivyo lakini? Hahaha, Ila na wewe ujirekebishe bwana, unaogopa kusema hata ndoto zako! Unazidiwa na mwanao……

Halafu unategemea uzifikie. Usipozifikia,unaanzaa kusema aliyekupa wewe ndiye kaninyima mimi. Hahaha!

Sasa ebu tuendelee tuone mambo mengine muhimu yanayokwamisha watu na kuwafanya washindwe kufikia ndoto zao na hasa yanayokukwamisha wewe.

Kutokuwa na utaratibu wa kujikumbusha ndoto zako kubwa mara kwa Mara. Bilionea Richard Branson aliwahi kunukuliwa  akisema, mabilionea ni watu wanaojikumbusha ndoto zao mara nyingi kwa siku.
Huku watu wa kawaida wakiwa hata hawajikunbushi kuhusu ndoto zao.

Wewe Leo ulipoamka asubuhi umejikunbusha ndoto zako kubwa. Au ndio umefungua Instagram.

Huwa kuna kichekesho kuwa mtu anaamka asubuhi. AKIWA HAJAJUA HATA KAMA ANA MIGUU YAKE, ILA TAYARI YUPO FACEBOOK NA INSTAGRAM.

Sasa sijui huyu mtu wa aina hii ni wewe? Halafu unataka ufikie ndoto kubwa? Rafiki yangu EBU FIKIRI TENA.

KINGINE kinachokuzuia kufikia ndoto zako Ni kukata tamaa mapema.
Unapoanza kufanyia kazi ndoto zako, unapaswa kujitoa haswa kufanyia kazi ndoto zako. Muda mwingine matokeo unayotaka hayatokei haraka. Yanachukua muda. Ukikata tamaa mapema hivyo utashindwa kufikia ndoto zako zote.

Hiki kitu kinaweza kukufanya ufanye Mambo meengi Ila mwisho wa siku matokeo yawe ni SIFURI. Kuna wazee wetu unakuta wameupiga mwingi ila hawakupiga hatua kubwa kimaisha. Utakuta mzee anakwambia niliwahi kufanya kazi fulani, nikafanya na kazi fulani, nikaenda eneo fulani n.k.

Nisikilize mimi: suala siyo kuupiga mwingi. Suala ni je, unaupiga mwingi kwenye kitu gani? Ukiupiga mwingi kwenye kila kitu utajikuta hufiki sehemu yoyote maishani mwako. Ila ukiupiga mwingi kwenye ndoto yako kwa muda mrefu. Kutoboa lazima tu!

Looo! Kumbe napaswa kuendelea na pointi nyingine halafu mimi nimekazana kuandika kuupiga mwingi. Kama vile kuupiga mwingi Ni pointi ya msingi kwenye makala ya leo.

Halafu mimi…..

Umeanzia juu kwenye ndoto yako
Umewahi kuona hili. Unakuwa na ndoto kubwa kiasi kwamba unaanzia juu sana. Kuanzia juu siyo kitu kibaya. Ila Sasa tatizo ni pale ambapo unakutana na changamoto ambazo wewe mwenyewe unashindwa kuzihimili.

Muda mwingine ni vizuri kuanzia kidogo, kisha ukaendelea kukua. ila hata ukigundua kwamba ulianzia juu na sasa mambo yamekuwa makubwa, unaweza kuamua kushuka chini kidogo ili uweze

Mambo mengine yanayokukwamisha wewe kufikia ndoto zako nimewahi kuyaeleza kwenye video hii fupi kwenye channel yangu ya youtube. naomba uiangalie pia maana ina vitu vikubwa na vya msingi sana. Uisahau kuSUBSCRIBE kwenye channel yangu.

JIUNGE NA MTANDAO HUU

* indicates required Email Address * First Name Last Name Phone Number


One response to “Kwa nini hufikii ndoto zako”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X