Milionea Ni Nani?


Milionea ni mtu anayemiliki rasilimali zenye thamani ya milioni moja.

Kutokana na thamani za fedha kutofautiana, kwa sasa kipimo kinachotumika kupima umilionea ni dola ya Marekani.

Kwa hiyo ukisikia wanasema fulani ni milionea, ujue ni kwa thamani ya dola za Marekani.  Hii ndio kusema kwamba unaweza unaweza kuwa na rasilimali zenye thamani ya milioni moja kwa fedha za Tanzania ila usiwe milionea kwa sababu kipimo kikuu kinachotumika kwa sasa kupima umilionea ni dola za Marekani.

Milioni moja ya shilingi za Tanzania kwa sasa ikiwekwa kwenye dola za Marekani ni sawa na dola mia nne thelathini na mbili. Kwa hiyo, ukiwa na milioni moja ya kitanzania unakuwa hata hujafikisha utajiri wenye viwango hata maelfu!

Ili uwe milionea kwa kipimo cha dola unapaswa kuwa na rasilimali zenye thamani ya shilingi za Tanzania bilioni 2.3

Napenda kusisitiza tu kuwa kipimo kinachotumika Utajiri kwa watu wote ni kimoja ili kusiwepo mchanganyiko. Kwacha ya Zambia ina thamani kidogo ukilinganisha na shilingi ya Tanzania. Na shilingi ya Tanzania ina thamani kidogo ukilinganisha na shilingi ya Kenya.
Shilingi ya Kenya ina thamani kidogo ukilinganisha na Rand ya Afrika kusini.

Sasa ebu fikiria milionea kwa thamani ya fedha za Zambia, Kenya, Tanzania, Afrika Kusini na Marekani watakuwa sawa endapo kila nchi itatumia sarafu yake kupima umilionea?

Ndio maana kinatumika kipimo cha aina moja kupima Utajiri wa watu wote duniani. Kwa sasa dola ndiyo inatumika kama siku zijazo kutakuwa na mabadiliko tutajuzana.

Jinsi umilionea unavyopimwa

Umilionea (UTAJIRI)= THAMANI YA RASILIMALI-MADENI YOTE.

Wewe mwenyewe pia unaweza kupima thamani ya utajiri wako kwa kuchukua thamani ya rasilimali zako kisha ukatoa madeni yote unayodaiwa.

Chukua thamani ya mali zako kwa sasa kama ungekuwa unaziuza kisha toa madeni.

Je,milionea ana fedha zote mfukoni.

Kwa sasa hivi umilionea unapimwa kwa kiwango cha thamani ya rasilimali ulizonazo baada ya kutoa madeni. Mamilionea wengi wamewekeza kwenye makampuni au rasilimali zisizohamishika (kama nyumba, ardhi,) au wamewekeza kwenye soko la hisa (hisa, hatifungani na vipande), hivyo milionea hana fedha taslimu mfukoni mwake. Utakuta ana fedha za kawaida tu za kumtosha kufanya mambo yake yote muhimu ila hana milioni zote za fedha taslimu mfukoni.

Ila mali zake zote zikiuzwa kwa thamani ya wakati husika zina uwezo wa kufikia milioni husika.

HAKIKISHA UMESOMA KITABU CHANGU CHA MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE ili ujifunze zaidi kuhusu UWEKEZAJI. Kinapatikana kwa elfu tano tu, irushe kupitia 0755848391 Jina ni GODIUS RWEYONGEZA ili nikutumie ebook.

Nawezaje kuwa milionea?

Watu wanakuwa mamilionea kwa kurithi
Au kwa kupambana wenyewe.

Kama huna sehemu ambapo utarithi umilionea basi utapaswa kupambana mwenyewe.

Ili kuwa milionea utahitaji kuweka kazi sana na kwa muda mrefu. Utahitaji kujipa muda, maana umilionea hauwezi kutokea ndani ya siku moja. Unahitaji muda, kazi, KUWEKEZA, kuanguka na kusimama tena.

SOMA ZAIDI: Hii Ndio Siri Kubwa itakayokusaidia kutengeneza fedha Nyingi

Je, ni kazi gani inaweza kunipa umilionea?

Niwe tu mkweli, hakuna kazi inayokulipa mshahara inavyoweza kukupa umilionea.
Ili ufikie umilionea utapaswa kuwa na biashara na (au) kufanya uwekezaji.

Kwa sasa ya mamilionea, wengi wanatoka kwenye sekta mbalimbali ila Kuna sekta 11 zimejitokeza  kuwa mamilionea wengi.

Nashauri upate ebook yangu ya SEKTA 11 ZA KUTENGENEZA MAMILIONI YA FEDHA TANZANIA ili ujue maeneo sahihi unapoweza kuwekeza fedha zako. Haya ni maeneo mazuri pia unavyoweza kuanzisha biashara ya kukupelekea kwenye umilionea.
Ebook hii inapatika kwa elfu tano (5,000/-) tu. Rusha elfu tano (5,000/-) kwa 0755848391 jina ni GODIUS RWEYONGEZA ili nikutumie ebook hii.

Mamilionea Wa Tanzania

Wengi wa wale wanaojiita mamilionea kwa Tanzania siyo mamilionea!  Hauwi milionea kwa kupokea mshahara wa milioni moja kwa mwezi. Rafiki yangu Kama wewe mshahara wako ni milioni, usijidai kuwa sasa wewe ni milionea. Umilionea ni viwango vingine kabisa kama ambavyo tumeona.

Kama kwa mwezi unapokea mshahara wa milioni moja utahitaji mishahara ya aina hiyo mara elfu tatu (3,000) ili ufikie umilionea. Mishahara ambayo huwezi kuipokea kipindi cha maisha yako yote!

Kwa hiyo  umilionea ndio haiwezekani kabisa?
Hapana. Siyo kwamba haiwezekani, ngoja nikupe mbinu ya kutengeneza kufikia umilionea.

Ukitengeneza bidhaa inayouzwa kwa dola moja moja. Ili uwe milionea unapaswa kuiuza kwa watu milioni moja na unapaswa usitumie hiyo fedha. Hahaha.

Ukiuza bidhaa hiyohiyo kwa dola mbili basi utapaswa kuiuza kwa watu laki tano.

Ukiiunza kwa dola kumi maana yake utapaswa kuiuza kwa watu laki moja.

Ukiwa na bidhaa mbili za aina hiyo maana yake utapaswa kuziuza kwa watu elfu hamsini mara mbili. Ukiwa na bidhaa tatu, utaziuza kwa watu elfu 33.3 mara tatu.

Kwa hiyo wewe, unaweza kuangalia namba ipi unaweza kupambania.

Kama nilivyoeleza hapo mwanzo. Umilionea siyo kitu cha kulala na kuamka ukiwa umekifia. Ni kitu kinachukua muda.

Mamilionea wengi wamefikia kiwango cha umilionea baada ya kufanya kazi kwa miaka 10 au zaidi.

Kwa hiyo nikate tamaa ya kupambania ndoto yangu ya umilionea kwa sababu unachukua muda kuufikia?

Unachopaswa kufahamu ni kuwa miaka 10 inaenda kupita. Sasa ikipita ni au utakuwa umeitumia kwa manufaa au umeitumia hovyo. Kama umeitumia kupambania ndoto yako ya umilionea utakuwa umepiga hatua kubwa sana hata kama utakuwa haujaufikia umilionea, Ila utakuwa umefika mbali.

Ila ukikata tamaa hata kabla ya kuanza. Ni wazi kuwa hata ulakionea utakushinda. Utashindwa hata kuwa elfunea, hahaha.

Kwa Tanzania miaka 10 ni mhura wa utawala wa rais. Kwa hiyo, rais ukiamua kupambana rais anapoingia madarakani mpaka anapotoka, unaweza kuufikia umilionea kwenye mhura wake.

JE, UNA MPANGO WA KUWA MILIONEA?
karibu ujiunge na kundi letu la THINK BIG FOR AFRICA.

BONYEZA HAPA KUJIUNGA.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X