Hii Ndio Siri Kubwa itakayokusaidia kutengeneza fedha Nyingi


Unataka kijua ni kwa namna Hani unaweza kutengeneza fedha Nyingi zaidi ya unavyotengeneza sasa hivi?

Umechoka na kipato chalo cha Sasa, ungependa kutengeneza kipato kikubwa zaidi ya unavyotengeneza Sasa?

Ndio Kuna njia. Na njia hii Ndio ninaenda kukueleza leo kwa umakini na kwa lugha rahisi sana.

Kwanza Anza na kufuatilia hesabu za fedha zako zinazoingia na zinazotoka. Hakikisha unaandika kila fedha inayoingia na kila fedha inayotoka.

Pili, hakikisha hautumii fedha zaidi ya Ile unayoingiza. Mtu ambaye anaingiza elfu kumi na kutumia elfu tisa mia tano, yuko kwenye nafasi kubwa ya kuwa tajiri ukilinganisha na mtu anayeingiza elfu 10 na kuitumia elfu kumi mia tano.

Tatu, hakikisha kwa kila fedha inayoingia unatoa kiasi cha kuweka akiba. Usidharau hili hata kama fedha uliyopokea ni kiwango kidogo sana.

Nne, Usikope kwa ajili ya matumizi yako binafsi. Kiufupi Usikope

Tano, kuwa na ndoto kubwa za kufikia kifedha. Iwe ni kuwa milionea au bilionea au kupata uhuru wa kifedha.

Sita,  wekeza fedha unayopata ili ikufanyie kazi. Ukifanya kazi ili upate fedha wewe ndiye unakuwa unaifanyia kazi fedha.
Ukiwekeza fedha yako, wewe ndiyo inakufanyia kazi. Jitahidi ujue kitu hiki kidogo kinachoitwa UWEKEZAJI,  kitakusaidia sana.

Kuujua UWEKEZAJI anza kwa kusoma kitabu cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE, rusha elfu tano tu ili upate kitabu hiki


2 responses to “Hii Ndio Siri Kubwa itakayokusaidia kutengeneza fedha Nyingi”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X