Uhuru wa kifedha ni pale ambapo unakuwa na fedha za kukutosha kwa kutumia kipindi fulani.
Kama wewe matumizi yako kwa siku ni shilingi elfu tano. Ukiwa na milioni moja maana yake utakuwa na uhuru wa kifedha wa siku 200.
Ila ukiwa na shilingi milioni moja na matumizi yako kwa siku ni laki moja maana yake wewe una uhuru wa siku 10 tu.
Uhuru kamili wa kifedha ni pale unapokuwa na fedha ya kukutosha wewe kutumia maisha yako yote hata kama hutafanya kazi.
Unapokuwa na uhuru kamili wa kifedha, unakuwa hulazimiki kufanya kazi tena.
Hii ndio kusema kwamba kama kwa siku unatumia shilingi elfu tano kwenye matumizi yako, wewe unakuwa na elfu tano na zaidi za kutumia maisha yako yote. Fedha inapaswa kuwa zaidi ya ile unayotumia kwa sababu kila mwaka kuna mfumuko wa bei unaotokea.
Jinsi ya kutengeneza uhuru wako wa kifedha
Ili kutengeneza uhuru wako wa kifedha, utapaswa kwanza kujua kiwango kamili cha fedha unachohitaji kupata. Kiwango kinapaswa kuwa kikubwa pengine kufikia umilionea au ubilionea.
Mahitaji yanatofautiana kati ya MTU mmoja na mwingine.
Baada ya hapo anza kuweka kazi ili ufikie uhuru kamili wa kifedha ambao kiuhalisia unahitaji muda kufikia.
Unahitaji pia kuweka kazi ya kutosha
Unahitaji kuzalisha thamani na kuwapa watu kile ambacho wao wanataka.
umeshajiunga na THINK BIG FOR AFRIKA wewe?
Jiunge na kundi letu maalumu la WhatsApp HAPA. Tutakutumia mafunzo kwa email pia