Usidharau fedha hata kama ni kidogo


Leo nataka ni kwambie kwamba fedha siyo kitu ambacho unapaswa kudharau.

Unaweza kukuta mtu ana fedha kiasi fulani ila akawa anakidharau.

Na hata akakitumia hovyo, ila unachopaswa kufahamu ni kuwa usidharau fedha.

Hivi hujawahi kujiuliza kwa nini Mo Dewji na utajiri wake wote kwa nini bado anaendelea kutengeneza hadi viberiti?

Kiberiti kimoja huku mtaani tunakinunua shilingi mia moja, ambayo kiuhalisia ndiyo fedha ndogo. ila jamaa na ubilionea wake wote bado anatengeneza viberiti. Kiufupi Mo anauza viberiti.

Na yeye hadharau fedha ndogo kwa sababu anajua kwamba fedha haina udogo, ubilionea haukamiliki bila ya kiasi hicho kidogo.

Sasa kazi ni kwako kuanzia leo hii kuhakikisha kwamba unaanza kujenga nidhamu kwa fedha yako hata kama ni kidogo.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X