Watu ambao wanapata wazo  bora la biashara huwa wafanya hivi


Usije ukafanya kosa la kukaa chini, na kuanza kusubiri upate wazo bora. Wazo bora halipatikani kwa kukaa chini n akuumiza kichwa.

Muda mwingine wazo bora linapatikana kwa kufanya kazi.

Ebu kwa mfano, hakuna mtu ambaye alikaa na kuumiza kichwa ili aje na wazo la tairi. Ugunduzi wa taili ulikuwa ni miongoni mwa mapinduzi makubwa, ambayo yalifanyika kwa wakati huo,mpaka sasa hivi. ila hakuna mtu alikaa chini na kuumiza kichwa, kisha akatengeneza taili.

Watu walipata wazo la taili katika kufanya kazi. kadiri walivyokuwa wanafanya kazi na kufeli na kuinuka ndivyo walikuwa wanakuja na wazo bora zaidi. inawezekana labda taili la kwanza lilikuwa ni la pembe nne.

Au fikiri kuhusu wazo la uchapaji wa vitabu. Hakuna ambaye alikuja na wazo bora lililokamilika la kuchapa vitabu. sote tunajua kwamba uchapaji wa vitabu wa zamani na wa sasa hivi ni tofauti. Ila haya maboresho tunayoyaona sasa hivi ni kutokana na watu waliokuwa tayari kufanyia kazi kile walichokuwa wanafikiri mwanzoni, wakakiboresha kadiri walivyokuwa wanaendelea mpaka wwe unalifahamu kama lilivyo. Hivyo, basi, usije ukakaa na kusubiri upate wazo bora na la kipekee ambalo halijawahi kutokea hapa duniani.

Leo hii Thomas Edison anapewa sifa nyingi sana kwenye ulimwengu wa uzinduzi wake wa taa. Ukisoma wasifu wake utagundua kwamba Thomas Edison hakuwa na wazo lililokamilika tangu mwanzo. Ila kadiri alivyokuwa analifanyia kazi ndivyo ambavyo wazo lake lilikuwa linazidi kuwa bora na kuimarika. Alijaribu mara elfu moja kabla hajapata kitu ambacho kilikuwa kinafanya kazi kwa asilimia 100.

Na wewe usije ukakaa na kuanza kusubiri wazo lako liwe bora. Anza kulifanyia kazi. utariboresha kadiri utakavyokuwa unaendelea

Ndio maana hata ukiangalia watengezaji wa simu hawatengezi simu moja na kutulia. Wanaziboresha simu kila siku, hii ndio kusema wazo la awali linaboreshwa na kufanywa kuwa imara zaidi.s


One response to “Watu ambao wanapata wazo  bora la biashara huwa wafanya hivi”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X