Wazo bora la biashara halishuki kutoka mbinguni~ Godius Rweyongeza
Moja ya kitu ambacho kimekuwa kinawakwamisha watu wengi na kuwafanya washindwe kuanzisha biashara ni wazo la biashara. Watu wamekuwa wanashindwa kupata wazo la biashara, sasa kwenye kipengele hiki ninaenda kukuonesha ni kwa jinsi gani ambavyo unaweza kupata wazo bora la biashara.
1. Wazo la biashara lipo kwenye huduma mbovu wanazotoa watu.
Kuna biashara ambazo zinafanyika kikawaida sana na watu wanapata huduma mbovu sana. Unaweza kuona hili na kuamua kuwa unaweza kuingia kwenye biashara hiyo na wewe ukatoa huduma mbovu.
2. Biashara unayoona unaweza kuunganisha teknolojia kidogo.
Hii inaweza kuwa biashara ambayo inafanyika kikawaida au biashara ambayo inafanyika vizuri ila wewe ukaona upenyo wa kuingiza teknolojia ambayo inaweza kurahisisha zaidi utoaji wa huduma na kuvuta wateja zaidi. Ukiona hii biashara unaweza kuifanyia kazi pia.
2. Unaweza kupata wazo bora la biashara kutokea kwenye matatizo yanayowakumba watu.
Matatizo yanayowakumba yanaweza kuwa fursa ya kuanzisha biashara kwako. Ukiangalia biashara nyingi zinafanyika, nyuma yake kuna lengo la kutatua matatizo ya watu.
Hospitali zipo kutatua matatizo ya watu
Migahawa ipo kutatua matatizo ya magonjwa
Mabasi yapo kutatua tatizo la usafiri. Ndio maana ukienda stendi ukakosa usafiri utaishia tu kusema hili ni tatizo kwelikweli.
Na wewe angalia lilipo tatizo, kisha jikite katika kulitatua hilo tatizo.
Matatizo ni fursa.
3. Unaweza kupata wazo bora kupitia kutembea.
Kama wewe ni mpenzi wa kutembea, basi unaweza kwenda sehemu moja na kuona biashara fulani inafanyika ila haifanyiki kwenu, basi ukaamua kuileta hiyo biashara katika mazingira yako pia.
4. Malalamiko ya watu
Ukiwa unaongea na watu utawasikia wanalalamikia huduma au kitu fulani ambacho wanaona kuwa hakifai. Kwako hii fursa ya kibiashara. Angalia Ni kwa namna gani unaweza kuyatumia malalamiko ya watu kama fursa ya kibiashara kwako.
5. Elimu, ujuzi au kitu chochote unachoweza
Elimu yako na ujuzi wako vinaweza pia kutumika kibiashara. Unaweza kutumia vitu hivi kuwahudumia watu zaidi na zaidi.
Mwanasheria unaweza kuitumia vizuri Elimu yako kuwahudumia watu zaidi
Daktari nawe unaweza kuitumia vizuri Elimu yako pia.
Kama una ujuzi wa kufyatua matofali au kutengeneza kitu chochote unaweza kuutumia huu kuanzisha biashara pia.
7. Kusoma vitabu
Vitabu ni rafiki ambaye hupaswi kumwacha, Ni rafiki mzuri unaweza kuambatana naye popote. Vitabu vina hazina ya mawazo mengi. Jitahidi kuwa unasoma vitabu mara kwa mara.
Kwa kuanzia unaweza kupata kitabu cha bure hapa
Kumbe basi, wazo la biashara halishuki kutoka mbinguni bali ni kupitia hivi vitu ambavyo tumeona hapo juu.
Umekuwa nami,
GODIUS RWEYONGEZA
Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA
Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA
Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA
Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391
kila la kheri
2 responses to “Njia 7 Za Kutumia Ili Kupata Wazo Bora La Biashara”
[…] Njia 7 Za Kutumia Ili Kupata Wazo Bora La Biashara […]
[…] Muda mwingine wazo bora linapatikana kwa kufanya kazi. […]