Ilikuwaje?
Kwa wasionijua, basi wanafikiri kwamba Godius Rweyongeza ni jitu fulani hivi la miraba minne. Lenye miaka zaidi 60+ na mabusara kama yote…
Hahaha!
Miaka sina mingi kiviiile, labda mabusara nadhani nitakuwa nayo. Ila mama yangu alinifundisha nisiwe najisifia…
Binafsi nilikuwa na ndoto ya kuandika kwa siku nyingi sana, tangu nasoma. Nakumbuka nikiwa kidato cha tatu au cha nne, niliongea na mama yangu nikamwambia kwamba nikihitimu kidato cha nne nitaandika riwaya (novel).
Baada ya kuhitimu kidato cha nne nilirudi nyumbani na kukaa miezi kama nane hivi, ila sikuwahi kuandika ile novel ya ndoto zangu…
Mama yangu alikuwa ananiuliza mara kwa mara, wewe si ulisema kwamba utaandika novel baada ya kuhitimu kidato cha nne… Nikawa namwambia ndio ila nitaandika..
Siku zikazidi kusogea… mara likizo yangu ikaisha na nikatakiwa kuanza kidato cha tano..
Hiyo nazungumzia ilikuwa ni mwaka 2013 /2014….
Kama umezaliwa miaka ya 1960… 2014 siyo mbali hata kidogo.. maana una mastori ya kuanzia uhuru mpaka leo..
Ila kama umezaliwa 2000, basi 2014 utaona ni mbali kiviile. Na hata ukipiga stori za kitambo unapiga za 2014 au 2015 wakati wazee wanajua mpaka ya vita vya Kagera… Wewe vita vya Kagera unavisoma tu vitabuni….
[birdsend form=16776]
Basi wacha niendelee…
Baada ya kuingia kidato cha tano, nilisahau kidogo kuhusu ndoto yangu mpaka baada ya kuhitimu kidato cha sita.
Sitaki nikuchose,
Baada ya kuingia chuo, niliweka lengo kuwa mpaka nahitimu chuo napaswa kuwa nimeandika vitabu 11.
Nakumbuka nilimshirikisha rafiki yangu mmoja hilo akakuna kichwa, akaniambia ungeweza kuandika hivyo vitabu,ila siyo kwa maisha ya chuo na hasa Chuo cha SUA.
Nikamwambia hicho wacha nikifanyie kazi, nikifeli, nifeli nikiwa kazini..
Nikifupisha stori zaidi ni kwamba, mpaka nahitimu chuo nilikuwa nimeandika vitabu 8. Sikuweza kuandika vitabu 11, ila walau nilikuwa nimeweza kuandika vitabu 8…
Kitu gani kilinisaidia kuweza kuandika hivyo vitabu, na kuandika vitabu zaidi baada ya maisha ya chuo..
Kitu kimoja kikubwa ni kwamba nilikuwa na lengo ambalo nilikuwa nalifanyia kazi.
Usipokuwa na lengo au malengo ambayo unayafanyia kazi maishani mwako, ujue kabisa kwamba unaenda kukwama. Kikwazo kidogo tu, kitakukwamisha wewe na kukurudisha nyuma.
Malengo yatakuonesha wapi uwekeze nguvu zako na vitu gani unapaswa kuachana navyo ili uweze kufika mbali.. ni uhakika kuwa mpaka sasa hivi utakuwa umeshaweka malengo ya kufanyia kazi maishani mwako.
Kama mpaka leo hii hauna malengo, maana yake unaishi tu. Yaani, kunakucha na kuchwa huku wewe ukiwa unazunguka bila mwelekeo.
Acha kila kitu unahofanya sasa hivi uweke malengo.
Lakini pia hakikisha kwamba umesoma kitabu cha Kutoka Sifuri Mpaka Kileleni. Hiki kitabu kina mwongozo mzuri wa kukusaidia wewe kufikia malengo yako. Sura ya pili nzima ya kitabu hiki imeingia kiudani kueleza malengo na jinsi ambavyo yanafanya kazi. Kisome kitabu hiki, kitakusaidia sana.
Kinapatikana kwa 20,000/- nakala ngumu. softcopt utaipata kwa 10,000.
Wasiliana nami sasa kwa 0755848391 ili nikutumie kitabu.
Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli
Godius Rweyongeza kutoka SongaMbele
Tuwasiliane kwa 0755848391
Ji