Nakumbuka mwaka 2019 kulikuwa na kijitabu kidogo hivi kilikuwa kinazunguka mtandaoni. Kijitabu hiki kilikuwa kinajulikana kama Baharia.
Kilikuwa kinazungumzia mambo kadha wa kadha ambayo baharia anafanya.
Kijitabu hiki kilizunguka sana, sana. Binafsi sikukisoma, Ila watu wengi ninaowafahamu mimi walikisoma hicho kijitabu. Kwa hiyo mada yao kubwa kwenye mazungumzo ikawa imekuwa BAHARIA.
Yaani, ulikuwa huwezi kupitisha nusu saa bila kusikia mtu akisema kuhusu Baharia.
Kwa sababu nilikuwa nimezungukwa na watu wengi waliosoma kijitabu kwa wakati huo, nikipata kujua kuhusu uwepo wa kijitabu hicho. Na hata baadhi ya vitu kwenye kijitabu hicho nilisikia watu wakiviongelea…
Wewe vipi ulikisoma?
Kama nakuona vilee….
Sasa katika kipindi hiki nilikaa nikajiuliza. Kama hiki kijitabu (ambacho mimi niliona hakina ujumbe wa maana) kinaweza kusomwa hivi, basi na Mimi naweza kukaa chini, nikaandika kitu cha maana kikasomwa na kusambaa sana kama hiki kijitabu….
Nilitafakari sana hili…
Ila sikujua niandike nini… Nilikuwa najiuliza hivi hiki kijitabu kina sifa gani ambazo zimekifanya kisomwe Sana.
Baada ya siku chache nikaamua kuandika kitabu kuhusu usomaji wa vitabu.
Kitabu hiki nilishaanza kukiandika muda kabla hata kusikia habari za BAHARIA. Ila nilikuwa nakiandika kwa mfumo wa hadithi. Na baadaye ile hadithi ilipotea nikiwa katikati baada ya kupoteza simu yangu..
Baada ya tafakari ya kina, nikaamua kurudia kuandika kitabu hiki, Ila zamu hii sikutaka kuandika hadithi kama ilivyokuwa mwanzoni.
Nikaanza kuandika. Sikumbuki nilitumia muda kiasi gani kuandika hiki kitabu, Ila nadhani nilikiandika siku za wikendi kikakamilika.
Nikakitengeneza vizuri, halafu nikamfuata mshikaji wangu Magambo kumpasha habari. Nikampa nakala aisome,
Wakati nasubiri mrejesho wake nikaamua kuwa kitabu kile nikitoe na nikigawe bure, Kama ambavyo nilikuwa nimepanga tangu mwanzo
Kilichotokea ni historia.
Kitabu hiki ambacho mwanzoni kilikuwa kinajulikana kama MAAJABU YA VITABU, na Sasa hivi kinaitwa MAAJABU YA KUSOMA VITABU kimesomwa na watu wengi tangu hiyo Septemba 2019.
Kimezungumzia kuhusu usomaji wa vitabu tu! Na kimekuwa kikitolewa bure tangu 2019 mpaka leo hii.
Kiukweli wengi wamekisoma, na sasa nina toleo la 2 kitabu hiki. Pamoja na marekebisho yake.
Wewe pia unaweza kupata zawadi ya nakala yako HAPA CHINI
Mpaka sasa kitabu hiki, kimekuwa kuwa mwongozo wa usomaji wa vitabu kwa watu wengi. Lakini kwa watu ambao hawajawahi kusoma kitabu changu chochote, huwa nawashauri waanze na hiki cha bure, halafu ndio waje kununua.
Wewe pia Anza na hiki Cha bure
Halafu baada ya hapo, njoo upate ebooks mbili kwa ofa ya pasaka. Ebooks hizi ni
MAISHA NI FURSA: ZITUMIE ZIKUBEBE pamoja na
Vyote hivi viwili utavipata kwa bei ya 8,000/- tu badala ya bei yake halisi. Tuma fedha kwa 0684408755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA
Orodha ya vitabu vyangu yote hii hapa
Ni mimi rafiki yako
Godius Rweyongeza
0755848391
Morogoro-Tz