Hii Ndiyo Kazi Rahisi Kuliko Zote Duniani


Nakumbuka siku moja kwenye redio kulikuwa mjadala mzito. Mada mezani lilikuwa ni swali lililouliza ni kazi ipi ni rahisi hapa duniani.

Kila mtu alijitahidi kuchangia mada kiundani kadiri alivyoweza. Nakumbuka vizuri jamaa mmoja alichangia mada kwa kusema kuwa hapa duniani hakuna kazi rahisi. Kila kazi ni ngumu.

Aliendelea kusema kuwa ukiwa mwanasheria utaona kuwa Sheria ni ngumu.
Ukiwa daktari, utasema utabibu ni mgumu.
Ukiwa unabeba mizigo, utasema kazi yako ni ngumu na
Mkulima naye atasema kazi yake ni noma!
Huku dereva wa masafa maredu Naye atasema, we acha. Muda mwingine hulali eti unaendesha gari.

Kwa kipindi hicho nilikubaliana na hilo jibu na kila mara ulipokuwa ukitokea mjadala wa aina hiyo, nilikuwa nikichangia kwa kusema kuwa hakuna kazi rahisi hapa duniani. Badala yake kazi ambayo kila mtu anafanya kwake ni ngumu.

Mara zote nilipokuwa nikisema hivi, nilikuwa naonekana kama nilikuwa natoa booonge na   pointi…. Laiti kama ningekuwa nachangia mada kwenye midahalo kama ile ya education is better than money, basi ningekuwa napigiwa makofi ya kishindo….

Unaikumbuka ile midahalo ya education is better than money?????

Mimi naikumbuka sana, maana enzi hizo kama ningekosa kuchangia pointi kwenye mdahalo siku hiyo ningeumwa. Moja ya mdahalo mzito ambao nakumbuka ulizua utata, ulikuwa ni mdahalo wa the love of money is the root of all evils.

Watu tulishusha kimombo hatari siku hiyo…..
Nadhani malkia angekuwepo siku hiyo angenipeleka kwenye kasri yake nikae humo tu 😂😂

Hivi nilisema nakwambia kazi rahisi kuliko zote hapa duniani eeh!

Nshajisahau nikajua sijui nipo nafundisha shule ya msingi. Maana kuna kipindi pia nilikuwa na ndoto za kuwa mwalimu😂😂..

Aaah,
Acha bwana tuendelee.

Ukipata na kazi ya aina hii, hii ndio rahisi.

Unajua kwa Nini?

Kwa sababu ni kazi ambayo hutahangaika kuifanya. Ni kazi ambayo hata ukiifanya kwa muda mrefu, hutaona kama umeifanya kwa muda mrefu. Kwa sababu tu unaipenda. Kwa sababu una Ilove.

Thomas Edison alikuwa alala saa tatu kila siku na kuwahi kazini. Siku moja aliulizwa kwa nini unafanya kazi kwa muda mrefu hivyo, akisema sijawahi kufanya kazi.

Si inashangaza eeh! Yaani, mtu anafanya kazi saa 18 mfululizo, halafu anasema eti hajawahi kufanya kazi….

Alikuwa anasema hivyo kwa sababu tu alikuwa anafanya kitu alichokuwa anapenda.

Ukiwa na unafanya kazi unayoipenda, hata huhangaiki kuangalia muda…
Yaani, wewe unapiga kazi tu, halafu baadaye unastuka kuona muda umeenda sana.
Unafanya kazi saa nane ila unaona kama vile ndio umeanza.
Husukumwi na mtu kuifanya, wewe mwenyewe unajisukuma kwa sababu unaipenda.

Hapa ndio namkumbuka Albert Einstein. Huyu jamaa naye wakati mwingine alikuwa na vituko…
Kuna siku alisema; ukikaa na binti mkali (mrembo) kwa saa mbili utaona kama umekaa naye kwa dakika moja, Ila ukikaa na kwenye makaa ya moto kwa dakika moja, itaonekana kama saa 2.

Hii pia inafanya kazi kwenye maisha ya kazi.
Ukifanya kazi ambayo huupendi. Kila sekunde kwako itakuwa ya moto. Utaona muda hauendi. Na utatamani uzurure huku na kule ili muda uende…

Acha kujiumiza. Kuanzia leo anza kufanya kazi unayopenda. Kama kazi uliyonayo Sasa hivi huipendi, basi ipende. Kama huwezi kuipenda achana nayo ukafanye kazi unayopenda.


2 responses to “Hii Ndiyo Kazi Rahisi Kuliko Zote Duniani”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X