Hiki kitu ndicho kitakusaidia wewe kukaa kwenye gemu la mafanikio kwa muda mrefu mpaka ukashinda


Kila mtu anapenda  kufanikiwa. Yaani, hapa ufahamu kabisa kuwa ni kila mtu  anapenda. Hakuna mtu anapenda kushindwa. Ukiingia kwenye chumba chochote ambacho kina watu, ukiuliza wangapi wanapenda kufanikiwa. Wote watanyosha mikono juu na tena wengine watanyosha mikono miwili juu.

Sasa swali letu ni kwa nini watu wengi huishia kufeli wakati wanapenda kufanikiwa.

Najua hapa unaweza kutoa sababu nyingi kama watu kutokuwa na malengo makubwa, kutojisukuma zaidi na mengineyo kama hayo; ila kitu kimoja kikubwa ambacho kinafelisha wengi ni watu waliowazunguka.

Ebu fikiria mtu wa kawaida amezungukwa na wangapi waliofanikiwa au wenye kiu kubwa ya mafanikio? Wangapi?
Ukifuatilia utakuta ni sifuri.
Mtu anatoka kwenye familia masikini
Anasoma na watu masikini
Anaoa au kuolewa na mtu masikini
Ila yeye ana ndoto ya kufika mbali.

Watu waliomzunguka wengine wote ni masikini na hakuna mwenye mtazamo wa kusema kwamba anataka kufika mbali kiuchumi. Na hawa ndio wanampa ushauri huyu mtu. Unadhanai atatoboa? Thubutu.

Yaani, ushauri upewe na masikini unadhani atakupa ushauri gani?

Siyo kwamba nadharau au kumshusha mtu, Ila ninachotaka ufahamu ni kwamba, chuma kinanoa chuma.

chuma kinanoa chuma

Ukizingukwa na chuma uwezekano wa wewe kunolewa kuwa chuma ni mkubwa. Ndio maana ni muhimu kwako kuzungukwa na timu ya watu sahihi.

Timu ya watu waliokuzunguka wana uwezo wa kukusaidia wewe kufanya makubwa au kushindwa kufanya makubwa.

Unataka kujiajiri? HAKIKISHA una timu sahihi iliyokuzunguka ya kukusaidia kufanya hivyo.

Unataka kufikia umilionea au ubilionea, hakikisha una timu sahihi ya kukusaidia kufanya hivyo.

Na timu sahihi ni watu ambao wamewahi kufanya hivyo au wanafanya hivyo kwa vitendo sasa hivi.

Kitu ambacho ni kigumu sana kukipata kwenye jamii. Wengi kwenye jamii Wana mipango mizuri ya mdomoni tu ya kufika mbali, Ila hawana mipango madhubuti ya vitendo.

Hiki kitu kinachokosekana kwenye jamii, ndicho tulichonacho kwenye THINK BIG FOR AFRIKA

Think big for Afrika ni jamii ya tofauti kabisa ambayo huwezi kuikuta sehemu nyingine. Iko hivi, hii ni jamii ya watu wenye ndoto kubwa za kufika mbali na sote kwa pamoja tunashikiriana kuhakikisha tunafika mbali.

Kila mmoja ni sehemu ya timu na kila mtu anamshika mkono mwenzake kuhakikisha kwamba  haachwi mtu nyuma.

Kila mtu ana ndoto kubwa ya kufanyia kazi na amezungukwa na wengine wanaozifanyia kazi. Ni sehemu maalumu yenye vyuma vinavyonoa vyuma.

Karibu ujiunge na jamii hii ya kipekee sana.
Ili kujiunga unapaswa kuwa na shauku ya kufanikiwa na kufika mbali na uwe tayari kufanya kazi kwa vitendo ili ufikie mbali.

Utaungana na watu sahihi walio kwenye gemu
Utapata mafunzo sahihi kila siku.
Utashirikiana na wenzako na mengineyo mengi.

Karibu sana ndani ya jumuiya hii ya kipekee. Eneo la kwanza kabisa la kujiunga jamii hii ni kupitia mafunzo yanayotolewa kwenye kundi la WhatsApp na baruapepe.

Mafunzo haya ya kipekee ambayo huwezi kuyapata kwingine yanatolewa kila siku kwenye maeneo hayo mawili.

Gharama za kujiunga na mafunzo haya ni 10,000 kwa mwezi.

Ila ukilipia kuanzia miezi mitatu kuna punguzo la asilimia 10. Hivyo, utalipia elfu 27000 badala ya elfu 30.

Ukilipia kwa miezi sita kutakuwa na punguzo la asilimia 20. Hivyo, utalipia elfu 48,000 badala ya elfu 60.

Na ukilipia kwa mwaka mzima kutakuwa na punguzo la asilimia 30. Hivyo utalipia 84,000 badala ya 120,000

Mafunzo haya maalumu yanatumwa kwa njia ya barua pepe na WhatsApp kwenye kundi la THINK BIG FOR AFRIKA

kila siku utapokea makala moja yenye mafunzo ya kina

kila jumapili utapokea ebook moja yenye uchambuzi wa kitabu, au andiko liliojadili mada fulani kwa kina kuhusu biashara, malengo au vipaji

inaweza kutokea kwamba jumapili ukatumiwa audio au video itakayokuwa inahusu jambo fulani hasa kuhusu biashara badala ya ebook.

Sambamba na hilo utakuwa na nafasi ya kunipigia na kuongea nami kwa ajili ya ushauri zaidi muda wowote utakapohitaji

Jiunge leo hii kwa kulipia ada ya mwezi mmoja, mitatu, sita au mwaka mzima.

Lipia kwa namba 0755848391 jina ni GODIUS RWEYONGEZA.
Baada ya kulipa niambie nikuunge.

Karibu sana Think Big For Afrika.

Umekuwa nami

Godius Rweyongeza


3 responses to “Hiki kitu ndicho kitakusaidia wewe kukaa kwenye gemu la mafanikio kwa muda mrefu mpaka ukashinda”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X