Kwa nini wazazi wanawalazimisha watoto kusoma kozi wanazopenda wao


Kila mwaka kikifika kipindi cha wahitimu wa kidato cha sita kuomba vyuo, huwa napokea simu za vijana ambao wanalazimishwa na wazazi kwenda kusomea kozi wasizopenda.

Unakuta kijana anataka akasomee uhandisi, mzazi anataka akasomee human resources.

Sasa leo kwa ufupi tu nataka niseme kwa nini, wazazi wanakuwa hivyo:

Moja ni kwa sababu ilikuwa ndoto ya mzazi, ikamshinda sasa anaisukuma kwa mwanae.
Unakuta mzazi wako alikuwa na ndoto ya kuwa daktari ila udaktari ukamshinda, akaapa kuwa nitahakikisha mwanangu anakuwa daktari. Sasa bila kujali wewe unaupenda au huupendi, utakuta anakulazimisha ukausome.

Kitu hiki siyo sahihi. Kama wewe ni mzazi unapaswa kufahamu kuwa jukumu lako siyo kumchagulia mwanao kozi ya kusoma Bali kumwongoza na kumwacha achague mwenyewe.

Wazazi wengi huwa wanatumia nguvu waliyonayo kama wazazi kuwalazimiaha watoto kuchagua kozi wanazotaka waaome. Na muda mwingine kuwatishia watoto kuwa endapo wataenda kinyume watawaadhibu kwa kuwanyima ada.

Mzazi kama mzazi unapaswa kuwa shabiki kwa kile anachofanya mwanao na anachopenda kufanya.

Kama wewe ulikuwa na ndoto za kusomea kitu fulani Ila ilashindikana, basi. Hiyo imepita, mwache na mwanao apambane na hali yake.

Pili ni kwa sababu, ya walivyowaona ndugu wengine.
Unakuta mzazi kamwona ndugu au rafiki yake amesomea kitu fulani na anatamani hicho kitu, basi analazimisha na mwanae asomee hicho kitu.

Unachopaswa kufahamu mzazi ni kuwa ukiona ndugu au rafiki amesomea kazi fulani na anaifanya inamlipa, jua kasomea kitu anachopenda. Na wewe mwache mwanao akasomee anachopenda.

Kitu kingine Ni kwamba, ajira inayolipa leo, haitakuwa inalipa kesho. Hivyo, Leo unaweza kumwambia mwanao kasomee kozi fulani inalipa Sana. Ila kesho kozi hiyohiyo ikawa haina dili kwenye soko la ajira….

Ndio maana nawashauri vijana wengi waaomee kile wanachopenda wenyewe.One response to “Kwa nini wazazi wanawalazimisha watoto kusoma kozi wanazopenda wao”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X