Nyakati Ngumu Hazina Ukomo


Leo nimekumbuka mwaka 2018 na 2019 jinsi watu walivyokuwa wanalalamika kwamba vyuma vimekaza. Kuna watu wengi walikuwa wanasema kwamba hawawezi kufanyia kazi malengo yao kwa sababu tu vyuma vimekaza.

Nakumbuka kila nilipokuwa nikiongea na watu, kitu muhimu nilichokuwa nikiwasisitiza kilikuwa ni kwamba, USISUBIRI VYUMA VILEGEE. Badala yake katika kukaza hukohuko, wewe mwenyewe pambana kuhakikisha kwamba kila kitu kinanyooka.

Baadaye mwaka 2020 kuliltokea ugonjwa wa UVIKO-19. Basi sasa kipindi hiki kisingizio kilikuwa ni UVIKO.

Ulipokuwa unaongea na mtu, kwa nini huweki akiba, sababu ilikuwa ni UVIKO-19

Mwingine ungemwuliza kuhusu ndoto yake, basi alikuwa anasema kwamba UVIKO-imenizuia kuifanyia kazi.

Kiufupi, kila kitu kilikuwa kinaelekezwa kwenye UVIKO-19.

Na sasa siku za karibuni umetokea mfumuko wa bei..

Kila kitu sasa kinaelekezwa kwenye bei za vitu kupanda.

Nataka nikwambie kitu……….hakuna wakati ambao mambo yatakaa yawe safi kabisa bila shida yoyote. Yaani, yanyooke kwa asilimia 100. Nyakati ngumu huwa haziishi. Unachohitaji ni wewe kuwa mgumu.

Muda mwingine unaamua tu kufanya kitu hata kama mambo mengine yanaonekana yanakwenda kinyume chako, maana ukisubiri kila kitu kikae sawa. UTASUBIRI SANA.

Unakumbuka miaka ya 2010 kusajili lailni ya simu kulikuwaje? Ulikuwa unaenda kwa wakala,anajaza fomu fulani hivi baadaye unapewa lalini yako na kuondoka.

Wakati mwingine ulikuwa unakuta laini imesajiriwa, unapewa laini yako unaondoka.

Vigezo havikuwa kama sasa hivi, si ndio?

Hii mitandao ya simu haikusubiri  mpaka ijue kila kitu ndio ianze. Walianza, halafu haya mambo mengine ya kiteknlojia wameyachukua humu njiani.

Nataka hiki kitu kikupe funzo na wewe pia.

Usisubiri mpaka kila kitu kikae sawa eti uanze. Anza, halafu mambo mengine, utakuwa unaboresha kadiri unavyoenda.

Sikiliza, nyakati ngumu huwa haziishi kwenye maisha. Nyakati ngumu zipo na zitaendelea kuwepo. Kitu kikubwa ni wewe kuamua kuwa mgumu pia kwenye kazi zako.

Haya maisha usipojitoa kufanyia kazi ndoto yako. Kila wakati kutakuwa na sababu ya kukuzuia usiifanyie kazi.

Kama siyo vyuma kukaza basi ni UVIKO-19, kama siyo UVIKO basi mfumuko wa bei.

Kuwa mgumu, pambania ndoto zako.

hiki kitu kinanifanya nikumbuke kitabu cha NYUMA YA USHINDI: Kuna kushindwa, Kushindwa, Kushindwa. Ni kitabu ambacho unapaswa kusoma pia maana ndani yake utajifunza mengi. Kupata kitabu hiki, wasiliana nami kwa 0755848391. kwa sasa hivi kuna ebooks au softcopy tu. na inapatikana kwa 5,000/- tu.

jiunge na mfumo wetu wa kupokea makala maalumu kwa watu maalumu hapa chini


One response to “Nyakati Ngumu Hazina Ukomo”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X