Huyu Ndiye Mtu Anayelipwa Kuliko Wote Hapa Duniani


Rafiki yangu siku ya leo nataka nikueleze mtu ambaye analipwa kuliko wote hapa duniani.

Hivi labda unafikiri mtu wa aina hii atakuwa yupi? Je, ni mtu ambaye amesoma sana?  Je, ni mtu ambaye amefanya kazi kwa siku nyingi kwenye kazi?

Wengine wanafiriki kwamba mtu ambaye amefanya kazi kwa muda mrefu kwenye biashara au kampuni au taasisi ndiye alilipwa kiasi kikubwa cha fedha ukilinganiha na yule ambaye alikuwa amefanya kazi kwenye taasisi husika kwa muda mfupi (newcomer).

Zamani ilikuwa ni mtu mwenye cheo kikubwa ndiye alikuwa analipwa kiasi kikubwa kuliko mtu mwingine.

Au la, alikuwa ni mtu ambaye alikuwa amesoma na ana viwango vya juu vya elimu.

Siku hizi zama zimebadilika. Unaweza kuwa na elimu kubwa, umefanya kazi kwenye taasisi husika kwa muda mrefu na hata cheo kikubwa lakini bado usilipwe kiasi kikubwa. Kwa nini? Kwa sababu siku hizi wanaolipwa sana ni

Wenye uwezo wan a ujuzi wa tofauti.

Wale wanaofanya kazi kwa bidii na kuonesha matokeo. Kumbuka kufanya kazi kwa bidii na kuleta matokeo hakuna uhusiano wowote ule na kiwango cha elimu ulichonacho sasa hivi, na wala hauhusiani kwa vyovyote vile na muda ambao umekuwa ukifanya kazi kwenye taasisi husika.

Hivyo ndivyo vitu vya msingi ambavyo vinahitajika kwako ili uweze kulipwa vizuri ukilinganisha na mtu mwingine.

Kama hauna ujuzi wowote wa kukutofautisha, anza kuujenga. Fanya mazoezi kwenye kile unachofanya kiasi kwamba uweze kukifanya kwa viwango vikubwa ukilinganisha na mtu mwingine ambaye yuko karibu yako. Ronaldo ni moja ya watu ambao wanalipwa sana, siyo kwa sababu tu anacheza mpira. Ila kwa sababu ya uwezo wake wa kipekee. Na uwezo wa Ronaldo siyo kwamba ni wa kuzaliwa nao. Ila ni uwezo ambao ameujenga.

Wewe mwenyewe unaweza kujijengea uwezo kwenye kazi au biashara ambayo unafanya. na njia bora ya kujijengea uwezo mkubwa ni kufanya mazoezi ya kutosha.

SOMA ZAIDI: Wanawake Watano Walioshindwa Karibia Kwenye Kila Kitu Na Bado Wakashinda Kwa Kishindo


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X