Kitabu: UNFAIR ADVANTAGE
Mwandishi: Robert Kiyosaki
Mchambuzi: Hillary Mrosso
Mawasiliano: 255 683 862 481
UTANGULIZI
Kama jina la kitabu hiki lilivyo, Unfair Adavantage, mwandishi anaeleza kwa undani namna alivyotoka kwenye ajira, namna alivyo anzisha biashara, namna alivyojifunza kwa undani masula ya kodi, hati fungani, mifuko ya pensheni, mifuko ya hifadhi ya jamii, mabenki na mifumo mingine ya kifedha, kuanzia marekani hadi sehemu nyingine duniani, pia ameeleza mifumo ya elimu jinsi ilivyofeli kutoa elimu ya kifedha wa wanafunzi. Maarifa yaliyopo kwenye kitabu hiki yatakufanya upate faida kwenye kila eneo ambalo unataka kuwekeza fedha zako, na hii ndio dhana kuu ya Unfair Adavantege.
Karibu tujifunze mambo 70, niliyoyaona ndani ya kitabu hiki;
- Watu wengi wanatumia maisha yao kuwa watumwa wa mishahara ya waajiri wao na kuwa watumwa wa kodi kwa serikali.
- Watu wengi bado hawajui kati ya chakula na chakula ambacho ni mtego ndio maana ni rahisi sana kukatatika.
- Wengi wanaingia kwenye ajira na hapo ndio inakuwa mtego kwao, kutoka inakuwa ngumu sana, kwasababu ya dhana ya usalama iliyopo.
- Kama unataka kuwa muwekezaji basi, jua kuwa hutakiwi kuwa mtu wa kawaida (average), unatakiwa kuwa mwekezaji mwerevu na mwenye busara zaidi.
- Wawekezaji wa kawaida ndio huwafanya wawekezaji werevu au wenye busara kuwa matajiri.
- Mwandishi anasisitiza sana kuwa uwekezaji ulio bora sio kwenye majumba, hisa, hati fungani, mifuko ya pensheni, dhamana, au kwenye mali zisizo hamishika, uwekezaji bora ni kuwekeza kwako mwenyewe.
- Kam usipokuwa mwerevu na mwenye busara katika kuwekeza, kila utakachowekeza kitapotea na utapata hasara, Kama wewe ni mjinga, hata uwekeze kwenye vitu gani, kwa kiasi kikubwa utaishia kushindwa vibaya.
- Siku zote, kama hujui cha kufanya na fedha zako, kitu bora cha kufanya ni kutomwambia mtu yeyote.
- Upeo ulionao kuhusu elimu ya fedha ndio huamua nini ufanye na fedha zako na ni sehemu gani sahihi zaidi ya kuwekeza fedha zako.
- Kama huna elimu ya fedha hatari zinakuwa nyingi, kodi zitakuandama, na faida zitaendelea kupungua. Elimu ya fedha ni muhimu sana katika uwekezaji na biashara.
- Watu wasio na elimu ya fedha huishia kuwekeza katika vitu visivyo na faida na vyenye hasara. Mfano kununua sana Liabilities.
- Haina maana kabisa kufanya kazi kwa nguvu zako zote kisha serikali ikachukua fedha zako, bila wewe kunufaika nazo.
- Fedha nyingi za waajiriwa zinakwenda serikalini kwa majina tofauti tofauti kama vile kodi, pensheni, nk
- Kama usipokua mwerevu serikali itazichukua fedha zako ulizozipata kwa damu na jasho baada ya wewe kufariki. Kuwa na mpango madhubuti wa kuondokana na hali hiyo, kwa kuwa mwekezaji mjanja.
- Usipokuwa mwerevu na mjanja magonjwa na madalali watanufaika zaidi na fedha zako kuliko wewe.
- Usipokuwa mjanja hata wanasheria nao watakuwa karibu ili kunufaika na fedha zako zaidi ya wewe mwenyewe ambaye umezitafuta kwa kufanya kazi ngumu usiku na chana
- Kabla ya kutafuta na kutengeneza fedha, jifunze namna ya kuzilinda fedha zako maana wanaozihitaji ni wengi sana.
- Hali ya kukosa Imani na usalama wa fedha zako ndio husababisha wengi kufikiria kuwa uwekezaji na kuingia kwenye biashara ni gumu na kuna hatari nyingi.
- Kumbuka siku zote kuwa chochote ambacho ni hatari ni kwasababu hakijadhibitiwa, kama ukiwa na udhibiti au usimamizi mzuri wa fedha na mali zako, hatari zinapungua au zinaweza zisiwepo kabisa.
- Elimu ya fedha inayofundishwa mashuleni na vyuoni inawafundisha watu kuwekeza fedha zao serikalini, banki, benk za uwekezaji, mifuko ya hifadhi ya jamii nk.
- Elimu ya kweli na nzuri kuhusu fedha ni ile inayokufundisha namna ya kuwafanya watu wakuletee wewe fedha zao, na sio wewe uchukue fedha zako upeleke serikalini, au uwape watu wengine wanufaike nazo.
- Mwekezaji mjanja na mwenye maarifa ni yule anayetumia fedha za watu wengine kupata utajiri, kama vile kukopa benk, serikalini na kwa watu wengine.
- Usiwape fedha zako matajiri, au kuhifadhi fedha zako benki, feha inashuka na kupanda thamani kila wakati, ukiweka fedha benki kama uwekezaji jua kuwa huo sio uwekezaji wa busara.
- Jinsi unavyoifanyia kazi fedha, ndivyo unavyokatwa kodi kubwa kwenye mapato yako.
- Jinsi fedha inavyokufanyia wewe kazi kwa nguvu, ndivyo unavyolipa kodi kidogo,
- Ndio maana waajiriwa wengi wanaandamwa na makato makubwa ya kodi, na jinsi wanavyojitahidi kuongeza kufanya kazi kwa bidi ndivyo na makato yanakuwa makubwa.
- Ukitumia fedha za watu wengine ndio zikufanyie kazi kwa bidi, uwezekano ni mkubwa sana wa kulipa kiasi kidogo cha kodi, na wakati mwingine unaweza usilipe kodi kabisa.
- Kama unataka kupata fedha zaidi na ulipe kodi kidogo, unahitaji kubadili aina ya mapato yako, yani sehemu mapato yako au fedha zako zinakotoka.
- Njia nzuri ya kubadili chanzo cha mapato yako ni kuwa na biashara au uwekezaji ambao unakuingizia fedha na kuacha kutegemea ajira pekee maana mapato yanayotoka kwenye ajira ndio hukatwa kodi kubwa.
- Katika ulimwengu wa kifedha na uzalishaji wanapenda sana wakopaji kuliko watunzaji wa fedha.
- Kama unakopa fedha benki kwa lengo la kuzalisha, mabenki yanapenda sana watu wa aina hiyo, maana ndio wanaoleta faida na kufanya benki ziwe na fedha zaidi.
- Wengi tunafahamu ilivyo rahisi kuingia kwenye madeni, ishu sio kuingia kwenye madeni, ishu ni unayabebaje hayo madeni, unayasimamia vipi hayo madeni, hapo ndipo ugumu ulipo.
- Kama wewe ni mjinga hakuna uwekezaji utakao kufaa, hata kama utawekeza kwenye dhahabu na silva, bado unaweza kupata hasara.
- Sehemu zote duniani, serikali huwa zinawalinda wazalishaji kuliko walaji wa mwisho ambao wanaifanyia kazi fedha, hasa waajiriwa wanaotegemea ajira.
- Wanaoifanyia kazi fedha mara nyingi ndio huwa wahanga wa kupata hasara na huishia kuwa masikini.
- Cha kushangaza zaidi huku duniani ni kwamba wengi wenye elimu nzuri ya darasani wanaheshimu sana maswala yao ya kitaaluma lakini wanashuindwa kuheshimu elimu ya kifedha ambayo ni muhimu sana kwenye maisha.
- Wengi wanataka fedha na wanataka kuwa matajiri, lakini wanataka utajiri na fedha bila kulipa ghrama au kujitoa sadaka kufikia malengo hayo.
- Njia nzuri ya kuisaidia na kuiokoa dunia ni kujiokoa na kujisaidia wewe mwenyewe kwanza. Kama huwezi kujisaidia na kujiokoa wewe mwenyewe, na utawezaji kuisaidia dunia?
- Mwandishi wa kitabu hiki ameandika haya ili kututia moyo tuwe wanafunzi wa elimu ya fedha, ili tujue namna ya kushughulika vizuri na maswala yetu ya kifedha na kuwa wakarimu kwa vipawa tulivyopewa na Mungu.
- Ni kama vile alivyowahi kusema Dr. Fuller kuwa ni kwa kuwa wakarimu ndio tunaweza kujua vipawa tulivyopewa na Mungu na uwezo wetu wa kipekee.
- Hii ina maana unapofanikiwa kifedha, uwe mkarimu zaidi kwa kuwasaidia wengine kufikisha malengo yao kifedha, usiwe mchoyo.
- Hali mbaya ya kifedha tunayopitia imesababishwa na matumizi mabaya ya fedha na rushwa katika ngazi za juu serikalini.
- Rushwa imeangusha mambo mengi mazuri na yenye tija kwa jamii. Imeaharibu misingi ya haki na usawa.
- Ni kweli kabisa kuna wengi wana tamaa ya madaraka kiasi cha kuuza hata nafsi zao, kuumiza maisha ya wengine, kumwaga damu ili kutimiza adhima yao ya kutaka madaraka.
- Dunia inashughudia kuwa na watu wa aina hiyo ambayo kwa kiasi kikubwa wamesababisha kukua kwa umasikini na kuwa matumizi mabaya tya fedha kama vile kutawala kwa rushwa.
- Siku zote kumbuka, ajira yako sio asset, huwezi kumrithisha watoto wako ajira uliyonayo.
- Fedha sio asset, siku hizi fedha inazidi kupungua thamani yake kwa jinsi deni la taifa linapovyongezeka.
- Proleteriat, ni watu wasiomiliki vitu vya uzalishaji, kama mashamba, walichonacho watu hawa ni mshahara wa ujira kutokana na kazi ngumu wanazozifanya.
- Mfumo wetu wa elimu na mitaala yake inawandaa wanafunzi kuwa waajiriwa, watu watakaotegemea mishahara na ujira wa mwezi baada ya kuwafanyia wengine kazi.
- Badala ya wanafunzi kuondoka shuleni na kuanza kutafuta ajira zenye mishahara mikubwa, inatakiwa wakitoka shuleni wafikirie namna ya kutengeneza ajira na kazi zenye mishahara mikubwa.
- Mfumo wetu wa elimu unatakiwa kuwa andaa wanafunzi waje kutengeneza ajira kwa ajili ya kuajiri wengine na sio kutegemea kuajiriwa pekee.
- Wengi wanaotoka vyuoni wanataka walipwe zaidi kwa kufanya kazi kidogo, jambo hili ni gumu, maana kwa jinsi kulivyo na uhaba wa ajira hakuna mwajiri atakayevumilia hilo.
- Badala ya kutoka vyuoni na kuanza kutafua ajira zenye mikataba mizuri na zenye usalama, inatakiwa wanafunzi wakitoka vyuoni, watengeneze ajira au kazi zenye mapato endelevu.
- Wengi wanakimbilia ajira maana zinaweza kuwa na mishahara, mikataba, na marupurupu mengine, lakini ukweli ni kwamba wanatafuta usalama, na sio fedha kiivyo,
- Kwa kiasi fulani mfumo wetu wa elimu unawaaminisha wanafunzi kuwa matajiri ni watu wenye tamaa na watu wabaya, wanafunzi wanatakiwa wajue kuwa tajiri ni jambo zuri na wanatakiwa kuwa wakarimu.
- Duniani kwa sasa kuna shule za sharia, shule za udaktari, mwandishi anahoji, kwanini kusiwe na shule kwa ajili ya kufundisha ujasiriamali na ubepari?
- Mwandishi anatamani kila mtu apate elimu ya fedha na uwekezaji, hii itaokoa muda na kukuondolea hatari za kupoteza fedha katika uwekezaji au biashara.
- Mwandishi hapendezewi sana na kuwapa fedha zetu watu wa mipango fedha au watalamu wa masuala ya kifedha, anaamini wengi wa watu hao sio wazuri na wanaweza wasikushauri vizuri kuhusu namna ya kuzalisha fedha zaidi.
- Kuna watu wanafikiri kuwekeza fedha benki ni ujanja, nasema, sio ujanja maana hata wasio na akili wanaweza kufanya hivyo. Pata elimu ya kifedha uwekeze kwenye faida.
- Kichwa chako au ubongo wako ndio asseti yako kubwa, lakini pia inaweza kuwa ni liability yako kubwa. Haya yote yameandikwa ili tupate unfair advantage ya kutumia na kugeuza akili zetu kuwa asseti yetu kubwa.
- Hutajua ladha ya uhuru wa kweli kama hujafanikiwa kuwa huru kiefdha, au kuwa na uhuru wa kifedha.
- Hivyo basi wekeza katika kupata uhuru wa kweli ambao ni kupata uhuru wa kiefha. Kupata elimu ya fedha ni muhimu kuliko kujifunza utalaamu au profession.
- Linapokuja suala la fedha kila mtu atatamani kukwambia lake, hivyo kamwe usiende kuuliza kwa mtu anayeuza bima kama unahitaji bima.
- Wawekezaji werevu na wajanja wanazingatia sana suala la kodi kabla ya kuingia kwenye uwekezaji.
- Wawekezaji halisi hawahifadhi fedha zao, huwa wanaziachia ziingie kwenye mzunguko ili kuzalisha zaidi kuna neno wanapenda kulitumia “velocity of money.”
- Kikubwa cha kujua siku zote, haijalishi unawekeza kwenye kitu gani, unatakiwa ujifunze kitu hicho jifunze na elewa mambo yote muhimu kuhusu uwekezaji wako.
- Ukiwa mwekezaji mzuri unaweza kuzalisha fedha katika hali zote bila kuangalia soko lipoje, hata kama uchumi ni mbaya bado unaweza kutengeneza fedha.
- Ukishajua unataka kufanya nini kwenye maisha yako, tafuta kocha, mtu ambaye atakusimamia hadi umalize jambo lako.
- Katika maswala ya kifedha, kuna hisia sana na kama huwezi kudhibiti hisia zako, basi jua hutaweza kudhibiti fedha zako
- Unaweza kusema kuwa huna fedha mara nyingi uwezavyo, lakini itakuwa haina tija kwenye maisha yako. Shauku ina nguvu kuliko elimu, tumia shauku uliyonayo kuingia kwenye utajiri kwa kuzingatia elimu ya fedha uliyoipata. Hata haya yote tuliyojifunza hapa, kama huna shauku ya kuyafanyia kazi hayatakuwa na maana sana kwenye maisha yako.
Ahsante sana!
2 responses to “Uchambuzi Wa Kitabu Cha UNFAIR ADVANTAGE”
Dah! nashukuru kaka kwa kufungua ubongo wangu asubuhi ya leo ubarikiwe
[…] SOMA ZAIDI: Uchambuzi Wa Kitabu Cha UNFAIR ADVANTAGE […]