Hivi Ndivyo Na Wewe Unaweza Kuandika Kitabu Historia Ya Maisha Yako Kama Sugu


Miongoni mwa watanzania ambao wameandiaka vitabu vya historia ya maisha yao ni Sugu. Kitabu chake kinaeleza historia ya maisha yake kuanzia alipozaliwa mpaka anaingia bungeni mwaka 2010. Kina mambo mengi mzuri na ya kujifunza kwelikweli. Nashauri kama hujasoma kitabu cha Sugu, kinachoitwa Maisha na muziki ukisome. Utajifunza mengi sana ndani ya hiki kitabu. Tunaweza pia kuwasiliana kwa 0755848391 ili nikutumie nakala ya kitabu chako kwa bei chee tu.

Sasa baada ya kusema hayo tuone ni kwa namna gani wewe pia unaweza kuandika kitabu cha kwako.

Watu wengi wanafikiri kwamba kuandika kitabu kikubwa na kizuri kama hicho basi ni kazi kubwa. Hapana. Kuna njia mbili za kuandika kitabu kama hicho.

SOMA: UCHAMBUZI WA KITABU CHA SUGU MAISHA NA MUZIKI. Mambo 14 niliyojifunza kwenye kitabu hiki kinachoeleza Maisha ya Sugu Kutoka Mtaani Mpaka Bungeni

Kwanza ni kuanza kukiandika kidogo kidogo. Yaani, unakiandika hatua kwa hatua. Kwa mfano leo hii, tena sasa hivi unaweza kuamua kuanza kuandika historia ya maisha yako kwa kuandika jina lako na sehemu ulipozaliwa. Kesho ukaongeza kitu kingine kwa kuandika sehemu ulipokulia. Siku nyingine ukaandika namna ulivyosoma shule ya msingi. Siku nyingine ukaandika masomo uliyokuwa unapenda shule ya msingi. Siku nyingine ukaandika kuhusu ile siku uliyotoroka shuleni mwalimu akakuchapa.

Muda siyo mrefu utakuta kwamba kitabu chako kinazidi kusogea na mara kitabu chako kitakuwa kimeisha. Kitachukua muda kukikamilisha. Lakini nina hakika huu mchakato utaufurahia sana. kila siku utakuwa ukiandika maneno kidogo. Hata kama ni maneno 1000 tu, lakini utakuwa umeyaandika na yatakuwepo kwenye kitabu chako bila shida yoyote ile. Nashauri sana kama una mpango wa kuandika basi usisite kuanza kuandika sasa hivi, tena leo hii. anza tu hata kama ni kidogo

Bado huna uhakika ni kitu gani ambacho unaweza kufanya? Basi wasiliana name kwa 0755848391 ili niweze kukupa mwongozo na kukushikamkono wakati unaandika kitbu chako. Nimesaidia wengi wanaoandika vitabu vya historia ya maisha yao. Wewe unaenda kupata msaada pia. Karibu.

Njia ya pili ya kuandika kitabu cha historia ya maisha yako. Na hii ni kama uko bize tu. kama hauko bize tumia njia ya kwanza, itakufaa sana. Kwa njia hii ya pili, maana yake unatafuta mtu ambaye anaweza kukusaidia kuandika na kupangilia matukio ya kitabu chako. Unakuwa unawasiliana naye, na yeye anakusaidia kupangilia matukio ya kitabu  chako mpaka kinakamilika.

Unampa taarifa kwa njia ya sauti.

Mnafanya mahojiano. Na hata anawahoji watu wako wa karibu kidogo, kisha anakusaidia kuandika kitabu kilichopangiliwa vizuri na kinachosomeka.

Hizo ndizo njia mbili unazoweza kutumia kwenye kuandika kitabu chako.

Kitu kimoja muhimu sana kwenye hili hapa ni kwamba unapaswa kuandika kitabu chako. Usikubali kuacha historia ya maisha yako bila kuandikwa kwenye kitabu. Kamwe usikubali kitu kama hiki kitokee kwenye maisha.

Historia ya maisha yako, itawanufaisha sana wanao mpaka wajukuu wako.

Kila la kheri.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X