Njia pekee ya itakayokuhakikishia wewe kupata matokeo ya tofauti


Siku za nyuma niliandika makala niliyoipa kichwa cha Kama Unataka Mali: Maeneo Matano Unapoweza Kupata Mali Halali…

Kwenye makala hii nilieleza mbinu mpya za kupata Mali. Najua kwamba wengi tulisoma shairi la kama mnataka Mali mtazipata shambani, Ila sasa je, siku hizi na zama hizi tunazoishi,  bado tunapaswa kutegemea Mali kutoka shambani? Hapo ndipo nilikueleza hizo mbinu za kukuaidia kupata Mali kwenye hizi zama.

Sasa siku ya leo nina kitu Kimoja. Leo nataka nikwambie Kuwa kama unataka kupata matokeo ya tofauti. Rafiki yangu sharti unapaswa kukubali kufanya vitu vya tofauti.

Huwezi kuendelea kufanya vitu vilevile kila siku huku ukitegemea kupata matokeo ya tofauti.

Matokeo ya tofauti hayapo kwenye kufanya vitu vilevile kila siku. Kama unataka kupata matokeo ya tofauti, sharti ukubali kufanya vitu vya tofauti kwanza.

Kama unafanya kile ambacho kila mtu anafanya, utapata matokeo ambayo kila mtu anapata. Njia pekee ya wewe kupata matokeo ambayo hujawahi kupata Ni kufanya vitu ambavyo hujawahi kufanya.

Kama umeajiriwa, unaenda kazini muda ambao kila mtu anaenda kazini na muda wa kutoka unakukuta getini. Ujue wazi kuwa hutapata matokeo ya tofauti maishani mwako. Fanya kitu Cha tofauti, wahi kazini, fanya kazi kwa bidii, chelewa kidogo kutoka, pangilia ratiba zako.

Kama umejiajiri unafungua biashara au unaenda kazini unapotaka na kutoka unapojisikia, jua wazi kuwa hutakuja kupata matokeo ya tofauti. Sikiliza, Anza kwenda tofauti. Jitume kufanya kazi zaidi ya saa 15 kila siku. Kumbuka siyo saa 15 za kuwa macho na kuperuzi mtandaoni. Ni saa 15 za kazi siriazi.

Rafiki yangu, popote pale ulipo. Pambana kufanya kazi kitofauti na vile ulivyozoea.

Ukiendelea kufanya kazi kwa namna ulivyozoea nakuhakikishia kuwa hakuna MUUJIZA wowote utakaouona maishani mwako.

Kila la kheri.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X