Kama Unataka Mali: Maeneo Matano Unapoweza Kupata Mali Halali…


Unalikumbuka lile shairi la kama mnataka mali mtaipata shambani? Ila shairi hili…walilisoma baba zetu, sisi tumelisoma na sasa watoto wetu wanaenda kulisoma pia. Hahah

Kitu kikubwa kwenye hili shairi ni kwamba kama unataka mali utaipata shambani. Leo hii nilikuwa nafiria hivi kwamba huyu mwandishi wa hili shairi angekuwa analiandika sasa hivi, hivi kweli bado angeendelea kusema kwamba kama mnataka mali mtaipata shambani au angesema kitu kingine?

Hapo ndipo nimegundua kwamba dunia ya sasa imebadilika sana sana kuliko zamani hizo. Nadhani mwandishi wa shairi hili leo hii angekuwa anatunga tena hili shairi, kuna kitu fulani ambacho angeongezea na hicho ndicho nimeamua kukiandika kwa mfumo wa makala siku ya leo kwa hiyo kama unataka mali. Haya hapa ndiyo maeneo muhimu unapoweza kuipata.

KWANZA KAMA UNATAKA MALI UTAIPATA SHAMBANI

Nadhani tuanze na ushauri wa mwandishi wa shairi mwenyewe. bado shamba ni eneo zuri tu kutengeneza mali hata kwenye ulimwengu wa leo. hata hivyo kuna mabadiliko makubwa wakati shairi linaandikwa na wakati wa leo. Mashamba ya leo hii ni ya kidigitali. Ni kweli bado utapata mali shambani, ila sasa haupaswi kulima hovyohovyo,

  • unapaswa kulima kitalaalam na kufuata taratibu zote za kilimo.
  • unapaswa kulima huku ukitunza mazingira
  • unapaswa kutumia mbegu bora, kilimo kinaanzia kwenye mbegu, ukipanda mbegu mbaya utapata mavuno mabovu, unavuna ulichopanda.
  • Lima hata kwa kutumia vifaa vya kisasa kama greenhouse na mwangilia kwa kutumia mfumo wa kisasa kama drip irrigation. Hapa sasa ndio utafurahia kilimo.

siyo unaendelea kusema kwamba kama mnataka mali mtaipata shambani wakati unaendelea kulima kwa mbinu zilizopitwa na wakati. Utapata mavuno kidogo na mwisho wa siku kilimo utaona hakifai. tafuta watalaam wakuelekeze. Kwa hiyo napenda nimalizie hii pointi kwa kusema kwamba kama unataka mali utaipata shambani, ila sasa lima kisasa.

PILI KAMA UNATAKA MALI ANZISHA, KUKUZA BIASHARA YAKO

Moja ya njia ambayo watu wngi wanatumia kwenye kuingiza kipato ni njia ya AJIRA. ahata hivyo, hii njia ina kikomo. kila mwezi kuna kiwango fulani cha fedha ambacho unapewa na mwajiri wako. hakiongezeki sana sana na hata pale kinapoongezeka, ongezeko linakuwa ni dogo.

Ila sasa kuna huyu jamaa anaitwa biashara. malipo kwenye biashara hayana ukomo. Ukomo pekee kwenye biashara yako ni ule ambao wewe mwenyewe unajiwekea. kadiri unavyoikuza biashara yako, ndivyo ambavyo unaweza kupata mshahara mkubwa zaidi. hapo bado kuna faida ya biashara.

Kumbe kwenye ulimwengu wa leo, kama unataka mali, biashara ni sehemu nyingine unapoweza kupat mali..

TATU KAMA UNATAKA MALI UTAIPATA KWENYE UWEKEZAJI

Uwekezaji ni kitu kingine ambacho unaweza kufanya na kikakusaidia wewe kuingiza kipato bila hata ya wewe kufanya kazi. lakini kikubwa zaidi ni kwamba uwekezaji wenyewe ni mali. Kama utawezekeza vizuri, uwekezaji unaweza ukakufikisha mpaka kwenye uhuru wa kifedha.

Kuna uwekezaji wa aina mbalimbali,

  • uwekezaji kwenye majengo
  • uwekezaji kwenye soko la hisa
  • uwekezaji kwenye soko la mitaji
  • uwekezaji kwenye hatifungani, vipande n.k

Nashauri baada ya hapa uchague eneo moja ambapo unaenda kuwekeza, kisha uanze kulisoma na kulitafiti kiundani ili uweze kulielewa. Unataka kuwekeza kwenye hisa? Anza kwa kusoma kitabu changu cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE, gharama yake ni 5,000/- tu. Tuwasiliane kwa 0755848391.

NNE, KAMA UNATAKA MALI UTAIPATA KWENYE SEKTA YA AFYA

Hii ni sehemu nyingine ambapo unaweza kupata mali

Labda niseme tu kwamba kila mtu anapenda awe na afya bora. Mtu akiumwa yuko tayari hata ajikopeshe kwa ndugu jamaa na marafiki ili apate huduma za matibabu.

Kama alikuwa ameweka akiba yake anakuwa tayari kwenda kuitoa kwa ajili ya kutibiwa.

Kama wewe unaweza kuwasogezea watu huduma za matibabu karibu yao ni njia ya kutengeza kutengeneza mali pia

TANO KAMA UNATAKA MALI UTAIPATA KWENYE SEKTA YA ELIMU

Kuongezeka kwa watu kunafanya sekta ya elimu izidi kupamba moto pia. Hii ndio kusema kwamba shule zilizopo sasa hivi haziwezi kutosheleza ongezeko la watu.

Tena kuna sera na misemo mbalimbali kuhusu elimu ambazo watu wamezishikilia, wapo wanaosema elimu ni ufunguo wa maisha, wengine wanasema; elimu ni nuru/mwanga, elimu ni daraja n.k.

Sambamba na hiyo misemo kuna imani maarufu ambayo tayari ipo kwamba maisha bila shule hayawezekani. Kwa hiyo, lazima mtu aende shule asome kwa bidii ndiyo aweze kufanikiwa maishani mwake.

Kwa hiyo, lazima shule zijengwe nyingine mpya ili kukidhi matarajio ya watu kuhusu elimu. Na wewe unaweza kuchamgamkia fursa hii moja kwa moja na kuianza safari yako ya kutengeza mamilioni ya fedha.

HITIMISHO

Najua kuwa kuna maeneo zaidi ya haya, ila kwa leo nimekuletea hayo tu. Kama utapenda kujifunza zaidi, nashauri uhakikishe umepata ebook yangu inayoitwa SEKTA 11 ZA KUTENGENEZA MAMILIONI YA FEDHA TANZANIA. inapatikana kwa elfu tano (5,000/-)tu


2 responses to “Kama Unataka Mali: Maeneo Matano Unapoweza Kupata Mali Halali…”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X