Uchambuzi Wa Kitabu Cha The 5Am Club: (Mambo 304 niliyojifunza kutoka kwenye hiki kitabu)


Kitabu: 5 AM CLUB; Own Your Morning Eleveti Your Life
Mwandishi: Robin Sharma
Mchambuzi: Hillary Mrosso
Simu: 255 683 862 481

UTANGULIZI;

The 5 AM CLUB, imiliki asubuhi yako, uyaboreshe maisha yako. Ni moja ya vitabu bora sana katika zama hizi. Ni kitabu kilichoandikwa kwa ustadi wa juu sana, kila sentensi kwenye kitabu hiki ina ujumbe mkubwa. Mwandishi wa kitabu anatutaka tuzifufue ndoto zetu, malengo yetu, maono yetu tuliyoyaacha au kayakatia tamaa, anatupa sababu zote kwanini ndoto na maono yetu vinaweza kutimilika na kufanyika licha ya kuishi katika ulimwengu wenye usumbufu mkubwa. Ulimwengu wa kidigitali licha ya faida zake, umewalevya watu wengi na wameshindwa kuwa na muda wa kufanya mambo mihimu ya maisha yao. Mwandishi anatueleza jinsi inavyowezekana kupata umakini, utulivu na kukaa mbali na usumbufu wa mitandao ya kijamii ambayo imekuwa uharibifu wa ubunifu na mahusiano mengi. Kuamka mapema alfajiri imeelezwa kuwa kina kuwa inaweza kuwa ndio tabia bora sana itayayotufanya kupata muda wa kufanyia kazi yale yaliyo muhimu kwenye maisha yetu. Kwa mengi mazuri karibu tujifunze kupitia uchambuzihuu.

 1. Nimetoa kila nilichotakiwa kutoa kwa ajili ya kuandika kitabu hiki. Nawashukuru kila mmoja aliyefanya kwa namna yoyote ile uandishi wa kiatabu hiki kukamilika.
 2. Matumiani yangu makubwa ni kuwa baada ya kuandika kitabu hiki ni kuwa kitatuwa kitabu bora sana kitakacholeta mapinduza ya kweli kwenye maisha yako ili uweze kutumia vipawa na karama ulizonazo kutoa huduma bora hapa dunaini.
 3. Dunia inahitaji sana watu mahiri na magwij, kwanini umekaa tu ukisubiria wakati una uwezo wote wa kufikia umahiri na kuwa gwiji kwenye eneo lako, anza leo.
 4. Kwa chochote chenye thamani maishani mwako, hujachelewa au kuwahi kukifanya, na kama hujakifanya kwa sababu zozote zile, bado una nguvu za kuanza kukifanya kitu hicho.
 5. Kamwe usiruhusu moto wa kufanya makubwa uzimike ndani yako, usikubali kabisa kutoa nafasi kwa mambo yasiyo na tija kuharibu kiu yako ya kufikia mafanikio yako.
 6. Mwandishi nguli wa vitabu Any Rand aliwahi kusema usiruhusu shujaa aliye ndani yako aangamie kwa upweke na mafadhaiko kwa kukosa maisha uliyostahili na kuyatamani sana. Dunia unayoitamani bado ipo, ndoto unazotaka kuzifikia bado ni halisi, na inawezekana kufikiwa na kuishida na kumiliki.
 7. Jua kuwa umezaliwa katika fursa na wakati sahihi, hivyo una wajibu mkubwa wa kuwa mahiri.
 8. Sote tumeumbwa kufikia ukuu wa juu sana, na tumeundwa kwa namna ya kipekee katika kutimiza malengo yetu kwa viwango vya juu sana ili kuifanya sayari hii kuwa sehemu nzuri ya kuvutia.
 9. Unao ndani yako ukuu, nguvu kubwa ambao umeshindwa kuuonyesha kutokana na jamii yetu kubariki na kuridhika na kiasi kidogo sana cha mafanikio tunaoonyesha.
 10. Mwanadamu ameumbiwa ukuu katika maisha yake, na anakazi kubwa ya kufanya ili kuudhihirisha ukuu huo kwa ulimwengu.
 11. Badala ya kuhangaika kutafuta heshima na ukuu kwa watu wengine, tunatakiwa kuwekeza vya kutosha katika maisha yetu ili kuchimbua na kuvitumia vipawa vyetu kwa viwango vya juu sana, kwa kufanya hivyo heshima na ukuu utatujia bila kuutafuta kwa njia za aibu na kuumiza wengine.
 12. Wengi tunadhani maisha mazuri na yanayotuletea heshima, furaha na ukuu ni kumiliki vitu vya gharama. Maisha mazuri na yanayoleta heshima, ukuu, furaha na amani ni kuishi kusudi la kuumbwa kwetu kwa kuwa sehemu ya kuinua na kufanya maisha ya binadamu wenzetu kuchanua na kuwa bora.
 13. Moja ya kazi kubwa unayotakiwa kufanya kama kiongozi ni kujisimamia mwenyewe hasa katika zama hizi za technolojia na mitandao ya kijamii, ambayo kwa kiasi kikubwa imefanya wengi kuwa watumwa wa mitandao hiyo.
 14. Epuka kwa nguvu zako zote utumwa wa kidigitali, fanya kazi kubwa kuwa huru mbali na ulevi na urahibu wa kidigitali, maana wengi wameshindwa kujenga maisha yao binafsi kwasababu ya kutumia muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii.
 15. Ili uwe mtu huru na mwenye umakini mkubwa kwenye kufanyia kazi ndoto zako, malengo yako ni kuhakikisha unatawaliwa na mazingira yasiyokuwa na usumbufu hasa usumbufu wa kidigitali, ambao kwa sasa ndio unaochangia kudumaza na kupunguza ufanisi kwenye kazi.
 16. Watu wakuu waliowahi kuisha na wanaoishi sasa ni watoaji na sio wapokeaji pekee. Wengi tunafurahia kazi zao zilizotukuka, kwa sababu walijitoa sadaka kukamilisha kazi bora ambazo zinadumu kwa vizazi vingi.
 17. Siku zote fanya kazi ya kishujaa itakayowashangaza wote watakaopita au kuiona kazi yako, fanya kwa ubora wa juu sana, zalisha kwa viwango vikubwa sana, shangaza soko lako kwa ubora, uimara na uhalisia wa kazi au bidhaa zako.
 18. Wakati ukipambania kufikia ndoto zako, tengeneza maisha yako binafsi katika viwango vya juu sana vya maadili ambayo hayatayumbishwa na kitu chochote kile, kwa kufanya hivyo utalinda amani na utulivu wako wa ndani na malaika watakuwa marafiki zako na utakuwa na sehemu katikati ya miungu.
 19. Kila binadamu anayeshi hapa duniani ana wito mkuu juu ya maisha yake, na kila mmoja wetu hapa duniani amebeba silika ya ya roho ya ubora katika viwango vya kiungu.
 20. Hakuna mtu ndani ya roho yake anakubaliana na hali ya kuishi maisha mgando au maisha ya wastani yasiyozalisha na kutoa ubora ambao unaweza kusaidia kuboresha maisha ya watu wengine.
 21. Vizuizi na ukomo vyote huanzia kwenye mawazo yetu, mawazo yetu yakikubaliana na ukomo tunaojiwekea ndivyo itakavyo mara zote. Mawazo yetu yakibadilika na kuanza kuona picha kubwa tunaweza kuchukua hatua na kufikia ndoto zetu.
 22. Mwandishi wa kitabu hiki anasema inahuzunisha na kuvunja moyo wake kuona watu wenye nguvu na uwezo wa kufanya makubwa wamekwama kwenye maisha kwa kuziamini hadithi kwamba hawawezi kufanya makubwa au hawawezi kuwa wakuu na watu mashughuri.
 23. Tunahitaji kukumbuka kuwa visingizio vyote tulivyonavyo vya kutofikia ndoto zetu ni vya udanganyifu, na woga tulionao ni uongo, na mashaka tuliyonayo ni wezi wa muda na maisha mazuri tunayoyatamani.
 24. Hata kama unapitia nyakati ngumu kwenye maisha yako, jua kuwa wewe sio wa kwanza, sote tunapitia nyakati ngumu pia, amua kutokata tamaana uendelee na safari yako ya kuvumbua ukuu na umahiri uliojificha ndani yako.
 25. Kuna wakati kwenye maisha unaona haupo sehemu sahihi, unaona nguvu zako zikipotea, unaona hauna watu sahihi, unaona ukikabiliana na vitu ambavyo hukustahili kukabiliana navyo. Mambo yamebadilika kuliko ulivyodhania, unaona unaishiwa nguvu na una kila sababu ya kukata tamaa, haya yote na zaidi yanatokea kwenye maisha na kuna wakati yanatufanya tujitafute na kujiangalia kama tunaenda sawa kwenye maisha.
 26. Changamoto za maisha zisikufanye utoroke majukumu yako muhimu ya maisha kama vile kujenga misingi imara ya kuzifikia ndoto zako. Wengi wanatoroka changamoto na kuzamia kwenye mitandao ya kijamii na hapo ndipo wanapoishia kuwa watumwa wa kidigitali.
 27. Mitandao ya kijamii inatakiwa iwe sehemu ya kuongeza ufanisi na ukuaji kwenye maisha binafsi, biashara na kazi na sio sehemu ya kutufanya watumwa wa vifaa hivyo.
 28. Tunakosea sana pale tunapokuwa tunaishi maisha hay ohayo kila wiki na kila mwezi na kuita mtindo huo ni maisha. Hii ndio maana mwandishi anasema wengi walishakufa miaka 30 iliyopita na wanazikwa miaka 80 ijayo.
 29. Tunatakiwa kuishi maisha yenye mabadiliko chanya kila wakati, tunatakiwa kufanya mabadiliko chanya kwenye maisha yetu, tuepuke kuishi kama wafu, yani miaka yoote, tuko vile vile, elimu ile ile, maarifa yale yele, chakula kile kile nk. Maisha yanakuwa na mvuto na kusisimua pale panapokuwa na ukuaji.
 30. Unaowaona hapa duniani wakiwa katika kilele cha mafanikio yao na kufanya kila walichofanya ili kufikia ndoto zao, kuwa na familia zenye furaha, na kuwa msaada kwa jamii zao na hao walipitia nyakati ngumu na za giza na wakaamua kuendelea mbele.
 31. Maisha unayoishi yamejaa usalama kiasi cha kuharibu ubunifu wako, kuua ukuu wako, kuweka ganzi ili usichukue hatua za kufikia ndoto zako, kutengeneza hofu zisizo halisi zinazo saliti ushujaa na umahiri unaoweza kuuonyesha kwenye hii dunia.
 32. Endapo tutaendelea kujifungia katika eneo la faraja na usalama basi tutakuwa na uwezo mdogo sana wa kuchimba migodi tuliyobeba, na hakuna cha thamani kinachoweza kupatikana endapo tutaendekeza kukaa kwenye comfort zone.
 33. Unahitaji ushujaa na ujasiri mkubwa kuingia kwenye mapambano makali ya vita kati nafsi yako, mwili wako na roho yako. Amua kutangaza vita isiyoisha juu yako mwenyewe ili ujikomboe na umiliki utayari wako, mawazo yako, hisia zako, nguvu zako, umakini wako, na ndoto zako.
 34. Usipokuwa tayari kujimiliki wengine watatumia hiyo nafasi na watamiliki maisha yako, watayachezea na kuyafanya watakavyo. Amua kwa dhati kuwa utashika hatamu ya maisha yako na hutamuachia mtu yeyote maisha yako.
 35. Usijirahisishe kiasi cha kujiuza kwa bei rahisi kwa walimwengu. Yathaminishe maisha yako na kuyafanya ya viwango vya juu sana kwa kufanyia kazi ndoto zako, malengo yako, kwa kufanya hivyo utajiweka kwenye daraja la juu sana la wakuu na watu mashughuhuri hapa duniani.
 36. Yapende maisha yako, huna maisha mengine zaidi ya hayo uliyonayo, jipe Jukumu gumu la kuyajenga maisha yako kwa viwango vya kiungu, jenga maisha yako yawe kielelezo kwa vizazi vya sasa na vizazi vingi vijavyo.
 37. Jipe Jukumu la kujenga nidhamu ya hali ya juu katika udhibiti wa hisia, fedha, muda na rasilimali nyingine muhimu kwenye maisha. Jenga maisha yatakayowatamanisha wengi.
 38. Jua kuwa una uwezo mkubwa sana ndani yako kuliko unavyojifahamu sasa, una uwezo wa kushinda na kuyageuza mambo yote mazuri yaliyokufa ndani yako kuwa hai ya yenye utukufu.
 39. Na hapo ulipo sasa ni sehemu sahihi kwenye maisha yako kupokea ukuaji wa kila eneo la maisha yako, ili uweze kuzalisha matokeo ya kipekee na kutengeneza ushawishi ambao ulifikiri hauna.
 40. Hivyo jua hakuna kilicho kibaya kwa wakati huu kwenye maisha yako, hata kama unaona kila kitu hakipo upande wako, au mambo hayaendi kama unavyotaka, jua kuwa unapitia sehemu muhimu sana kwenye maisha yako. Kwasababu usipopitia mambo magumu kwenye maisha yako huwezi kukua au kuboresha chochote kwenye maisha.
 41. Na pia kama unaona majanga yamekuwa mengi sana kwenye maisha yako tambua kuwa huenda hofu zako zimekuwa na nguvu zaidi kuliko Imani yako, hivyo kwa kufanyia mazoezi sehemu zenye udhaifu katika maisha yako unaweza kuizima sauti ya hofu inayoibuka na kukutia hofu na mashaka.
 42. Kuna wakati ili uongeze ushindi kwenye maisha yako, unatakiwa kukubaliana na ukweli mchungu kuwa changamoto nyingi unazopitia, watu wabaya unaokutana nao, na majaribu yote yanayokupata ndio yamekuandaa kuwa mtu imara uliye sasa.
 43. Mwandishi anasisitiza kuwa, unahitaji kupitia changamoto hizi na masomo magumu ili uweze kutumia uwezo wako mwingine uliojificha ndani yako, hazina ya nguvu zako zilizopo ndani yako zinahitaji upitie kwenye magumu na changamoto ili zitokee na zikusaidie na zikuache ukiwa mshindi, na mwenye furaha.
 44. Hakuna bahati mbaya wala kupoteza kwenye safari ya kuishi ndoto zako, yote uliyopitia ni masomo muhimu sana katika kujenga misingi imara ya maisha yako ambayo itakufanya uendelee kutumia uwezo wako kwa viwango vya juu sana
 45. Kuwa na wazo bila kulifanyia kazi ni bure kabisa, hata kama unachukua hataua ndogo kiasi gani katika kufanyia kazi wazo lako, inaweza kuwa ni bora sana kuliko kutofanya chochote.
 46. Ingekuwa kuwa mtu mashuhuri, hodari na mwenye mafanikio makbwa ni kazi rahisi basi kila mtu angejipatia sifa hiyo. Kazi kubwa mno inahitajiki ili kutumia uwezo wako, talanta zako na hazina zilizopo ndani yako.
 47. Kuna wakati kwenye maisha yetu tunapata raha ambazo zinatugandisha kwenye eneo la usalama, yaaani comfort zone, na tunadanganywa na jamii yetu kuwa ukuu na ushujaa hauitaji kufanyia kazi vipawa vyetu ili kutoa matokea bora ya viwango vya juu.
 48. Kuishi maisha yasiyo na uhalisia kwa kufuata mambo rahisi rahisi yanatufanya tushindwe kuwa watu imara ambao wanaweza kusimama kidete kutetea ndoto zao kwa nguvu zao zote.
 49. Ukitaka kuwa mtu unayefanya mambo kwa viwango vya juu, unatakiwa uondoke kabisa kwenye maisha laini na kutaka vitu rahisi rahisi, unatakiwa kuwa zaidi ya wengi wanaokuzunguka ili uibuke shujaa na hodari.
 50. Na wakati mweingine tunaona kama tumekosea njia ya mafanikio pale tunapoona mambo ni magumu. Kuelekea kwenye umahiri wa viwango vya juu unahitaji sana uvumilivu maana mambo sio rahisi kwenye njia hii ya kufikia mafikio makubwa.
 51. Tumehimiza umatamaduni laini ambao umezalisha watu laini na dhaifu wasioweza hata kutimiza ahadi zao, tumekuwa na watu ambao hawafai hata kuwekewa dhamana kutokana na kuwa na uwezo wa chini mno katika kutimiza waliyoahidi, tuna kizazi cha ajabu sana ambacho hakiwezi kubeba majukumu, tuna watu laini mno ambao wakiona changamoto kidogo tu kwenye njia yao ya mafanikio wanakata tamaa na kuacha kuendelea.
 52. Mwandishi wa kitabu hiki anasema ugumu ni mzuri. Ukuu wa kweli na dhamira ya kufikia kilele cha mafanikio haujaandaliwa kuwa rahisi, hakuna urahisi katika kufikia ndoto unazozitamani, itahitaji ujisukume na kujitolea vya kutosha kila siku ili kufikia kingo za mwisho kabisa ili kutoa uwezo na ukuu ulio ndani yako.
 53. Jiongeze kila siku kujisukuma kufanya zaidi na kuchukua hatua za ziada katika kufikia kilele cha ndoto zako; haijawahi kuwa rahisi safari hii jifunze kwa waliofanikiwa.
 54. Moja kati ya vitu vitakavyokupa furaha na amani maishani mwako nikujua kuwa ulifanya kila ulichoweza na kutoa kila kilichotakiwa ili kufikia mafanikio uliyoyapata.
 55. Mfano, gwiji wa muziki wa Jazz Miles Davis alijisukuma na kujitolea isivyo kawaida ili kutumia vipawa na uwezo wake wa kipekee uliokuwa ndani yake kuzalisha kazi bora ya mziki hapa duniani.
 56. Michelangelo alijitoa sana kiakili, kihisia, kimwili na kiroho alipokuwa anatengeneza Sanaa yake iliyobakia kushangaza ulimwengu kwa uzuri na ubora wake wa hali ya juu.
 57. Aina hii ya kujitoa bila kujibakisha ili kutimiza malengo makubwa na yenye manufaa kwa jamii nzima yanahitaji sana kujitolea mno, kwa sasa ukionekana unaweka juhudi kubwa kiasi hiki katika zama hizi watu wanaweza kukuita chizi.
 58. Hivyo, sehemu ambapo usumbufu wako mkubwa upo huenda hapo ndipo penye fursa zako. Fursa zimejificha kwenye mambo magumu, kwenye hatari, kwenye shida, na kwenye changamoto.
 59. Huenda una mawazo yasiyokuachia, kuna hisia zinakutisha, kuna imani zinakusumbua, kuna miradi unaiwaza usiku na mchana, kuna wakati unapata hofu kufanya mambo makubwa, ni kwambie tu ukweli unatakiwa kuzikabili bila kuziogopa, unatakiwa kuziendea njia za hofu maana huko ndio utaona thamani kubwa ya maisha yako na nguvu kubwa uliyonayo katika kukabiliana na mambo magumu na ya kutisha.
 60. Nguvu yako kubwa itagundulika na itatumika vizuri endapo utajipa nafasi ya kipekee kuzikabili hali zote zinazokuogopesha, hutajua uwezo, ubunifu, vipawa na uwezo wako wa kipekee kama hutazikabili changamoto zinazokuzonga.
 61. Usizikimbie kabisa changamoto, wala mambo yanayokutisha, jinsi unavyojihusisha na utatuzi wa changamoto na magumu yanayokuja kwenye maisha yako ndivyo unavyokuwa na utawala wa kweli kwenye maisha yako, na kwa kufanya hivyo utakuwa mtu huru na hodari.
 62. Mwanafalsafa Marcus Aurelius aliwahi kusema, usiishi maisha yako kama vile una miaka elfu kumi ya kuishi. Kifo kipo karibu kuliko unavyofikiri. Kazana siku zote kuishi maisha yenye maana, kazana siku zote kujitengeneza kuwa mtu bora kabisa kuwahi kuishi hapa duniani.
 63. Kuna watu wanaota na kutamani tu vitu vizuri na bora vitokee kwenye maisha yao. Sheria ya asili haifanyi kazi namna hiyo, tenegeneza mwenyewe, fanyia kazi mwenyewe kila kitu unachotamani kitokee kwenye maisha yako, hakuna kitu kizuri na bora kitakuja chenyewe kwenye maisha yako kama ajali, fanyia kazi matamanio yako.
 64. Mwandishi wa kitabu hiki Robin Sharma, ametufundisha kwa kina moja ya tabia muhimu sana tunayotakiwa kuwa nayo kwenye maisha ili tuweze kufanyia kazi ndoto zetu na kuweza kutumia uwezo wetu mkubwa ulio ndani yetu ni kuisimika tabia ya kuamka mapema asubuhi yaani saa 11 alfajiri (5 AM).
 65. Umuhimu wa kuwa na tabia ya kuamka mapema zaidi ndio umefanya Robin Sharma kutumia muda mwingi kuandika kitabu hiki bora kabisa hasa katika zama hizi za mitandao ya kidigitali.
 66. Uzoefu wake kama mwalimu na kocha, na pia baada ya kujifunza kutoka kwa magwiji na watu mashighuri na wenye historia ya kufanya makubwa katika dunia hii unaonyesha wengi wakiwa na tabia ya kuamka mapema zaidi kuliko binadamu wengine.
 67. Wnapoamka mapema wanafanya moja ya majukumu muhimu sana katika kutimiza ndoto zao, wanafanya mazoezi, wanafanya tahajudi, wanasoma na kujifunza kwa kina katika muda huu wenye utulivu mkubwa.
 68. Muda wa asubuhi ndio muda bora sana kufanyia kazi ndoto zako, maana muda huu hakuna usumbufu wa aina yoyote na watu wengi wemelala, mwili na akili yako vinakuwa kwenye ufanisi wa hali ya juu, hivyo ni rahsi kukamilisha mambo muhimu kwenye maisha yako.
 69. Mwekezaji maarufu sana duniani, Warren Buffett aliwahi kusema, matajiri wanawekeza kwenye muda, masikini wanawekeza kwenye fedha. Matumizi ya muda unaopita kwenye maisha yako ni muhimu sana kuliko hata fedha, muda ndio huamua aina ya maisha na mafanikio yako, pangilia vizuri muda wako tangu siku inapoanza hadi inapoisha.
 70. Chagua mwenyewe utafuata upande gani, utaifuatisha dunia hii upotee pamoja na ndoto zako? Au utaamua kuingia gharama za kuitumikia ndoto yako bila kujali utaumia kiasi gani. Chagua maana huwezikufanya vyote.
 71. Sifa zienda kwa mtu ambaye mara zote yupo kwenye uwanja wa mapambano akipambania kufikia malengo na ndoto zake, sifa ziende kwa yule anayejisukuma na kuanguka na kuinuka tena na tena na kurudi uwanjani kupambania kufikia ukuu na umahiri katika kutumia vipawa vyake alivyojaliwa na Mungu. Sifa ziende kwa wale wanaoamka mapema zaidi kuliko wengine, kwa lengo la kufanyia kazi malengo yao. Maana watu hawa ndio watakaoibariki dunia kwa vipawa vyao.
 72. Mwandishi anasema kwenye biashara zake huwa anafanya kazi na watu wanaojituma sana na kutumia uwezo wao wote kufanya makubwa, alimaanisha huwezi kuwa kazi ya kiwango cha daraja A ukataka ifanyike na mtu wa daraja C.
 73. Watu waliokuzunguka wanachangia sana katika kujenga mtazamo wako, pia hata vitabu unavyosoma vina mchango mkubwa sana katika kujenga mtazamo wako. Hivyo angalia watu au vitu vilivyokaribu yako vianaweza kuathiri kwa kiasi kikubwa mtazamo wako wa maisha.
 74. Kama unafanya biashara au unajihusishana masuala ya biashara, sababu kuu ya kuingia au kuwa kwenye biashara isiwe kupata fedha pekee, bali iwe kuinua na kuboresha maisha ya watu wengine.
 75. Fedha inatakiwa iwe ni zao au matokeo ya huduma bora unazozitoa kwenye jamii ili kuboresha na kuyafanya maisha ya wateja au watu wanaonunua au kutumia bidhaa zako kuwa bora.
 76. Kila binadamu hapa duniani ana ukuu ndani yake, na ili huo ukuu uonekane kuwanufaisha wengine inabidi uweke mipango ya muda mfupi na muda mrefu itakayokufanya uchukue hatua za kuonyesha ukuu wako kwa dunia kwa kutoa huduma bora kupitia kipaji au kipawa chako.
 77. Kumbuka ulivyokuwa mtoto ulikuwa na ndoto za kuwa mtu mkuu, ulikuwa na ndoto za kuwa mtu mahiri, lakini jinsi unavyokuwa mtu mzima ndoto hizo zimefifia na kupotea kabisa, wakati mwingine hata huzizungumzii kabisa.
 78. Usiisaliti ndoto yako na ukuu ulio ndani yako, fanya kila unachoweza, toa kila kinachotakiwa kutolewa ili ukamilisha malengo yako makubwa.
 79. Jenga tabia mpya zitakazokusaidia kufikia kwenye kilele cha mafaniko kwenye ndoto yako, mojawapo ya tabia nzuri kujenga ili uanze kuifanyia kazi ndoto na malengo yako makubwa ni kuanza kuamka asubuhi na mapema saa 11 alfajiri au zaidi.
 80. Kwa kujenga tabia nzuri na mpya za kuamka mapema kabla ya dunia kuamka, utakuwa umeisimika tabia ya kuwa mtu wa kuamka mapema zaidi na utaimiliki asubuhi yako na utayainua au kuboresha maisha yako.
 81. Dhamiria kabisa kuwa na tabia ya kuamka mapema zaidi ya wengine, inaweza kuwa kuanzia saa 11 alfajiri. Muda huu una utulivu mkubwa, muda huu mwili wako unakuwa na nguvu, akili yako inaweza kufikiri kwa kina, na hapo ndipo unapotakiwa kushughulika na mipango na ndoto zako kubwa.
 82. Kuwa sehemu ya watu wachache sana waliowahi kuishi hapa duniani na kuibariki kwa vipaji vyao, kwa kufanya zaidi ya wengi walio lala usingizi na kuua kabisa ukuu walioumbiwa.
 83. Usizimishe taa ya ukuu wako, ubunifu wako, upekee wako, ujasiri wako, umahiri wako na uhodari wako ambao utatokea endapo utachukua juhudi za makusudi za kuamka mapema na kuanza kufanyia kazi vipawa ulivyopewa.
 84. Maumivu, kuvuja jasho na kuteseka ni kwa muda tu, lakini majuto na kujutia ni vya milele. Shughulikia maisha yako ya baadaye sasa, usimwachie mtu mwingine.
 85. Ingia kwenye hstoria ya watu wachache walioibadili dunia, ingia kwenye dunia ya watu wachache wenye akili nyingi, ingia kwenye dunia ya wacheche wenye ujasiri wa kuziishi ndoto zao, ungana na magwiji wengine duniani kwa kuamka mapema zaidi.
 86. Jipe nafasi, jipe bahati, jipe upendo, jipe furaha, jipe amani, jipe mafanikio makubwa, jipe fedha, jipe utawala wa kudumu wa nafsi yako, mwili wako, na roho yako. Jitoe bila kujibakiza, jitoe bila kujionea huruma, fanyia kazi matamanio yako, ndoto zako, malengo yako.
 87. Kumbuka kila ulichopitia ni kizuri na kinafaida yake kwenye maisha yako, maana baada ya kupitia magumu, utajua ni kipi sahahi kwako, ni kipi sio sahihi, magumu yamekufanya kuwa mtu imara, yameondoa na kuchoma udhaifu ulio nao na kuondoa kiburi na majivuno ndani yako, magumu yanakufanya uwakumbuke wengine na kuisha maisha yako kwa unyenyekevu.
 88. Shujaa mmoja wa kivita anayeitwa Sapartan aliwahi kusema, mtu anayetoka jasho na damu nyingi wakati wa mafunzo atatoka damu kidogo wakati wa vita.
 89. Hii ina maana maandalizi ni muhimu sana kwenye jambo lolote, hivyo na jinsi unavyokuwa na maandalizi ya kutosha na mafunzo mengi ya kutosha, huta pata taabu wakati wa kufanya jambo lako.
 90. Kumbuka mafunzo yoyote yanahusisha maumivu, uchungu, kuumia, na hata wakati mwingine mateso makali. Wekeza zaidi kwenye maandalizi na mafunzo makali katika kufanya mambo yako, jipangie muda mwingi wa kujinoa na kujiandaa kwa uvumilivu mkubwa.
 91. Ushindi wa siku yako unapatikana kwenye masaa ya mwanzo kabisa wa siku yako, wakati ambapo dunia imelala na hakuna mtu anayekuona.
 92. Ukitaka ushindi kwenye siku yako, jifunze kuamka mapema zaidi, fanya yote muhimu kwenye masaa unayoamka mapema, kamilisha na imiliki asubuhi yako kwa kufanya yale muhimu na yenye tija.
 93. Watu waliofanikiwa sana na kufikia kwenye kilele cha mafanikio ya world class, au mafanikio ya juu sana, wana utaratibu wa kuamka mapema zaidi kablya ya jua kuchomoza, wanafanya yale ya muhimu katika muda huo wenye utulivu.
 94. Dhana ya kuamka mapema zaidi yani saa 11 alfajiri ni muhimu sana hasa kwatika zama hizi za fujo za mitandao ya kijamii, ambazo zimekubikwa na usumbufu mwingi sana.
 95. Kiukweli, hakuna asiyeweza kuamka mapema na kuanza siku yake kwa ushindi, kila mtu anaweza kuamka mapema na kufanyia kazi mipango yake.
 96. Chukua umakini wa hali ya juu kwenye masaa yaliyo mbele ya siku yako, maana yakiharibika yanaharibu siku yako yote, na yakipotea hayarudi kamwe. Hivyo imiliki siku yako na kuitawala kwa kuhakikisha unaamka mapema zaida na kufanyia kazi mipango yako muhimu.
 97. Watu wakuu na waliofanya makubwa duniani hawakurithi uwezo huo kutoka kwa wazazi wao, wala hawakuzaliwa na vinasaba maalumu vya kuwafanya wawe wakuu. Badala yake ni tabia bora kabisa walizoamua kujijengea kwenye maisha yao ndio zimewapatia ukuu na umaarufu walio nao kutokana na kazi bora wanazozifanya.
 98. Sahau kabisa kuhusu vipaji maalumu, au vinasaba vya kurithi unapozungumzia kazi bora, mafanikio makubwa, haya yanatokana na kazi kubwa mno waliyoifanya wakiwa nyuma ya pazia, walijitoa sana kujenga na kutoa matokeo ya viwango vya kimataifa.
 99. Tabia ni muhimu sana kwenye mafanikio yoyote, hakuna kinachoweza kuleta matokeo ya haraka kwenye maisha yako kama hakuna uwekezaji bora kwenye ujenzi wa tabia bora. Mfano, kama unataka utajiri basi uwe na tabia za kitajiri.
 100. Wanamichezo maarufu, magwiji wa biashara, wabobezi na wanasayansi wakubwa tunaowajua leo, waliwekeza kwenye tabia zilizowaletea mafanikio waliyoyapata, hakuna kilichotokea kwao kama ajali.
 101. Uvumilivu na kujitoa sadaka ili kukamilisha jambo ni tabia tunayotakiwa kuwa nayo kwenye safari ya mafanikio.
 102. Tukiwaangalia watu wengi waliofanikiwa duniani, waliwekeza nguvu zao zote, umakini wao wote na muda wao mwingi kwenye kufanya jambo moja, au mambo machache kwa ubora wa hali ya juu sana, na hivyo wakazalisha matokeo ya viwango vya juu sana.
 103. Wengi wetu leo hatuna ufanisi na hatuzalishi matokeo bora ya viwango vya juu kwa sababu tuhangaika na mambo mengi kwa wakati mmoja, hatuna umakini kwenye mambo tunayoyaanzisha, tunasumbuliwa sana na kila fursa inayokuja mbele yetu hivyo hatuna nguvu ya umakini.
 104. Angalia moja wapo ya malengo yako, chagua moja au mawili, kisha yatengee muda wa kutosha kuyafanyia kazi, weka umakini wako wa hali ya juu, jitolee kwa viwango visivyo vya kawaida katika kulifanya jambo hilo, weka msimamo dhabiti na usioyumbishwa na chochote katika kulifanyia kazi jambo hilo, kamwe usitawanye umakini wako na pia onyesha uvumilivu wa hali ya juu katika kutekeleza jambo lako.
 105. Kumbuka kila mtaalamu na gwiji unayemuona sasa alianzia chini na hatua chache, alingangana bila kukata tamaa, alivumilia magumu mengi na kushindwa kwingi kabla ya kufikia ukuu alio nao.
 106. Usiogope unapoanza chini kwenye jambo unalolianza, jipe muda na utulivu wa kutosha, jitoe vya kutosha kufanya kila unachoweza kufikia kilele cha mafanikio yako, ukianguka inuka, jifunze na endelea kupigania malengo yako.
 107. Dhibiti kwa dhati kila aina ya uharamia unaotaka kukutoa kwenye umakini wako unapofanya jambo lako, maharamia wanaweza kuwa meseji na mitandao ya kijamii ambayo inakutamanisha uendelee kuitumia.
 108. Jenga ukuta mkubwa sana kati yako na usumbufu wa mitandao ya kijamii, jijengee kwenye jela ya kwako yenye utulivu ambao utakuifanya utoe kazi bora za kibunifu.
 109. Mitandao ya kijamii sio afya tena siku hizi, imetengenezwa kwa namna ya kutufanya tuharibu ubunifu wetu, kupunguza nguvu zetu za kufikiri, na hata wakati mwingine kuondoa furaha zetu kwa kuanza kujilinganisha na watu tunao waona kwenye mitandao hiyo.
 110. Sayansi inasema hata miale na mionzi inayotoka kwenye simu zetu au komputa zetu sio mizuri kwa afya zetu za kiakili na kimwili. Hivyo usiendekeze sana kutumia mitandao hiyo. Kuwa na muda mchache sana wa kuitumia pale inapobidi.
 111. Kila mtu anapenda uhuru kwenye maisha yake, lakini hakuna uhuru usio na gharama, utaingia gharama ya kukosa starehe za kuangalia vinavyoendelea kwenye mitandao, uhuru wa kweli ni kutosumbuliwa na jambo lolote na kuwa na utawala na udhibiti wa maisha yako kwa asilimia 100.
 112. Tengeneza na wekeza vya kutosha katika upekee wako na uachane kufuatilia mambo ya watu wengine ambayo hayana tija kwako. Wekeza ndani yako vya kutosha ile uwe wa kipekee na uzalishe matokoea ya kipekee.
 113. Kila mmoja wetu ameumbwa ili kutengeneza historia yake ya kipekee kwa upekee wake aliozaliwa nao, amua kufanyia kazi ndoto zako zisizokuacha tangu ukiwa mdogo, hizo ndio zitakazokupa upekee kwenye eneo lako.
 114. Wengi katika zama hizi wanaishi maisha ya kuigiza na yasiyo halisi, wapo bize kwenye mambo yasiyo na tija, wanakazana na kukimbizana na vitu visivyo halisi vya juu juu tu. Ni wachache sana wanaoisha maisha halisi.
 115. Ni hasara sana, na inavunja moyo sana kutumia masaa yako ya asubuihi kufanya mambo yaiyo na msaada kwenye maisha yako. Usipoteze muda wako wa thamani kufukuzia mambo yaliyo nje ya ndoto na malengo yako.
 116. Moja ya kazi kubwa ya kiongozi ni kuwafanya waliokata tamaa na kuziacha ndoto zao waziamini tena, wasio na maono wawe na maono, wasio na imani wawe na imani, na wasiojiamini wajiamini.
 117. Mwandishi anasema, kama kila kitu kwenye maisha yako kionaonekana kipo kwenye udhibiti, basi ujue bado maisha yako hayaendi kwa kasi inayotakiwa, yaani unakua taratibu sana, au hakuna kinachokua kwenye maisha yako.
 118. Simu yako, simu janja au smartphone, itakugharimu sana maisha yako ya baadaye kama unaitumia kutwa nzima kufuatilia yasiyo na tija.
 119. Changamoto na dhoruba zinazokuja kwenye maisha yako zinakupima kujua kama una dhamira ya dhati ya kutaka mafanikio makubwa, dhamira ya dhati ya kufikia ukuu.
 120. Pressure ni nzuri kwenye maisha maana zinatusukuma kwenye kufikiri kwa kina na kuwa wabunifu ambao watazalisha matokeo bora ya ubunifu.
 121. Kama una dhamira ya kweli kufikia kilele cha mafanikio, kufikia ukuu, au kuwa gwiji na mtu hodari basi unatakiwa kuwa kiongozi mzuri kwako binafsi.
 122. Hakuna kitu kizuri kama kujiongeza na kukua kila siku, unaposhindwa kitu au kuanguka katika jambo Fulani, hii ndio fursa nzuri ya kukua na kuwa mtu bora.
 123. Mwandishi wa vitabu Tolstoy aliwahi kusema, kila mtu anafikiria namna ya kuibadili dunia, lakini hakuna aliyetayari kujibadili. Mabadiliko ni rahisi sana kuyatamka na kuyasema, ila sio rahisi kuyatekeleza.
 124. Sehemu ya maisha yako inayokutia hofu inatakiwa isulubiwe na kufa, ili kuwe na ufufuo wa heshima na utukufu na maisha mapya ya ujasiri na furaha.
 125. Ili uweze kujipata wewe uliyebora zaidi, unahitaji uwe tayari kujipoteza wewe uliye dhaifu.
 126. Kama hutainuka kila wakati na kila siku kwenye maisha yako, ili kujiboresha, kujithathmini, bado utaandamwa na majanga mengi yasiyokoma.
 127. Maafa makubwa maishani sio vifo, bali ni vile vitu vyenye ukuu tunavyoviacha vife ndani yetu wakati tukiwa hai.
 128. Tukitaka kuwa na mabadiliko makubwa ndani yetu tunatakiwa kuwa na uhusioano mzuri na sisi wenyewe. Kama huna uhusiano mzuri na wewe binafsi huwezi kuwa mtu wa kuleta matokeo yenye maana maishani.
 129. Kazana kujielewa na kuwa na mahusiano mazuri na bora kati yako mwenyewe, mahusiano mazuri binafsi yatakufanya ujikubali, ujiamini, ujitambue na kutumia ubunifu wako wa kipekee kufanya makubwa kwenye maisha yako na maisha ya watu wengine hapa duniani.
 130. Kuna watu hawezi kukaa peke yao, hawawezi kujisimamia wenyewe, mara zote huwa wanapenda kuishi kwa makundi na kusimama kwenye migogo ya watu wengine.
 131. Mwandishi anasema, watu wasioweza kujisimamia na wasioweza kuwa wenyewe huwa wanapenda kuwa na watu wengine ili kujisahaulisha na kukimbia ndoto zao zinalia ndani yako zikihitaji kufanyiwa kazi.
 132. Robin Sharma anasema, wengi wasioweza kukaa wenyewe na kutulia, hawawezi kuwa na muda wa kutosha wa kujithathmini, hivyo wanakosa kujua upekee wao na hekima ambayo wanaweza kuwa nayo.
 133. Mwandishi anaendelea kwa kusema, watu wasiopenda kujitenga na kukaa wenyewe kwa muda, mara nyingi utawakuta wakiangalia TV, kuchati mitandaoni, jambo ambalo linaharibu uwezo wao mkubwa wa kufikiri, kubuni, na kuwaza makubwa.
 134. Watu hawa wasiopenda upweke, huwa wanaambatana na watu wasiowapenda, wakiishi maisha ya maigizo, maisha yasio na maana.
 135. Maisha anayoyajua mwandishi wa kitabu hiki sio mepesi kama wengi tunavyodhania, maana maisha yatakayokufanya uache alama hapa duniani kwa huduma za viwango vya juu utazotoa hapa duniani yanahitaji kujitoa sana, kwenda hatua za ziada sana, utakuwa na muda mwishi wa kufanya kazi na kuwa mwenyewe ili ujigundue vizuri na ugundue vipaji vyako vyote na ufanye kazi ya ziada.
 136. Japokuwa maisha yatakugharimu hatua za ziada za kila siku kufanya kazi na kujitoa vya kutosha, kuna wakati utachoka na kuumia. Lakini John Lennon alwahi kusema mwisho kila kitu kitakuwa sawa, na ikiwa hakuna kitakachokuwa sawa ujue sio mwisho wa kila kitu.
 137. Tunatakiwa kufahamu wakati tunaweka juhudi kubwa kila siku ili kubiresha maisha yetu na kunoa ujuzi wtu, sio mara zote tutakuwa tunajisikia vizuri katika michakato yote hii.
 138. Mwandishi Robin Sharma anasema kwenye maisha yake amejifunza jambo moja muhimu sana kuwa; uchungu na maumivu tunayoyapata katika ukuaji wetu au kukuza vipaji vyote ni bora mara mia kuliko gharama mbaya za kutisha za majuto.
 139. Wakati mwingine huwa tunajidanganya sana kwa kuona kuwa mambo ya nje, au vitu vya nje vinaweza kujaza utupu uliopo ndani yetu. Jambo ambalo sio kweli kabisa, utupu ulio ndani yetu utajazwa na kufanya wito wetu tuliozaliwa nao, ambao unahusisha kazi na kujitoa sana ili kuutimiliza.
 140. Historia inaonyesha binadamu huwa anachukua hatua za ziada na kufanya kazi kwa viwango vya juu, kuwa na maadili mema ya viwango vya juu sana endapo anajua ana siku chache za kuishi hapa duniani.
 141. Tunaweza kukitazama kifo kama kitu muhimu sana cha kutusukuma kujitoa zaidi, kufanya kazi zaidi, na kuishi maisha yetu yaliyosalia hapa duniani kwa viwango bora vya kiungu.
 142. Kifo tunaweza kukitazama kama ndio kitu kitakachotusukuma na kutukumbusha kufanya vitu vya muhimu na vyenye tija pekee. Hivyo tunaweza kukitazama kifo kwa namna hiyo kama sehemu ya kutufanya tusipoteze muda wetu wa thamani kubwa.
 143. Unapochukua uongozi wa maisha yako ni pamoja na kukubaliana na kila kitu kitakachokuja mbele yako, haijalishi kitu hicho kitakuwa kibaya au kizuri namna gani? Itumie kila fursa inayotokea maishani mwaka kama sehemu muhimu ya kukufanya uwe gwiji, shujaa na mtu hodari hapa duniani.
 144. Kamwe mambo yako ya nje yasikutambulishe, wewe ni zaidi ya hayo machache yanayoonekana, wewe umebeba utukufu mwingi, umebeba ukuu, umebeba shujaa na uwezo mkubwa sana ndani yako, endapo utatoka wote dunia itashangaa sana na kubarikiwa.
 145. Kamwe usipimwe kwa utajiri wako, au mafanikio yako, hayo ni mambo ya kawaida sana na hata waovu wanaweza kuwa na mali na utajiri mkubwa, tengeneza tabia na maadili mema ya viwango vya juu, hayo ndio yatadumu na watu wakupima kwa hayo maana ndio yanayodumu.
 146. Epuka udanganyifu unaoendelea hapa duniani, tengeneza na ishi maisha yako kwa uhalisia wote. Usiyumbishwe na mambo yasiyo halisi yanayoendelea sehemu nyingi duniani.
 147. Tengeneza kinga ya mwili kupiga vita kila aina ya maisha yanayokufanya uishi maisha ya kawaida, maisha yasiyozalisha matokea makubwa. Usikubali kabisa asilani kuishi maisha chini ya uwezo wako mkubwa ulio ndani yako.
 148. Kuwa na uelewa mpana wa dhana ya uongozi, au kiongozi sio kikundi cha watu wachache wanaoendesha mifumo na taasisi kubwa duniani, biashara kubwa za kimataifa, au watu maalumu walioteuliwa au kuzaliwa kuwa viongozi. Uongozi ni kwa ajili ya kila mtu aliye hai hapa duniani.
 149. Uongozi hauhusiani na vyeo vikubwa, majina makubwa, fedha nyingi, mali, utajiri, au watu wenye nguvu nyingi. Uongozi ni kipawa kilichopo ndani ya kila binadamu, na anakazi ya kukidhihirisha kupitia vipawa vyake vya kipekee alivyo navyo.
 150. Una Jukumu kubwa la kuzuia kila aina ya uharamia kwenye maisha yako, ndoto zako, na uwezo wako wa kipekee. Uharamia utakuletea utumwa maishani mwako endapo utapata nafasi.
 151. Uongozi ni kuonyesha njia na kuleta matokeo chanya mahali popote unapoishi. Uongozi ni uwezo wako wa kutoa kazi bora za viwango vya juu kwenye jamii yako.
 152. Kwenye maisha yako, kamwe usifanye kazi kwasababu ya fedha au mapato. Fanya kazi yenye athari chanya kubwa kwa jamii yako. Umwage moyo wako wote, damu yako yote, jasho lako lote, umakini wako wote na akili yako yote kwenye kazi yako, ili uzalishe matokeo yasiyo ya kawaida kwa ubora na upekee wa juu sana yatakayoushangaza ulimwengu.
 153. Katika safari ya kuelekea kilele cha mafanikio yako, teneneza misuli isiyo ya kawaida ya uvumilivu, vumilia na kuwa na utulivu kwenye safari ya kufikia ndoto zako, maana unahitaji sana kuvumilia mengi ili kuzifanyia kazi ndoto zako.
 154. Dhamiria kuwa miongoni mwa binadamu wachache hapa duniani, wenye maadili mema yasiyoyumbishwa na kitu chochote, wenye tabia bora sizizotetereka kwa lolote, kuwa binadamu wa msimamo.
 155. Robin Sharma anasema, ukuu wote, uhodari, ushujaa na ugwiji wote tunaoutaka na kuutamani kwenye maisha yetu hautakuja bila kuwekeza kwenye tabia ya kishujaa ya kuamka mapema kila subuhi na kuanza kufanyia kazi ukuu huu tunaoutaka.
 156. Hutaweza kutimiza ndoto zetu na matamanio yetu ya dhati kama huna muda wa kutosha kuyafanyia kazi, hivyo anapendekeza tuamke mapema sana kabla ya wengine ili tupate muda na utulivu wa kutosha kufanyia kazi malengo na ndoto zetu.
 157. Kama una dhamira ya kupata muda wa kufanyia kazi ndoto zako na matamanio yako ya muda mrefu, basi ingia kwenye clubu ya watu mashughuri wanaoamka mapema zaidi asubuhi, inaweza kuwa ni saa 11 asubuhi ili uanze safari yako.
 158. Tabia ya kuamka mapema asubuhi sana kabla ya dunia haijaamka inatakiwa iwe ni sehemu ya maisha yako yote, iwe ni kama asili kwako, yaani ikifika saa 11 alfajiri uwe ushaamka na kuanza kufanyia kazi malengo yako.
 159. Umeshacheza ligi ya mchangani vya kutosha, umeshacheza ndondo vya kutosha, umeshacheza ligi daraja la kwanza vya kutosha, umeshacheza ligi kuu vya kutosha, sasa unatakiwa kuingia ligi ya mabingwa duniani ucheze na wababe wenzio, magwiji wenzio, na malegendi wenzio ili uzalishe matokeo ya viwango vya kimataifa.
 160. Ili ucheze na mabingwa wenzio, magwiji wenzio wa kimataifa inatakiwa ubadili kabisa mfumo wa maisha yako, upate muda mwingi wa kufanyia kazi uwezo uliolala ndani yako ili utoe kila unachoweza kutoa ndani yako kuzalisha matokeo bora na ya viwango vya hadhi ya kimataifa.
 161. Kila siku unapoamka mapema zaidi unapata nafasi ya kuandika ukurasa mpya kwenye historia ya maisha yako, na utaweza kukazana kila kisku kujisukuma kwenda hatua za ziada, huatakuwa wa kawaida tena.
 162. Usije ukaingia kwenye mtego wa kuwekeza kwenye mambo ya kale ambayo yalishapita, tumia nguvu, utulivu na umakini na muda wako vizuri kuboresha yaliyopo mbele yako, acha yaliyopita yapite maana huwezi kuyabadili kabisa.
 163. Katika dunia inayokazana kukuangusha, simama, katika dunia inayokazano kukutia giza, simama na kimbilia kwenye mwanga wako, kila siku jikagague maisha yako usije ukanaswa na udanganyifu na ulaghai wa ulimwengu ukapoteza maisha yako ya thamani sana.
 164. Tukazane kuwa mabingwa na hodari kwenye upekee wa vipaji vyetu, tuwe watu wenye upendo na wanaonyesha upendo wa dhati usio na masharti.
 165. Onyesha kutoka moyoni mwako heshima, huruma kwa kila binadamu aliyepo kwenye hii dunia ndogo bila kujali asili yake au rangi yake.
 166. Wasaidie wengine kwa kadri ya uwezo wako, usiwe moja ya watu wanaodidimiza na kupanda mbegu za chuki miongoni mwa binadamu wenzako, kuwa binadamu mwenye utu aliyekamilika.
 167. Tumia muda wa maisha yako yaliyobaki hapa duniani kuinua na kuboresha maisha ya wengine. Na kukazana kila siku kuwa binadamu bora mwenye utu wema na maadili yasiyo na mashaka.
 168. Kuwa mmoja wapo wa malaika wa nuru kwa kutembea katikati ya binadamu wengine, fanya yanayooneka kuwa ni magumu na yasiyowezekana kuwa yanayowezekana kama vile tabia njema, kuzalisha kazi bora, kusaidia kutimiza ndoto za wengine na maadili mema.
 169. Kwa kufanya kazi bora ya kuinua utu na kufanya maisha ya binadamu wengine kuwa bora hapa duniani, utaibuka kuwa miongoni mwa roho adhimu zilizowahi kuishi miongoni mwa binadamu hapa duniani.
 170. Jua siku zote haitakuja kutokea dunia ikuletee furaha ya kweli yenye utoshelevu, furaha ya kweli na ya kudumu inatokana na kujua kusudi kuu la kuumbwa kwako na kuliishi na kulitimiza kwa viwango vya vya uwezo wako wote.
 171. Dunia haitajitolea kukupatia furaha ya kudumu, furaha ya kudumu ni kujua hakika kusudi la kubwa hapa duniani na kulitimiza kwa moyo, nafsi, mwili, akili na kila kitu ndani yako.
 172. Jiapize nafsi yako kutumika kikamilifu bila kujibakiza hadi pale utakapoondoka hapa duniani, na jinsi unavyojitoa kufanya kazi kwa bidii ndiivyo furaha yako inavyoongezeka, yafurahie maisha kama yalivyo.
 173. Dunia haijakubebea nuru ili uangaze maisha yako, nuru ipo ndani yako ishi kimamilifu, tumia nuru iliyo ndani yako kuingaza dunia na yafanye maisha yako kuwa nuru inayong’aa sana na uangaze vizazivingi.
 174. Kila mtu hapa duniani amebeba hatima ya maisha yake mikononi mwake. Hivyo una uwezo wote wa kubadili maisha yako upendavyo.
 175. Kuna vitu vimekua adimu sana kupatikana katika zama hizi, vitu hivyo ni kujitoa kikamilifu, nidhamu na uvumilivu, zimekuwa bidhaa adhimu sana kupatikana.
 176. Hakuna kitakachofanya kazi kwa ambao hawafanyi kazi, punguza maneno weka kazi, maneno yawe kidogo, kazi iwe sana. Pia huwezi kushinda kwenye mchezo ambao haujaucheza.
 177. Amka mapema kablya ya jua kuchomoza, fanyia kazi malengo yako makubwa, kwa kufanya hivyo utatimiza mambo mengi ya muhimu ambayo mtu wa kawaida ingemchukua wiki nzima kuyafanya.
 178. Usumbue moyo wako, nafsi yako, akili yako, na mwili wako ili ukujengee tabia zitakazokupeleka kwenye mafanikio ya malengo yako, fanya hivyo bila huruma yoyote, maana kuna dhawabu kubwa.
 179. Amua kuwa na ujasiri mkuu ili usirudi nyuma katika vita ya kupigania ndoto na malengo yako makubwa, safari ya kuelekea kilele cha mafanikio yako inahitaji ujasiri sana.
 180. Katika moja ya hotuba zake za mwisho kabla ya kuuwawa, Dr. Martin Luther alisema, ili uweze kutoa huduma bora kwa binadamu, huitaji degree, huitaji kuwa mjuvi wa lugha, huitaji kujua kuhusu falsafa ya Plato, huitaji kujua sayansi wala nadharia yoyote, unahitaji moyo uliojaa neema ili kutoa huduma bora kwa binadamu.
 181. Mwandishi anasema moja ya kitu kikubwa alichojifunza kwa miaka mingi ni kwamba, kujitoa na kutoa kwa ajili ya wengine ni zawadi unayojipa mwenyewe.
 182. Yainue maisha ya wengine, inua furaha ya watu wengine na wewe utapata zaidi mafanikio na furaha zaidi.
 183. Watu walifanikiwa sana hapa duniani walikuwa wakarimu, tabia ya matajiri na waliofanikiwa wanatabia ya utoji.
 184. Hatutaondoka hapa duniani na vyeo, umaarufu, wala utajiri wetu, tujifunze kuwa wakarimu na kuepuka ubinafsi kwenye maisha yetu.
 185. Kitakachokuwa na maana hapa duniani baada ya kufa ni maisha ya watu uliyoyabariki, ushujaa, wema na ukarimu ulioonnyesha.
 186. Maisha yetu hapa duniani yana ukomo, kamwe usijaribu kuishi maisha yasiyo yako, usihadaiwe na mambo yasiyo halisi ukaacha kuishi uhalisia wa ndoto na malengo yako.
 187. Usikubali mawazo na mitazamo ya watu juu yako ikakuondoa kwenye njia ya malengo yako makubwa, mitazamo ya watu sio muhimu hata kidogo kwako, usikubali ikakuathiri.
 188. Kutokana na usumbufu uliopo duniani, wengi wameshindwa kuwa na umakini kwenye mambo muhimu, hivyo basi endapo utatengeneza tabia ya kuamka mapema zaidi, utaushinda upinzani uliopo baada ya jua kuchomoza.
 189. Hakuna utakachokamilisha kwa kutoa sababu nyingi, achana na sababu tafuta namna ya kukamilisha majukumu yako ya msingi.
 190. Mwanzo ni mgumu siku zote, hakuna kinachoanza kirahisi, hasa unapofikiria kuwekeza katika tabia mpya.
 191. Kama unataka kufikia mafanikio makubwa kama 5% ya waliofanikiwa duniani, basi uwe tayari kufanya yale ambayo 95% ya watu hawayafanyi.
 192. Pale unapotaka kusalimu amri na kukata tamaa, endelea, maana ushindi unawapenda sana watu wasiokata tamaa.
 193. Dunia inaenda kasi, mambo yanabdalika kwa kasi sana, lakini binadamu tumekuwa wagumu sana kubalika, huwa tunachukua muda mwingi kuwaza namna ya kubadilika.
 194. Kuwa mtu wa kutenda na kufanyia kazi maneno yako unayoyasema, fanyia kazi ahadi zako uwe mtu unatabirika kwa kauli na maneno yako, usime moja na kufanya mbili.
 195. Dunia ina watu wazuri sana ambao wanaenda kuzika uwezo wao kipekee ambao unalia ndani yao. Usiwe mmjoa wao wa wanaoenda kuzika ndoto na malengo yako makubwa.
 196. Ingia gharama kidogo ili kuzifanyia ndoto zako, muda mzuri wa kuanza kufanyia kazi malengo yako ni kujifunza kuanza kuamka mapema zaidi ili upate muda usio na usumbufu.
 197. Una akili za kutosha kutambua kuwa huitaji mazingira yawe bora sana, na dunia ikufanye ujisiki vizuri ili uanze kufanyia kazi malengo yako. Fanyia kazi hivyo hivyo hata kama hujawa tayari.
 198. Kamwe usisubirie muda muafaka ili uanze kuishi maisha unayaoyatamani. Unaweza kuanza sasa kwa kuamka mapema na kufanyia kazi malengo yako makubwa.
 199. Hatua ya kwanza utakayoanza kuchukua kuziendea ndoto zako zinatosha kukupa nguvu za ajabu ili zikusukume kupiga hatua nyingine.
 200. Tumia uwzo wako wa kuamua ndani yako, amua kujichagua mwenyewe kama ndiye mtu mkuu na kiongozi wa maisha yako atakayejitoa kwa asilimia 100 kutimiza ndoto zako.
 201. Nafikira sana endapo utaanza kuchukua hatua sasa, mwakani wakati kama huu utakuwa mwenye furaha sana na utajishukuru sana maana ulijichagua kama ndiye mtu sahihi anaweza kukupa furaha kwa kufanya kazi ndoto zako.
 202. Maisha yana tabia ya kuwaadhibu wale wanaosita sita, na kuwapongeza wale wanaochukua hatua wakati wote.
 203. Historia inaonyesha watu maarufu hapa duniani walimili vitu vichache sana, utajiri mkubwa waliwekeza kwenye ukombozi wa watu mfano Mahatma Gandhi alipokufa alibakiwa na miwani, saa, sahani kawa ajili ya chakula na viatu vyake.
 204. Mwandishi wa kiatabu hiki anasema kuwa, watu hawa wakuu walifikia kiwango cha juu sana cha kujitambua na waliona mafanikio ya kweli na yanayodumu sio kushikamana na vitu vya muda kama fedha, magari, nyumba nk. Waliwekeza vya kutosha sana kwenye tabia na maadili mema yenye nguvu sana ambayo yaliwafanya wavumilie na watosheke kabisa maishani.
 205. Epuka sana anasa, maana ukiendekeza anasa zitakutoa kwenye utulivu na utashindwa kujizuia na kujenga tabia ya kiasi na utoshelevu.
 206. Unapoonyesha kazi ya vingo vya juu sana, ni sawa na kuonyesha thamani yako na heshima yako mweneywe.
 207. Kweye utalaamu wako pata ujuzi wa juu sana na uelewe kwa undani kuhusu unachokifanya, usifanya fanye tu ilimradi.
 208. Jitoe kweli kuwa binadamu asiye wa kawaida, ili uweze kufikia ndoto na dhahabu ilifichwa ndani yako, acha kuishi kuizoeza kwenye roho za uoga, umeumbiwa ujasiri na binadamu asiye wa kawaida.
 209. Kuwa mtu wa viwango, kuwa mtu mkali kwako mwenyewe, kuwa mtu mgumu, jivike ujasiri wa kwenda hatua za mbali, piga hatua za hatari, tengeneza maisha yako kwa viwango vya daraja la juu sana la maadili na utendaji wa mambo yako.
 210. Tumia muda unaotaka hataka kama ni miaka mingi kukalimisha kazi bora itakayodumu, kuliko kuruka ruka na vitu vidogo vidogo visivyo na thamani.
 211. Katika juhudi zako za kuzalisha kazi bora, mara nyingi utajikuta ukiwa mwenyewe, utawaliwa na upweke, mara nyingi utabakia peke yako kwenye uwanja wa kuboaresha na kujisukuma kwenda hatua za ziada.
 212. Katika mazingira haya ya upweke kamwe usikate tamaa, jing’ang’anize ubakie kwenye kazi yako hata kama itakugharimu siku nyingine nyingi za ziada ili uzalishe kazi bora zaidi.
 213. Mbingu zinapenda ung’ang’anizi, maana hiyo ndio inapima ni njaa na kiu kiasi gani unayo ya kutaka kufanya unachokifanya. Hivyo usiondoke kwenye uwanja wa vita hata kama umebakia mwenyewe, pambana hadi mwisho wa nguvu zako zote.
 214. Upinzani ni mkubwa sana kwenye njia ya mafanikio, angalia maisha yako ilivyo kazi na upinzani mkubwa kuamka mapema asubuhi kwa ajili ya kupambania ndoto zako. Ndio maana mbingu, na malaika watakuwa upande wako ili wakubariki endapo utakataa kukata tamaa.
 215. Amka mapema zaida ya wote, muda huu wa asubuhi sana utumie kujenga na kusimamisha himaya yako yenye nguvu, tengeneza ufalme wako kwa kuwekeza kazi za viwango bora kabisa.
 216. Jinsi unavyoongeza ung’ang’anizi kwenye kazi zako ndivyo hofu, mashaka, na wasiwasi unavyokachia na kuondoka kwenye maisha yako.
 217. Ipokee kila siku mpya kwa furaha, na dhamiria kuiishi kwa ukamilifu wote, usipoteze hata sekunde yako kwenye mambo yasiyo na tija.
 218. Namna nzuri ya kukabiliana na ulimwengu usio huru ni kuwa huru kweli kweli kiasi ambacho uwepo wako hapa duniani idhaniwe kama kitendo cha uasi.
 219. Kila wakati unapopvumilia kwenye safari yako ya mafanikio unatengeneza bahati nyingi, kumbuka bahati hazikujii tu, bahati zinatengenezwa na hatua unazochukua kila siku.
 220. Mfalme Alexanda mkuu aliwahi kusema, haogopi kundi la simba linaloongozwa na kondoo, anaogopa zaidi kundi la kundoo linaloongozwa na simba.
 221. Tunataikiwa kuutazama ulimwengu kwa mtazamo mpya kabisa na sio kwa miwani ya malezi yetu ya kale ambayo yanatulaimisha kuwa na ukomo katika kufikiri na kutenda.
 222. Sisi binadamu ni viumbe wa kiroho, tumeletwa duniani na kupewa miili tuliyonayo ili tuuishi ubinadamu. Hivyo basi asili yetu ni roho na sio mwili, wekeza kwenye ukuaji wa roho yako maana ndio maisha yako.
 223. Hakuna atakayekuja kukuamini na kuamini katika uwezo wako, ni wewe mwenyewe unatakiwa kuwa wa kwnza kuchukua hatua za awali kabisa na kuanza kujiamini na kuamini katika uwezo na vipawa vilivyo ndani yako.
 224. Watu wenye malengo makubwa, wanaofanyia kazi ndoto zao, hawana muda wa kupatikana kila wakati, sio mara zote utawapata kama unavyowataka, hawapatikani kirahisi, muda mwingi wamejikita katika kufanyia kazi ndoto zao.
 225. Kila siku mpya inapoanza, anza kwa kujichagua wewe mwenyewe kwanza, anza kujiwaza wewe kwanza kama ndiye mtu wa pekee mwenye hatima ya kuyafanya maisha yako kuwa bora zaidi.
 226. Inapofika swala la hatima yako, jichague mwenyewe usitoe nafasi ya mtu mwingine kuwa na ufunguo wa maisha yako, shika hatamu ya kuyaishi maisha yako kwa viwango vya juu.
 227. Kumbuka siku zote wewe ndio mwamuzi wa mwisho kwenye maisha yako, ni wewe ndio utaamua uamue kuwa jasiri, au uamue kuwa muoga, uamue kuishi ndoto zako au uendelee kuifuatisha dunia hii upotee.
 228. Wekeza masaa mengi ya kutosha kujiboresha, watalaamu wanasema ili ufikie ubobezi na kuwa gwiji kwenye fani yoyote, unatakiwa kuwekeza muda wa masaa yasiyopungua 10,000.
 229. Jipe zawadi kila siku, kwa kujipa muda wenye utulivu, muda ambao akili, mwili na dunia yote imelala, jipe zawadi ya masaa yasiyo na usumbufu ili ufanyie kazi malengo yako makubwa kwenye.
 230. Boresha sana himaya zako za ndani, ambazo ni roho, nafsi akili na hisia zako. Hizi zikiimarika na kuwa na nguvu utaweza kushinda majaribu na mambo mengi yanayowashinda wengi hapa duniani.
 231. Uimara wa utu wako wa ndani ndio utafanya uimara katika utu wako wa nje, hivyo usikimbizane na ulimwengu wa nje, wekeza kwenye ulimwengu wako wa roho. Visivyoonekana kwa macho ni halisi zaidi ya vinavyoonekana kwa macho.
 232. Mwanamapinduzi mashughuri na baba wa taifa la India Mahatma Gandhi aliwahi kusema, shetani tunayetakiwa kukabiliana naye ni yule aliye ndani ya mioyo yetu. Kwenye mioyo yetu ndio upinzani mkali hutokea, na ndio sehemu ambayo vita ya kweli inatakiwa kupiganwa.
 233. Ukuu na uhodari ni mchezo wa kiroho zaidi, ni mchezo unachezwa ndani yako zaidi kuliko nje ya mwili wako. Greatness is an inside game.
 234. Mpaka sasa unatakiwa kujua una himaya kuu nne unatakiwa kuzifanyia kazi ili ziimarike sana ambazo ni, akili yako, moyo au roho yako, afya yako, akili na nafsi yako yani Mindset, Heartset, Healthset and Soulset.
 235. Yapende maisha na panga kuishi kwa muda mrefu hapa duniani, hivyo wekeza kwenye mfumo wako wa akili, nafsi, afya na moyo wako.
 236. Jinsi na nmna tunavyoitazama dunia kwa mitazamo yetu ndivyo tunavyoenenda. Tabia ni muhimu maana zinaamua kwa kiasi kikubwa hatima ya maisha yetu.
 237. Mwandishi wa kiatabu hiki amependekeza moja ya kanuni anazotumia kuboresha kila sehumu muhimu ya maisha yake, kanuni hii inaigawanya dakika 60 kwa 20/20/20.
 238. Yani unapoamka asubuhi wekeza dakika 20 kwenye afya yako kwa kufanya mazoezi, mazoezi yanatakiwa yawe ya kukutoa jasho, fanya hivyo kwa muda huo ili kuboresha afya yako na kutoa kemikali chafu ndani ya mwili wako.
 239. Wekeza dakika 20 kuboresha roho yako kwa kusali na kufanya tahajudi, ni muhimu sana ukawa na muda wa kufanya tafakuri ya kina kuhusu maisha yako yote, ya kiroho na kimwili, omba msaada kutoka juu ili Mungu akusaidie, malaika wawe upande wako na mbingu zikutetee.
 240. Dakika 20 za mwisho boresha akili na mfumo wako wa kufikiri kwa kusoma na kujifunza mambo mapya kila siku. Weka mpango wako wa kujifunza uwe mzuri na wakuvutia mara zote ili kila siku ujifunze kitu kipya katika muda huu wa utulivu.
 241. Kumbuka, uwekezaji huu utafanyika kwa ufanisi wa viwango vya juu endapo utafanyika mapema sana asubuhi, inapendekezwa iwe saa 11 alfajiri maana ndio muda amboa una utulivu.
 242. Fikiria mwenyewe endapo kila siku utaamka mapema sana asubuhi kabla ya mtu mwingine yoyote na ukaamua kuweka nguvu zako zote kwenye kubioresha maeneo hayo manne muhimu kwenye maisha yako, hakika utakuwa binadamu pekee sana.
 243. Epuka kuhairisha mambo muhimu kwenye maisha yako, ikatae na kaa mbali na roho ya kugairisha mambo muhimu kwenye maisha yako. kama ni mambo ya muhimu kwenye maisha yako, yafanye tu hata kama unajisikia hovyo kiasi gani.
 244. Zikabili hofu zako, ukabili udhaifu wako, jisukume kuchukua hatua za ziada katika nyakati mbaya na ngumu, maana ndio utaona uhalisia wa nguvu kubwa iliyo nadani yako.
 245. Kila unapoona unataka kufikia ukomo na kushindwa kuendelea mbele, jidai nguvu na ubora ambao umejifucha ndani yako, jidai ujasiri na ubunifu wa kipekee uliolala ndani yako utoke ukusaidie.
 246. Nguvu zako za kweli utaziona katika nyakati ngumu, uwezo wako halisi utadhihirika katika nyakati za hatari na ngumu, usiogope maana ndio unakaribia kujipata.
 247. Jiimarishe uwe mtu imara asiyezuilika kwa changamoto zitakazotokea kwenye maisha yako. Dhamiria kwenda mbele hata kama unaona kila kitu hakiendi tena mbele.
 248. Nguvu unazoziona kwa wengine, ujasiri unaouona kwa wengine, matumaini, nidhamu, imani na ustahimilivu unaouona kwa wengine jua kuwa hawakuzaliwa nao. Walifika hatua kwenye maisha yao wakaamua kuwa wajasiri, wavumilivu na wasioogopa, walivitengeneza kwa gharama kubwa.
 249. Onyesha mapenzi ya dhati kwako mwenyewe, ili uchukue hatua zote zinazotakiwa ili uyafanye maisha yako kuwa bora. Nguvu za kukubadilisha na kukuletea mafanikio zote zipo ndani yako.
 250. Ongeza udhibiti na nidhamu kali kwenye maisha yako, hii itakusaidia kufanya yote uliyojiahidi kuwa utafanya ili kuboresha maisha yako.
 251. Kama yapo mambo ya muhimu sana kwenye maisha yako yafanye hata kama ni magumu kiasi gani, utaongeza ukuu na ujasiri kwa kufanya unayoyaona magumu sana kwenye maisha yako.
 252. Hutakuwa mtu mkuu na mwenye ushawishi duniani kwa kuishi maisha laini na mapesi, ugumu unakukuza na kukufanya uonekane na wengi, hivyo kufanya maisha yako kuwa na mvuto.
 253. Hutakuwa na akili unayoitaka, utapata akili ambayo umeifanyia kazi kuipata. Vitu unavyotamani havitakuja tukwako, unahitaji kuvifanyia kazi ili uvipate ulivyovifanyia kazi.
 254. Tumia akili yako kwa akili sana, jinsi unavyoitumia ndivyo inavyokuletea majibu ya maisha yako, na itaongezeka kupanuka na kuwa na upeo mpana wa kuelewa mambo mengi.
 255. Unapofika wakati wa kuamka mapema amka mapema iwezekanavyo usianze tena kufikiria fikiria maana ukitoa hiyo nafasi utaanza kutengeneza sababu nyingi na hizo sababu zitakushawishi uendelee kulala.
 256. Jiamulie kujitoa kuwa mwanachama wa kudumu wa watu wachache wanaoamka mapema zaidi, yaani saa 11 alfajiri ili kuanza kufanyia kazi malengo yao.
 257. Usifanya maamuzi wakati umechoka au wakati nguvu yako ya maamuzi ipo chini, uzoefu unaonyesha kuwa maamuzi mabaya hufanyika wakati nguvu yako ya kufanya maamuzi ipo chini. Usiruhusu nguvu yako ya maamuzi ichoke.
 258. Kama hakina ugumu wowote wakati unakianza ujue kinaweza kisiwe na mabadiliko ya kudumu.
 259. Nadhani unafahamu kwanini roketi zikitaka kuruka kwenda kwenye angala la juu sana huwa zinatumia nishati kubwa sana ya mafuta, ni kwasababu hapa mwanzoni kuna ukinzani mkubwa sana, hivyo nguvu ya kuanza huwa kubwa zaidi mwanzoni mwa jambo.
 260. Unahitaji kutoka kwenye uraibu mbaya, tabia mbaya na tamaduni au imani potofu zilizoishi na kukutawala kwa miaka mingi, na kutoka kwenye hali hizo inahitajika nguvu kubwa sana, maana upinzani na maumivu yake ni makubwa endapo unataka kuachana na tabia za kale.
 261. Mwandishi anatoa ushauri kwamba kwa vyovyote vile, kwa gharama yoyote ile endelea kupambana na kung’ang’ania kusalia kwenye njia za ndoto zako, maana kinachoonekana kuwa kigumu na upinzani mwingi mara nyingu huwa na thamani kubwa.
 262. Kunapokuwa na machafuko, uharibifu na mambo kuenda bila utaratibu hapo ndipo utaratibu mpya, mbinu mpya na mipango mipya ya kuishi au kujenga kitu huandaliwa.
 263. Mwandishi anasema atafurahi endapo mbinu zote ulizojifunza kwenye kitabu hiki utawashirikisha na watu wengine wazijue ili maisha yao yawe bora.
 264. Watu wanatakiwa wabadili maisha yao yawe bora sio kwasababu ya vyeo vyetu, umaarufu wetu au utajiri wetu bali maadili bora tutayayoyaishi hapa duniani.
 265. Jinsi unavyowafundisha wengine ndio unajua mambo mengi zaidi, walimu wanajua zaidi kwa kuwa wanawafundisha wengine wajue.
 266. Usiwe mchoyo kuwafundisha wengine maarifa haya, mnunulie mtu kitabu hiki, mtumie kitabu hiki, mwambie umuhimu wa kusoma kitabu hiki, kama unaweza mtumie uchambuzi huu pia.
 267. Tumia muda wa asubuhi sana kufanya mambo magumu na muhimu kwenye maisha yako, wanasayansi wanasema kipindi hiki cha asubuhi sana kiwango chako cha homoni aina ya cortisol kinakuwa juu ili kukufanya ili kukufanya uongeze umakini na kufanya kazi bora.
 268. Sayansi inasema wakati wa asubuhi sana unapofanya kazi, hata umengenyaji na kusharabiwa kwa chakula hufanyika vizuri zaidi wakati huu.
 269. Unapoamka mapema sana asubuhi saa 11 alfajiri au kabla unaongeza utimamu na uimara wa kinga za mwili wako, hivyo unaimarisha mwili wako na kuufanya kuonekana wenye afya wakati wote.
 270. Katika kupambania ndoto zako na ili ufikie kilele cha mafanikio makubwa unatakiwa kuishi muda mrefu. Maana yake usife mapema. Fanya unaloweza kwa uwezo wako wote kulinda afya yako maana bila afya njema hutaweza kufikia ubora tunaousema.
 271. Yachukua mafunzo haya yote tunayojifunza hapa na uyafanyie kazi, yafanye yawe sehemu muhimu ya maisha yako, yafanye yawe yako ili maisha yako yawe bora.
 272. Maanisha kabisa kwa yote unayoyataka kwenye maisha yako, usifanya mambo ilimradi, dhamiria kufanya jambo lako kwa ufanisi mkubwa.
 273. Inua tanga na safiri mbali sana na bandari salama, ukamate upepo unaosafiri kwenda mbali nenda nao, nenda mbali na mipaka na ukomo uliozoeleka, upeleke ubunifu na kipaji chako kwenye kingo za misho kabisa za uwezo wako, nenda mbali gundua vitu vipya.
 274. Jihadhari nafsi yako usije ukawa mwanachama wa wanaopeleka utajiri, vipaji, uwezo wa kipekee makaburini. Nenda kaburini ukiwa umeisha, ukiwa umeshatoa kila kilichowekwa ndani yako, nenda kaburini na kubali kufa ukiwa umeshatumika na kumalizika kabisa, nenda ukiwa mtupu kabisa.
 275. Kila siku mpya inayokuja kwenye maisha yako, andika mipango utakayoifanyia kazi na andika mambo ambayo utayakamilisha kwa siku hiyo, fanya hivyo kila siku ya maisha yako.
 276. Mwandishi ameshauri tufanye tahajudi au meditation mara kwa mara ili kupata nguvu mpya na kujiondoa kwenye msongo wa mawazo. Tahajudi ina faida nyingi sana za kiroho na kimwili, kama kuongeza umakini wako katika kufanya mambo.
 277. Jitahidi kujitenga na kuwa peke yako sehemu yenye utulivu ili ufanye tahajudi, jiondoe sehemu zenye usumbufu, jipe muda mwingi wa kukaa mwenyewe ili ujigundue zaidi.
 278. Una kila kitu ndani yako kama kinga dhidi ya maradhi, umasikini, na mikosi, hata hivyo mawazo mengi huwa yanapita kwenye kichwa chako, chagua moja ulitafakari kwa kina.
 279. Heshimu sana muda wako wa kulala, muda wako wa kulala unapofika usianze tena kwenda kitandani na smu au computa yako, lala muda ambao umepanga kulala.
 280. Uwe na muda bora wa kulala, usijikute unalala zaidi ya masaa nane, au unalala chini sana ya masaa hayo, inaweza kukuletea shida kwenye afya yako, masaa 5 hadi 8 yanatosha kulala.
 281. Robin Sharma amesisitiza sana tuepuke ulevi wa mitandao ya kijamii, kuangali Tv, na kusikiliza habari hasi, anasema haoni faida iliyopo kwa wewe kuzingatia kusikiliza habari.
 282. Mitandao ya kijamii ni kama uharamia kwenye maisha yako, maana inakutoa kwenye umakini, inakutoa kwenye mapenzi ya kufanya malengo yako, inakuongezea msongo wa mawazo, inakupunguzia nguvu zako za kufanya kazi. Nk.
 283. Jifunze mwenyewe kutoruhusu akili na mwili wako kuruka ruka kama nyani kwenye miti, itulize akili yako. thibiti kabisa hali zote za kutaka kujitoroka unapofanya kazi.
 284. Muda wa kazi fanya kazi, sio tu umefika ofisini au eneo la kazi kitu cha kwanza unaanza kuangalia simu na kuingia kwenye mitandao ya kijamii. Hii ni usumbufu na inakuondolea morali ya kufanya kazi yako kwa viwango bora.
 285. Ili kuboresha umakini wako unaweza kujipangia kuwa utafanya kazi kwa umakini wa hali ya juu kwa dakika 60, baada ya hapo unaweza kupumzika dakika 10, halafu unarudia tena kufanya kazi kwa umakini kwa dakika nyingine 60.
 286. Jambo jingine muhimu la kuimarisha umakini na afya yako ni kufanya matembezi, tembea bila kifaa chochote cha kidigitali kama simu, tembea kwa dakika chache maeneo ya asili yenye uoto wa asili ili uhuishe nguvu zako.
 287. Mwandishi ameshauri pia tuwe na utaratibu wa kufanya masaji, ili kuhuisha nguvu na tishu za mwili wako, angalau mara mbili kwa wiki. Utafiti unaonyesha wanaoweza kufanya hivyo wanaongeze urefu wa maisha yao.
 288. Kuwa karibu na timu ya watu wanajitoa kufikia mafanikio makubwa, watu ambao watakufanya uchukue hatua na ujisukume kufikia kilele cha ndoto na mafanikio yako.
 289. Kuwa moja ya watu wachache waliodhamiria kuishi maisha yao kwa viwango vya juu sana, kuwa mwanafunzi wa kweli kwa kujifunza kila siku za maisha yako.
 290. Jikubali kweli kweli, kuwa mfano wa maisha unayoyataka, ujasiri unaoutaka, ushujaa, uhodari na dhamiria kufikia viwango vya juu vya kimataifa katika utendaji wako.
 291. Jidai kazi bora kutoka ndani yako, kisumbue sana kipaji na uwezo wako uliolala ndani yako uamke, nenda hatua nyingi za ziada na kipaji chako.
 292. Wewe ni mtu hodari, shujaa, gwiji, una ukuu na nguvu ndani yako, hunatakiwi kuzalisha vinyonge na dhaifu, unatakiwa kuzalisha vitu bora na kuonyesha ujasiri wenye utiisho mkuu.
 293. Siku zote tumia lugha ya matumaini, upendo na sema sentensi zenye nguvu na ongea maneno yalijaa uhuru na nuru kama mtu aliye huru.
 294. Jizoeze akili yako kufikiri na kutafakari mawazo bora na mazuri yatakayokuletea mafanikio na furaha maisha mwako.
 295. Kuwa mtu wa shukrani kwa yoyote yaliyotokea na unayoyapata kwenye maisha yako.
 296. Kuwa mtu wa kubariki kwa yote yaliyopo kwenye maisha yako, ibariki fedha kwa kuwa inakulipia bili mbali mbali za maisha yako, wabariki wakulima maana wanalima na kuzalisha chakula tunachokitumia kila siku, wabariki boda boda maana wanarahisisha maisha yetu na kukufikisha sehemu kwa wakati na kwa gharama nafuu.
 297. Wabariki waimbaji maana wanatumia muda mwingi kutunga nyimbo nzuri ambazo zinatupa hamasa, kutuburudisha na kututia moyo tusonge mbele.
 298. Wabariki waandishi wa vitabu maana wameingia gharama kubwa sana kuandaa kazi bora ambazo zinatusaidia kuboresha maisha yetu.
 299. Bariki kila mtu kwenye maisha yako, bariki wala usilaani, maana kila mtu kwa ukubwa na udogo wake wamechangia sana kufanya maisha yako yaende na yawe bora.
 300. Wekeza kwenye kununua vitabu bora kabisa kwa ajili ya kuboresha maisha yako.
 301. Kula chakula bora kabisa, hata kama ndio una uwezo wa kununua hicho tu, angalia mtaani kwako na nenda kale chakula bora kwenye moja ya mighawa bora sana hapo karibu.
 302. Usiahirishe chochote chenye thamani maishani mwako, ukuu uhodari hautakujia kama ajali, usizuie ukuu wako kwa mambo ya muda yanayopita.
 303. Ishi na kuwa mfano bora kabisa wa binadamu kuwahi kuishi hapa duniani, ishi kwa maadaili na tabia bora kabisa kiasi kwamba vizazi vijavyo vione kabisa mtu wa aina yako hawakupaswa kuishi pamoja na wanadamu wengine kwa jinsi ulivyoishi kwa ubora na kuyafanya maisha ya wengi kuwa bora sana.
 304. This is your time. And now is your day: to make your leap, in your original way, into the rare-air of the finest leaders who have ever lived. And to enter the universe of the true masters, eminent virtuosos and authentic heroes who have been responsible for all progress of civilization.

Kitabu hiki kina mambo mengi sana ya muhimu, haya niliyoandika hapa ni machache. Nashauri sana kila mtu akisome kitabu hiki, ni kitabu bora sana kwenye zama hizi, kitakusaidia sana sana.
@Hillary Mrosso, 25 Jul, 2022.


2 responses to “Uchambuzi Wa Kitabu Cha The 5Am Club: (Mambo 304 niliyojifunza kutoka kwenye hiki kitabu)”

 1. Napenda sana vitabu kwa sababu kusoma vitabu kunaongeza maarifa na uwezo kufanya kazi kwa Weledi mkubwa sana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X