Tuna facebook, twitter na mitandao mingine ya kijamii. Kila mtu anakazana sana kuhakikisha kwamba kwenye hii mitandao anakuwa na wafuasi wengi
Hata hivyo, ukweli ni kwamba hii mitandao huimiliki wewe. Muda wowote ule wanaomiliki hii mitandao wanaweza kufanya chochote na watu wazuri wanaofuatilia kazi zako wakashindwa kuziona tena. Hii ni mbaya sana.
Instagram wanaweza kukufungia leo na watu wote ambao wanafuatilia kazi zako huku wakashindwa kuona vitu vizuri wanavyopata kutoka kwako.
Facebook na majukwaa mengine yote yanaweza kukufungia na watu wakakosa vitu vizuri kutoka kwako. Unakumbuka kilichomtokea Trump?
Ila kuna vitu viwili ambavyo kwenye zama za leo ni uhakika hakuna mtu anaweza kukuzuia ukiwa navyo.
Kwanza ni email list
Hawa ni watu wanaokuwa wamejiunga na mfumo wako wa kupokea mafunzo kwa njia ya baruapepe. Unaweza kupoteza wafuasi wako wa facebook, instagram au sehemu nyingine lakini hawa huwezi kuwapoteza. Hawa watu ni wako na umiliki wa haya mawasiliano unakuwa nayo wewe wala siyo Zuckerberg au mtu mwingiine.
Halafu isitoshe barua pepe ni kitu binafsi. Unapokuwa unawasiliana mtu kwa njia ya barua pepe unakuwa unawasiliana naye yeye kama yeye. Hivyo, inakuwa rahisi kujenga uhusiano wa karibu na watu wako. Kwa sababu wanaweza kufunguka kwako chochote na wewe unaweza kufunguka kwao chochote. Kwa hiyo mnajenga uhusiano wa kudumu.
Baruapepe za watu unakuwa nazo wewe, siyo kwamba wanakuwa nazo facebook au instagaram ambao wanaweza kusepa na followers wako muda wowote.
Kwa hiyo rafiki yangu, japo unajenga wafuasi kwenye hii mitandao. Ebu fikiria pia kuhusu namna unavyoweza kujenga email list yako. Mfumo wa kupokea makala kwa njia ya barua pepe ambapo watu wako watakuwa wanapokea mafunzo kwa njia ya baruapepe.
Unaweza kuanza kujenga huu mfumo kupitia jukwaa kama mailchimp, mailmunch, mailerlite na nyinginezo nyingi zilizopo. Chagua moja na komaa hiyo kwa kuanzia.
Pili Ni Tovuti Au Blogu
Hki ni kitu kingine ambacho wewe mwenyewe una umiliki nacho na wala siyo facebook wala twitter. Hawana mamlaka yeyote huku.
Ebu chukulia mfano wa kawaida tu. ukiandika status ya whatsap inapotea baada ya saa 24.
Leo hii kuna vitu ambavyo uliandika kwenye instagrama yako mwaka 2020 ila unavitafuta na huwezi kuvipata. Na isitoshe hakuna namna ambavyo unaweza kumwambia mtu arejee masomo yako ya nyuma ii kujifunza na kunufaika zaidi. Ila mimi kwenye blogu hapa naweza.
Mfano, soma hili somo nililoandika siku za nyuma kwa KUBONYEZA HAPA
Unaona ee! Hiki kitu kwenye blogu nakifanya ndani ya sekunde tu na kinaisha, ila ukitaka kufanya hivi facebook, inabidi utenge masaa ya kutafuta kile ulichoandika siku za nyuma.
Ukibahatika kukiona ndio unaweza kumwonesha mtu akiangalie. Rafiki yangu naomba unisikilize kwenye hili
Kuwepo facebook, kuwepo instagram, ila kitu kimoja tu ni kwamba usiache kuwa na blogu yako pamoja na email list maana hivi ni vitu viwili ambavyo unaweza kumiliki mtandaoni.
Hii ni maalumu kwa ajili yako wewe unayefanya biashara kwa njia ya mtandao na unataka kujenga mtandao wa watu utakaodumu nao bila kuwapoteza. Na ngoja nikwmabie kitu. Hivi
Kila la kheri
Umekuwa name Godius Rweyongeza (Songambele)
0755848391
Morogoro-Tz