Moja ya sababu ambazo watu huwa wanatoa linapokuja suala zima la kuweka akiba ni kuwa hawawezi kuweka akiba kwa sababu wana vitu vingi vya kufanya na fedha. Utakuta mtu anakwambia kwamba nina kodi, ya nyumba na bili nyinginezo ambazo ninapaswa kulipa na hata fedha hainitoshi.
Kitu kimoja cha muhimu sana na cha kushangaza ni kuwa watu hawa watu huwa wanapambana kuhakikisha kwamba wanalipa hizi bili ila huwa wanajisahau kwenye suala zima la kuweka akiba na kuwekeza.
Bili zao hata zikiongezeka huwa wanahakikisha kuwa wanatafuta namna ya kuzilipa ila huwa hawatafuti namna ya kuhakikisha kuwa wanaweka akiba.
Sasa leo ninachotaka kukwambia ni kuwa fanya uwekaji wa akiba na uwekezaji kama ulipaji wa bili. Yaani, kama ambavyo unalipa bili zote bila kujali bili hizo zimeongezeka au zimebaki palepale. Hivyo hivyo, unapaswa kuweka kipaumbele kwenye kuweka akiba na kuwekeza. Kamwe usikubali kuishi maisha bila ya kuweka akiba wala kuwekeza. Ni muhimu sana kwako kuweka akiba. Ni muhimu mno kiasi kwamba haupaswi kupuuzia kitu kama hiki hapa rafiki yangu.
Kuweka akiba kwako kuwe kipaumbele kama vile unalipa kodi ya nyumba. Kuweka akiba kwako kuwe kipaumbele kama vile unanunua luku ya umeme.
Kuna baadhi ya familia umeme ukikitatika, utakuta kwamba kwenye familia wanahaha, kama baba au mama ambaye anapaswa kununua umeme hayupo wakati umeme unakatika, basi wanafamilia wote watatafuta namna ya kuhakikisha kwamba wanawasiliana naye hata kwa kumpigia simu, hata kama wanaomba simu kwa jirani.
Sasa nataka na wewe ufanye uwekaji wa akiba kuwa kipaumbele. Mwambie mpaka mwenza wako awe anakukumbusha kuweka akiba kama kitu cha kwanza. Asikukumbushe tu kulipa kodi ya nyumba kwa sababu mkifukuzwa kwenye nyumb mtaaibika, asikukumbushe tu kulipia umeme kwa sababu mkikaa bila umeme hawezi kuangalia tamthiliya, akukumbushe pia kuweka akiba na kuwekeza kwa sababu usipofanya hiki kitu, itakuwa aibu kwako miaka mingi ijayo mbeleni. Fanya uwekaji wa akiba kuwa kipaumbele kwenye maisha yako tena kiwe kipaumbele kikubwa sana. Usipuuzie uwekaji wa akiba na uwekezaji rafiki yangu.
Kila la kheri, hilo ndilo jiwe langu kwa watu ambao hawataki kuweka kuweka akiba siku ya leo.
Kujifunza zaidi nashauri usome kitabu changu cha MAAJABU YA KUWEKA AKIBA.
Hiki kitabu kitakufungua vitu vingi sana kuhusu uwekaji wa akiba na namna ambavyo unaweza kuwa wenye manufaa kwenye maisha yako. Halafu kitabu chenyewe ni elfu tano tu. Ndio, elfu tano ya kitanzania. Namba ya malipo ni 0755848391 na jina ni GODIUS RWEYONGEZA.
Karibu sana
Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli
Godius Rweyongeza (Songambele)
0755848391
Morogoro-Tz
One response to “Jiwe la uzito wa tani moja kwa wale ambao hawataki kuweka akiba”
[…] Soma zaidi: Jiwe la uzito wa tani moja kwa wale ambao hawataki kuweka akiba […]