Kama una mpango wa kufunga Ndoa 2024, hakikisha unasoma hapa


Kama unamjuaa anayefunga ndoa mwaka huu mtumie ujumbe huu

Una mpango wa kufunga ndoa 2024 rafiki yangu. 

Kwenye jamii zetu kumekuwa na utaratibu ambao unajirudia kila mwaka. Kila mwaka kuna maelfu ya watu wanaofunga ndoa na utaratibu ambao huwa unafanyika huwa ni uleule kila mwaka..

Mtu akitaka kufunga ndoa, anaandaa harusi kubwa, anaalika watu mbalimbali wamchangie, ili kuonesha ubabe anaweka vitu vya gharama kubwa.

Hela inapokuwa haitoshi anakopa na sherehe inafanyika.

Wengine wanafanya harusi wakiwa na matarajio kuwa ile fedha watakayopata siku ya harusi ndiyo iwasaidie kulipa mkopo au kuanzia maisha baada ya harusi.

sasa sipo hapa kusema kwamba usifanye harusi. Hilo utafanya au hutafanya kulingana na wewe mwenyewe au kulingana na ukubwa wa mfuko wako. lakini chonde chonde, usifanye harusi kwa kukopa hela. Usianze maisha ya mahusiano ukiwa na deni. Hii siyo sehemu nzuri ya kuanzia kimaisha.

Usikope fedha kwa ajili ya kufunga ndoa ukitegemea kuwa zawadi utakazopata zitaweza kurejesha ule mkopo. Mara nyingi huwa haiwi hivyo. Kumbuka sijasema mara zote, ila mara nyingi.

Najua kabla ya kufunga ndoa huwa kuna mafunzo ambayo huwa yanatolewa. Lakini kuna mafunzo ambayo huwa yanasahaulika. na mafunzo haya ni ya uwekezaji.

Kabla hujafunga ndoa mwaka huu hakikisha kwamba unajifunza uwekezaji. Siyo wewe tu, hata huyo mwenza wako, hakikisha anajifunza uwekezaji. Na hasa uwekezaji kwenye hisa, hatifungani na vipande. Nakwambia, utanishukuru kwa hili maisha yako yote. 

Hii ni elimu ambayo haitolewi unapokuwa unataka kufunga ndoa ila ni elimu muhimu ambayo ukiipata itakuwa yenye manufaa kwako, kwa familia yako na kwa kizazi chako, hata miaka buku ijayo. hivyo basi, nikushauri kitu kimoja, jifunze uwekezaji kwenye hisa, hatifungani na vipande wewe na mwenzako kabla ya kuingia kweye ndoa mwaka huu.

Na sehemu nzuri ya kuanzia ni kusoma kitabu cha MAAJABU YA KUWEKEZA kwenye hisa, hatifungani na vipande. Kitabu hiki unaweza kukipata kwa kuwasiliana na 0684408755 sasa. 

Soma zaidi: Jiwe la uzito wa tani moja kwa wale ambao hawataki kuweka akiba


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X