Siku siyo nyingi nilipokea ujumbe kutoka kwa mmoja wa watu wanaofuatilia kazi zangu mtandaoni. Kitu kikubwa sana ambacho aliweza kuniambia ni kuwa anapata changamoto hasa anapoweka malengo, anashangaa siku zinaenda ila hayo malengo yake hayatimiii.
Sasa siku ya leo kwa namna ya kipekee ningependa kumjibu huyu rafiki pamoja na watu wengine wengi ambao wanawakuwa na shida kama hii hapa ili sote kwa pamoja tukitoka hapa twenda kufanyia kazi malengo yetu kwa manufaa na kwa namna ambayo ni bora zaidi.
Kabla sijaingia ndani zaidi, ningependa sana kukwambia kuwa karibia kila mwanzoni mwa mwaka watu wengi huwa wanaweka malengo makubwa ambayo watayafanyia kazi ndani ya mwaka huo, ila cha kushangaza ni kuwa mpaka kufikia tarehe 19 januari watu wengi huwa wamesahau malengo yao, na wachahe ambao huwa wanaendekea kukumbuka malengo ndio huweza kuendelea nayo mbele kidogo huku wachache zaidi wakiwa ndio wanafikia malengo yao. Sasa swali kubwa sana ambalo mtu unaweza kujiuliza ni kwa nini?
Jibu ni kwamba ule mkumbo na motisha ya tarehe moja vinakuwa vimeisha. Mwanzoni unapokweka malengo unakuwa na motisha kubwa, ila kadiri siku zinavyokuwa zinazidi kwenda, ile motisha inapotea, sasa watu huwa wanaishia hapo. ila sasa wewe haupaswi kuishia hapo, baadala yake unapaswa kuendelea kujisukuma zaidi ili uweze kufika kule unapotaka kufika. Na utaweza hili kama utajiwekea utaratibu wa kuwa unajikumbusha malengo yako karibia kila siku. Kila siku hakikisha kwamba unaandika chini malengo yako ambayo unayafanyia kazi, ili usiyasahau.
Pili, usisubiri mpaka uwe kila kitu ili ufanyie kazi malengo yako. Kuna watu wanaweka malengo mazuri tu, ila kinachowafanya washindwe kuweza kufanyia kazi malengo yao na kuyatimiza ni kwa sababu wanasubiri mpaka wawe na kila kitu ili waje kufanyia kazi malengo yao. Naomba unisikilize kwa kitu, huhitaji kuwa na kila kitu ili uwezer kufanyia kazi malengo yako. Anza na kile ulichonacho, fanya kile kinachowezekana, mwisho wa siku utajikuta kuwa umeweza kufanya yasiyowezekana.
Tatu, usisubiri mpaka tarehe 31 disemba ili ufanyie kazi malengo yako. Wengine wanaweka malengo makubwa ila wanasubiri mwisho wa mwaka ili malengo yao hayo yaweze kutimia. Unachopaswa kufahamu ni kuwa malengo makubwa huwa hayatimii mwishoni mwa mwaka. Hivyo, badala ya wewe kusubiri mpaka mwisho wa mwaka ili uweze kutimiza malengo yako, anza kuyafanyia kazi siku ya leo hata kama ni kwa udogo.
Nne, watu waliokuzunguka. Moja kati ya usemi wenye ukweli mkubwa sana ndani yake ni usemi kuwa miaka mitano ijayo utakuwa jisnsi ulivyo isipokuwa kwa vitu viwili tu, watu waliokuzunguka na vitabu unavyosoma. Rafiki yangu, kama kuna kitu unahitaji sana ili kuweza kufikia malengo yako basi ni watu, hakikisha kwamba unazungukwa na watu ambao ni chanya na wale ambao wanaendana na malengo yako.
Watu ambao ni hasi watakufanya ukwame na ushindwe kuweza kufkia malengo yako.
Tano, kuweka malengo madogo sana. malengo madogo yanakunyima hamasa na yanakufanya ushidnwe kusonga mbele ila malengo makubwa yanakupa msukumo wa kufanya makubwa na kujisukuma zaidi. hivyo basi rafiki yangu nakushauri sana uweke malengo makubwa na kila mara uhakikishe kwamba unajisikuma kwenye kuyafanyia kazi na kuyatimiza. Kamwe usirudi nyuma kwenye kufanyia kazi malengo yako.
Kil la kheri
Umakuwa nami rafiki yako wa ukweli
Godius Rweyongeza
0755848391
Morogoro-Tz
One response to “Vitu Vitano Vitakavyokuzuia wewe kufanikisha malengo yako”
[…] SOMA ZAIDI: Vitu Vitano Vitakavyokuzuia wewe kufanikisha malengo yako […]