Mara kwa mara kuna watu huwa unakuta wameandika kwenye sehemu mbalimbali mtandaoni au nje ya mtandaoni wakiwa maneno kama “dancing mode activated” au running mode activated n.k
Sasa tunapouanza mwaka mpya 2024, kuna maeneo muhimu sana ambayo wewe unapaswa kuya”activate” na kuhakikisha yako “activated” kwa mwaka mzima unaokuja.
- UWEKEZAJI (INVESTING MODE ACTIVATED). Huu mwaka huu, usirembe mwandiko linapokuja suala zima la uwekezaji. Zembea sehemu nyingine lakini usizembee kwenye uwekezaji. Ufanye uwekezaji kuwa kipaumbele kwako ndani ya huu mwaka. Yaani, kila unapopokea fedha, kipaumbele chako cha kwanza kiwe ni kufanya uwekezaji. Na hata baada ya kuwa umeweza kufanya uwekezaji, kiasi kingine ambacho kitabaki, ondoa matumizi yoyote yale ambayo siyo ya lazima ili fedha nyingi uweze kuielekeza kwenye uwekezaji.
SOMA ZAIDI: Uwekezaji Kwenye Hisa vs Uwekezaji Kwenye Maeneo Mengine
- KUONGEZA KIPATO. Ili uweze kuweka akiba, unapaswa kuhakikisha kwamba una kipato cha uhakika. Wengi huwa wanafikiri kwamba tunapozungumzia kipato cha uhakika basi tunakuwa tunzungumzia ajira hasa ya serikalini.
Japo wengi wanaiona ni ajira ya uhakika, ila mimi sioni uhakika wowote ndani yake. Ajira ni ajira tu. Kumbe unapasawa kuwa unafikiria nje ya ajira mara zote. Na unafikiria nje ya ajira kwa kuhakikisha kwamba, unaanza kutengeneza vyanzo vingine vya kipato ambavyo vinakuingizia kipato nje ya ajira yako. Kwenye maisha yako usikubali kipato chako cha mwaka jana kuendelea kubaki vilevile ya mwaka unaofuata. Kila mwaka tafuta namna ya kuhakikisha kwamba kipato chako unakiongeza walau mara mbili zaidi ya kilivyokuwa mwaka mmoja ambao umetangulia. Na kama kuna mbinu ambayo unaona unaitumia na inaleta matokeo, basi hiyo mbinu kamwe usiache kuitumia. Itumie zaidi na zaidi ili uweze kuleta matokeo makubwa zaidi.
SOMA ZAIDI: Unawezaje Kujiajiri kwa Mtaji Kidogo?
- Vitendo (action mode activated). Mambo yote unayojifunza hapa, hayatafanya kazi kama wewe hutakuwa tayari kuyafanyia kazi. Ni mpaka ufanye kazi ndiyo utaweza kupata matokeo. Hivyo, mwaka huu fanyia kazi kila unachojifunza bila ya kurudi nyuma.
SOMA ZAIDI: Nguvu Ya Vitu Vidogo Kuelekea Mafanikio Makubwa katika Vitendo;
- Biashara (business mode activated). Ili kuongeza kipato chako mara mbili unahitaji kuhakikisha kwamba unakuwa na biashara. Biashara ndiyo njia pekee ya uhakika ambayo inafahamika ya kuongeza kipato chako mara mbili zaidi kadiri muda unavyokwenda, ni tofauti na njia nyingine zozote zile. Uongezwaji wa kipato kwenye ajira, una ukomo. Na mshahara kwenye ajira hauwezi kuongezeka mara mbili kila mwaka kwenye ajira. Lakini kwenye biashara, kama kweli utajifunza biashara kwa kina na kufanyia kazi yale unayotakiwa kufanyia kazi. Inawezekana. Kama kweli utaongeza juhudi zaidi kwenye mauzo ya biashara yako, ni ukweli kuwa unaenda kufanya makubwa kwenye biashara yako bila ya kurudi nyuma. Hivyo basi, mwaka huu wa 2024, kama bado hauna biashara, anzisha biashara. Kama una biashara tayari, basi ongeza juhudi zaidi na zaidi li uweze kuwafikia watu wengine zaidi.
SOMA ZAIDI: Vitu Vitano Vitakavyokuzuia wewe kufanikisha malengo yako
- Watu (people mode activated). Watu ni muhimu sana, ili ufanikiwe, unahitaji watu. Aidha ni watu wa kukusaidia wewe ili uweze kufanikisha ndoto na malengo yako. Wanaweza pia kuwa ni watu wa kukusimamia (makocha na mamenta). Aidha wanaweza kuwa ni timu yako unayofanya nayo kazi. Sasa wewe unahitaji ujuzi sahihi wa kukaa na watu na kuweza kufanya nao kazi. Unahitaji ujuzi wa kuhamasisha watu ili waweze kuchukua hatua kwenye majukumu yao ambayo wanatakiwa kufanyia kazi. Jifunze sana kuhusu watu na namna ya kushughulika nao. Huu ujuzi utakusaidia sana ndani ya huu mwaka 2024. Kumbuka, pesa zako wanazo watu. Kama umeajiriwa maana yake unamtegemea bosi wako ili aweze kukulipa mshahara (mtu). Na unahitaji kujua namna sahihi ya kuendana naye. Kama umeajiajri maana yake unategemea wateja wanunue kwenye biashara yako (watu). Na unapaswa kujua namna sahihi ya kushughulika nao. Kama umeajiri maana yake unafanya kazi na watu tayari. Unapaswa kujua namna sahihi ya kushughulika na watu wako. Kwa vyovyote vile rafiki yangu, hakikisha kwamba unakuwa na ujuzi sahihi wa kushulika na watu huu ujuzi utakusaidia parefu sana kwenye maisha yako.
Hizi ndizo aina za ujuzi ambazo unapaswa kuanza kuzifanyia kazi mara moja kwa manufaa yako wewe mwenyewe
Najua kuwa ungependa kupata ushauri wa karibu zaidi moja moja kwa moja kutoka kwangu. Nitafute tuone ni lini nitakuwa na muda, ili nikupangie ratiba ya kuongea na wewe. Utalipia kiasi kidogo tu.
Saa moja ni laki moja mazungumzo kwa njia ya mtandao.
SAA MOJA NI LAKI MBILI NA NUSU MAZUNGUMZO YA ANA KWA ANA. Malipo yanafanyika kwanza, kisha unapewa tarehe (appointment) tutakapoweza kuongea
Tumia namba ya simu +255 755 848 391 kuwasiliana nami.
Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.
Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa
Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com
Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana naye kwa +255 684 408 755 na orodha ya vitabu vyenyewe unaweza kuiona HAPA. Chagua unachopenda, kisha twanga, +255 684 408 755
Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396
For Consultation only: +255 755 848 391 au godiusrweyongeza1@gmail.com