Kwa Nini Watu Wenye Kipaji Hushuka Kiwango


KIPAJI NI DHAHABU
Rafiki yangu, nimeandika kitabu. Kinaitwa KIPAJI NI DHAHABU. Ili kupata kitabu hiki, wasialiana na mi kwa 0755848391 sasa

Nadhani umewahi kusikia hili, kuwa wachezaji au wasanii au hata wawekezaji wameshuka viwango. Unakuta mtu mwanzoni alikuwa na kipaji na uwezo mzuri sana ambao alikuwa akiutumia kwa viwango vikuwa na viwango vya hali ya juu, ila kadiri siku zinavyoenda basi mtu huyo anazidi kushuka viwango mpaka kufikia hatua ambapo inadhihirika kuwa kiwango chake kimeshuka. Sasa kwa nini baadhi ya watu hushuka viwango?

Kwenye makalaya leo tunaenda kuona sababu kwa nini baadhi ya watu hushuka viwango, na jinsi ambavyo wewe unaweza kuepuka hili.

Moja ya kitu kinachofanya watu washuke viwango ni kukosa nidhamu ya kazi.

Unakuta mtu alikuwa anajituma sana kwenye kazi mwanzoni alipoanza kufanyia kazi kipaji. Mtu yupo tayari kufanyia kazi kipaji chake kwa saa 15 na zaidi kila siku kwa siku saba za wiki bila ya kupumzika, ila pale anapoanza kufanikiwa na kuapata mafanikio mazuri anarelax na kusahau kabisa kuwa anapaswa kupambana kuhakikisha kuwa anaendelea kunoa kipaji chake.

Tena wengine huwa wanapanda mpaka kufikia viwango vya juu kabisa, ila sasa kadiri ambavyo siku huwa zinaendelea basi huwa inafikia hatua ambapo huwa wanarudi nyuma kwa sababu ya kukosa nidhamu ya kazi. kama ambavyo tumeshaona mpaka hapa, ninachotaka ujue ni kuwa unapaswa kujituma kwenye kazi kama vile muda wote na mara zote wewe ni mchanga.

Kingine ni kuendekeza Starehe sana kuliko kazi. Hiki ni kitu kingine ambacho kinawakumba watu wengi wenye vipaji. Mtu anapoanza kujulikana na kupata hela kutokana na kipaji chake, basi kinachofuata kinakuwa ni starehe. Sasa hiki kitu lazima baadaye kinawaponza watu kwa sababu starehe kwa vyovyote vile unapaswa kuzigharamikia.

Njia ya kuondokana na hali hii ni kujifanya mara zote kama vile hauna pesa. kila ukipata fedha unaiwekeza sehemu ili tu uendelee kuweka juhudi zaidi na kupata fedha zaidi. Na kumbuka kuwa hapa nimeongelewa kuiwekeza fedha, wala siyo kitu kingine.

Kuiga maisha ya baadhi ya watu. kadiri unavyokuwa unapanda viwango, ndio unakutana na watu wengine zaidi. sasa moja ya kitu ambacho kinaweza kukupumbza ni pale unapokutana na watu wengineambao wanaonekana kama hawaweki juhudi kwenye kazi ila wanapata matokeo mazuri. Hiki kitu kinaweza kukupumbaza na kudhani kuwa hata usipoweka juhudi wala kazi utapata matokeo mazuri tu. Ninachotaka kukwambia rafiki yangu ni kitu kimoja tu, na kitu hiki ni kuwa, juhudi na kazi kwenye kile unachofanya haziwezi kukuangusha.

Lakini pia nataka ujifunze kutoka kwa jamaa mmoja ambaye niliwahi kusoma stori yake kwenye kitabu kimojawapo cha Robert Greene. Huyu jamaa alikuwa na kipaji ila alikuwa ni miongoni mwa watu ambao walikuwa wanafanya mazoezi sana nyuma ya pazia.

Yaani, yeye alikuwa na fomula ambayo ni wachache sana wanaoifahamu. Fomula hii ilikuwa ni kwamba muda wa usiku alikuwa anachapa kazi na kujituma na kufanya mazoezi yote ambayo alikuwa anapaswa kufanya.

 Alikuwa anajituma sanasana nyuma ya pazia wakati wa usiku kiasi kwamba hakukuwa na mtu ambaye alikuwa anajituma kwa viwango kama vya kwake. Ila muda wa mchana alikuwa anajidai kama mla bata vile. Yaani, muda wa mchana alikuwa anarelax na kutulia. Ulipokuwa unafika wakati way eye kufanya maoonesho, alikuwa kiyafanya vizuri kiasi kwamba watu walikuwa wanashangaa kwa namna ambavyo alikuwa akifanya vizuri sana.

Baadaye sana ndipo wachache walikuja kugundua kuwa huyu jamaa alikuwa akifanya mazoezi ya nguvu sana muda wa usikua na na kupumzika muda wa mchana. Hapa ninachotaka kukwambia siyo kwamba ufanye mazoezi muda wa usiku na muda wa mchana ulale, la hasha! Ila ninachotaka kukwambia ni kuwa unapaswa kufanya mazoezi ya kutosha nyuma ya pazia. Ili pale utakapofika muda wa wewe kuonekana mbele ya watu basi unafanya vizuri sana.

Kitu kingine kinachowakwamisha watu wenye kipaji ni kujiona kwamba wameshafika, wakati safari yao ikiwa bado tu. Yaani, yale mafanikio ya muda mfupi yanamfanya mtu anafikiri kwamba tayari amefika wakati safari yake bado inaendelea.

Rafiki yangu naomba kujua ni kitu gani ambacho kinakukwamisha wewe kwa muda huu. Ebu niambie hapa chini kwenye sehemu ya maoni.

Makala zaidi za kusoma


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X