Kila mwaka serikali kupitia benki kuu ya Tanzania huwa inatoa takwimu za mfumuko wa bei. Unakuta ripoti inasema kwamba mwaka huu mfumuko wa bei ni asilimia 4, 5,au 3.5,7 au vyovyote vile kulingana na ripoti inavyokuwa inasema.
Wengi huwa hawajui mfumuko wa bei ni kitu gani na una madhara gani kwao.
Leo hii ningependa kukueleza mfumuko huu wa bei kwa lugha rahisi sana kiasi kwamba ukishasoma hapa uweze kumweleza mwanao wa miaka 6, aweze kukuelewa.
Mfumuko wa bei ni pale ambapo fedha inapoteza uwezo wake wa kununua vitu.
Tukichukulia mfano wa shilingi mia tano. Mwanzoni mwa miaka ya 2000, kama ulikuwa na shilingi mia tano,ungeweza kununua kipande cha sabuni, kiberit na chumvi na bado ukabaki na chenji. Ila leo hii, kwa shilingi mia tano hiyo hiyo, huwezi kununu hata kipande kimoja cha sabuni. Hii ndio kusema kwamba fedha imepoteza uwezo wake wa kufanya manunuzi.
Shilingi mia tano imebaki kuwa ileile, ila uwezo wa kununua vitu kama ilivyokuwa mwaka 2000 siyo kama ulivyo sasa hivi.
Serikali ikitangaza kwamba mwaka huu mfumuko wa bei ni asilimia 4. Maana yake uwezo wa fedha kufanya manunuzi umepungua kwa asilimia 4.
Hii ndio kusema kwamba kama una shilingi elfu moja kama akiba haiwezi tena kufanya manunuzi kama iliyokuwa inafanya mwaka jana.
Kama mwaka jana shilingi elfu moja ilikuwa inaweza kununua
- Sabuni kipande kimoja (500)
- Kiberiti (100)
- Kalamu kwa ajili ya mwanao 200/-
- Na ukabaki na chenji 200
Mwaka huu hutaweza kufanya manunuzi hayohayo na hela yako hiyohiyo. Elfu moja itabaki kama elfu moja. kama ni noti itakabaki kama elfu moja noti, ila uwezo wake wa kufanya manunuzi utapungua kwa shilingi 40. Kumbuka mfumuko wabei ni asilimia 4.
Kwa hiyo kwa mwaka huu maana yake vitu vitapanda bei kidogo. na hivyo chenji uliyobaki nayo mwaka jana itapungua au pengine hutakuwa na chenji tena!
Sasa unafanyaje ili kuukwepa mfumuko wa bei.
Njia pekee ya kuukwepa mfumko wa bei ni kufanya uwekezaji. Ambao unaweza kukupa mrejesho ambao ni mkubwa kuliko uwekezaji.
Ndio maana nimekuwa nashauri watu kuwekeza UTT. UTT wamekuwa wanatoa mrejesho mkubwa ulio juu ya mfumuko wa bei.
Ili uniewe vizuri angalia kwanza chati hii hapa chini.
Mrejesho wa wastani tangu kuanzishwa mei 2005 ni asilimia 15.7
Hii ndio kusema kwamba kama uliweka shilingi elfu moja kwenye mfuko wa UTT mwaka 2005, mpaka leo hii hiyo shilingi elfu moja tu uliyoweka, imekuwa inapata ongezeko la wastani wa asilimia 15.7 kila mwaka.
Hii ndio kusema kwamba kila mwaka elfu moja yako, imekuwa inapata ongezeko la asilimia 157 kwenye UTT ukitoa mfumuko wa Bei bado unakuwa juu.
Mfano kwa mwaka huu ambao mfumuko wa Bei ni asilimia 4.4 Kama tukivyoona hapo juu, maana yake.
Kama hiyo elfu moja yako uneiweka UTT, ukapata mrejesho wa 15.7 Ni sawa na ongezeko la shilingi 157.
Ukitoa kiasi kikichotokana na mfumuko wa bei. Yaani, shilingi 44 maana yake utakuwa na (157-44=113).
NB. Wastani wa mrejesho wa 15.7 Ni wa jumla kwa yangu mfuko wa UMOJA uanzishwe mwaka 2005 mpaka 2022 Juni 31.
Ili lunielewe vizuri naomba nitolee mfumuko wa bei kwa mwaka mmoja uliopita.
Tuchukulie mfano tuna watu wawili
Bwana CHACHA NA BW. MWASHA
Bwana Chacha ana shilingi elfu moja, ambayo ameiweka akiba chini ya godoro mwaka 2021 julai mosi. Mwaka mmoja baadaye, tarehe 31 Juni 2022, serikali kupitia benki kuu ya Tanzania (BoT) inatangaza kuwa mfumuko wa bei ulikuwa ni asilimia 4.4 kama inavyoonekana kwenye jedwali hapo chini
Hii ndio kusema kwamba thamani ya fedha ya bw. Chacha, itakuwa imepungua uwezo wa kufanya manunuzi kwa shilingi 44/- tu. Elfu moja yake aliyoiweka akiba, itabaki kama elfu moja. ila itakuwa imepungua uwezo wa kununua kwa shilingi 44 tu.
Yaani, kama bw. Chacha alikuwa anaweza anaweza kununua
- Karanga (kwa shilingi 100)
- Pipi kifua (shilingi 50)
- Andazi (shilingi 100)
- Sabuni 500
- Kitunguu 100
- Majani ya chai (shilingi 100)
- Na kubaki na chenji ya shilingi 50
Kwa mfumuko wa bei wa mwaka huu, ambao ni asilimia 4.4, maana yake akienda dukani kununua vitu. Ile chenji yake ya shilingi 44. Haitabaki, badala yake itabaki shilingi 6 tu. kama mwenye duka ana shilingi 6, basi atampa hiyo shilingi 6.
Mfumuko wa bei umemeza shilingi 44. Maana yake vitu alivyokuwa ananunua hapo zamani kwa elfu moja na kubaki na chenji sasa hivi vimepanda bei.
ILA KWA UPANDE MWINGINE
Bwana Mwasha naye ana shilingi elfu moja, ambayo ameiweka UTT mwaka 2021 julai mosi. Mwaka mmoja baadaye, tarehe 31 Juni, serikali kupitia benki kuu ya taifa inatangaza kuwa mfumuko wa bei ulikuwa ni asilimia 4.4 . lakini wakati huohuo, mfuko wa UTT, ukatangaza ongezeko la thamani la asilimia 11.7 kama inavyoonekana hapo chini.
Hii ndio kusema kwamba mfumuko wa bei wa asilimia 4.4 ni sawa na shilingi 44 na
Ongezeko la thamani la asilimia 11.7 lilitolewa UTT ni sawa na shilingi 117. Hivyo basi, kwenye ile elfu moja yetu. Tutaongeza shilingi 117 ambayo UTT wametoa kama ongezeko la Thamani, hivyo ile elfu moja ya Bw. Mwasha aliyokuwa nayo mwanzoni mwa mwaka 2021 itakuwa tena siyo elfu moja bali itakuwa ni shilingi 1117. Tukitoa kiwango cha mfumuko wa bei ambayo ni shilingi 44 tutabaki na 1073.
Kwa hiyo bwana Mwasha akifanya manunuzi baada ya mfumuko wa bei bado atabaki na shilingi 73 ya chenji.
Bw. Chacha atakuwa ameupiga mfumuko wa bei na kuukwepa.
Kumbe basi, njia pekee ya mtu yeyote yule kuukwepa mfumuko wa bei, ni kuhakikisha kwamba anafanya uwekezaji, na eneo la kuanzia ni kwenye Hisa, hatifungani na vipande.
Ndio maana nashauri wewe rafiki yangu uweze kujipatia nakala ya kitabu cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE.
Kitabu hiki cha kipekee gharama yake ni 20,000/- tu. na utaletewa popote pale utakapokuwa. Nakala laini Ni 10,000/-
Kwenye hiki kitabu nimeeleza kwa kina dhana nzima ya mfumuko wa Bei. Na mengine mengi yako kwenye kitabu
Tuwasiliane sasa kwa 0755848391 ili uweze kupata nakala yako.
Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.
Godius Rweyongeza ni mwandishi wa vitabu zaidi zaidi ya 20. Na ni mwendeshji wa mtandao wa Songambele. Amekuwa akiandika kwenye huu mtandao huu tangu mwaka 2016. Kitabu chake cha Kutoka Sifuri Mpaka Kileleni kimekuwa #1Best Seller kwa muda sasa kwenye mtandao wa GETVALUE
Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.
Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.
Mtandaoni, vitabu vyake unaweza kuvipata kupitia mtandao wa GETVALUE kwa KUBONYEZA HAPA
2 responses to “Mfumuko wa bei ni nini?”
[…] kwenye makala ya jana tuliongelea juu ya suala zima la mfumuko wa bei. Lakini mwisho wa siku tuliona ni kwa namna gani […]
[…] SOMA ZAIDI: Mfumuko wa bei maana yake nini? […]