Kwa Nini Unahitaji Kuwa Na Vyanzo Vingi Vya Kipato


Unahitaji Kuwa na vyanzo vingi vya kipato

Moja ya Kitu Cha muhimu ambacho unahitaji  kuhakikisha umekizingatia ni kuwa na vyanzo vingi vya kipato. Labda swali la kwanza la kujiuliza ni je, vyanzo vingi vya kipato maana yake nini?

Vyanzo vingi vya kipato, Ni pale unapokuwa unaingiza kipato kwa njia zaidi ya moja. Yaani, siyo tu unakuwa unategemea njia moja ili kupata fedha, bali unakuwa na uhakika wa kuingiza kipato kupitia vyanzo mbalimbali. Vyanzo hivyo vinaweza kuwa ni
1. Ajira yako
2. Ujuzi wako
3. Uwekezaji
4. Biashara
4.  Kamisheni
5. Mrabaha n.k

Kwa nini unahitaji kuwa na chanzo zaidi ya kimoja cha kipato.

Rafiki yangu, hiki Kitu cha kuwa na chanzo zaidi ya kimoja cha kipato, hakifundishwi shuleni na hata majumbani. Hii ni elimu ambayo MTU unajiongeza kwa kuhakikisha unakuwa nayo huku mtaani. Ila ni elimu ya lazima na wala siyo hiyari.

Kuna sababu nyingi za kwa nini unapaswa kuwa na vyanzo vingi vya kipato.

Kwanza ni kwa sababu ya mabadiliko ambayo huwa yanatokea. Hiki kitu kinaweza kufanya baadhi ya vyanzo vya kipato  visikuingizie kipato. Mfano mfumuko wa bei ambao umetokea mwaka huu, kwa namna moja au nyingine unakuta kwamba unaathiri kipato chako, pia. Unakuta kwamba fedha uliyokuwa nayo haitoshi kukuwezesha wewe kununua bidhaa husika. Ndio maana unahitaji kuhakikisha kwamba unakuwa na chanzo kingine Cha kipato

Pili, ni Kujijengea kinga. Kama unakitegemea  na chanzo kimoja tu cha kipato ili uingize fedha, unakuwa unapotea rafiki yangu. Kwa sababu inaweza kutokea siku moja ambapo chanzo hicho kikawa hakijaingiza kipato kama inavyostahili. Hiki Kitu kitakufanya wewe ukwame kufanikisha malengo yako. Lakini unapokuwa una chanzo zaidi ya kimoja, huo ndio unakuwa ni mwanzo wa wewe kupiga hatua Kubwa kimaisha. Kwa sababu chanzo kimoja Cha kipato kinapokwama, kingine kinakuwa tayari kufanya kazi kwa ajili yako na kuhakikisha kwamba kimekuinua zaidi.

Tatu, Huwa Kuna mabadiliko ya hapa na pale ambayo huwa yanatokea karibia kwenye kila sekta, ambayo huwa yanapelekea aidha kipato kushuka au hata muda mwingine kukoma kabisa. Ninachoshauri rafiki yangu Ni wewe kujiwekea Kinga kwa kuhakikisha unakuwa na chanzo zaidi ya kimoja Cha kipato.

Nne, ili kuingiza fedha kwa nyakati tofauti. Chanzo maarufu ambacho watu wanacho ni ajira. Ajira huwa inaingiza fedha kwa MTU mara moja kwa mwezi, mwishoni mwa mwezi, lakini unaweza kuwa na vyanzo vingine ambavyo vinaweza kukuingizia kipato tofauti na ajira na hivyo kukupa uhakika zaidi.

Tano, kufanya mishahara yako ikutane. Imezoeleka miongoni mwa wafanyakazi kuwa mishahara huwa haikutani, vyanzo vingi vya kipato vina uwezo wa kuifanya mishara yako iweze KUKUTANA.

Sita, vyanzo vingi vya kipato, vina uwezo wa kukufanya ufanye uwekezaji. Kama mshahara pekee ulikuwa haukutoshi, sasa vyanzo vingi vya kipato, vinakuwezesha wewe kufanya uwekezaji pia. Chanzo kimoja kinaweza kutumika kwa ajili ya uwekezaji na chanzo kingine kikasaidia kwenye matumizi ya hapa na pale ya kila siku 

Sifa ya vyanzo vingi vya kipato

Kuna watu baada ya kusikia kuwa wanapaswa kuwa wanapaswa kuwa na vyanzo vingi vya kipato wameenda kichwakichwa na kujikuta waanzisha vyanzo vingi vya kipato, ilimradi tu wameanzisha Sasa zifuatazo Ni sifa za vyanzo vya kipato.

Kwanza, vyanzo vyako vinapaswa kuwa kwenye sekta tofauti. Yaani, usitegemee sekta moja tu kwa ajili ya kukuingizia kipato. Mfano kipindi Cha Corona Kuna baadhi ya sekta zilikwama au kufungwa kabisa, lakini kipindi hichohicho sekta nyingine zilizidi kukua na kuwa na kuwa Bora ZAIDI. Sasa kwa MTU ambaye anategemea sekta Moja kwa ajili ya kuingiza kipato, na Kama sekta hiyo iliyumba basi, ni wazi kuwa MTU huyu Atakuwa aliyunva pia.

Kwa hiyo basi, vyanzo vyako visiwe kwenye sekta moja.

Kama ni kampuni au biashara, usiwe na bidhaa moja tu, maana Kuna baadhi ya bidhaa huwa zinauzika Sana kipindi fulani. Sasa ikitokea unategemea chanzo kimoja Cha kipato na kipindi hicho chanzo hicho kikakwama, Basi Ni wazi kuwa na wewe utakwama.

Pili, Vyanzo vyako visikutegemee wewe kufanya kazi ili viingize kipato vyanzo vyako vyote rafiki yangu havipaswi kuwa vinakutegemea wewe kufanya kazi moja kwa moja ili uingize kipato.

Ndio chanzo kimoja au viwili vinaweza Kuwa vinakutegemea wewe kufanya kazi moja kwa moja, ila kama unavyojua rafiki yangu. Kufanya kazi huwa juna ukomo. Unafanya kazi na unachoka. Kumbe basi, baadhi ya vyanzo vya kipato havipaswi kuwa vinakutegemea wewe ufanye kazi moja kwa moja ili uingize kipato. Vingine vinapaswa kuwa na uwezo wa kukuingizia kipato hata kama hufanyi kazi. Vingine unapaswa kufanya kazi Mara moja na vikulipe milele. Mfano mzuri ni Kama kuandika kitabu. Ukiandika kitabu, unafanya kazi Mara moja, Ila kipato kinachotokana na kazi hiyo ya Mara moja kinakuwa cha kudumu maisha yako yote.
Au kutengeneza video kama YouTube. Ukishaitengeneza video hii ndio unakuwa umeitengeneza.

Makosa kwenye vyanzo vingi vya kipato

Kosa la kwanza huwa ni kuanzisha vyanzo vyote vya kipato kwa wakati mmoja.
Kutegemea na Aina ya chanzo Cha kipato, baadhi ya vyanzo vya kipato haviwezi kuanzishwa kwa wakati mmoja. Kuna baadhi ya vyanzo vinapaswa kuanzishwa kwa nyakati tofauti, ili kukupa wewe mwanya wa kujenga chanzo kimoja kwa uhakika kwanza.

Kosa la pili huwa Ni kuchanganya hela kutoka kwenye kila chanzo. Wengi wanapopokea hela kutoka kwenye vyanzo mbalimbali huwa wanazichanganaya na kuzitumia bila ya mwelekeo wowote. Hivyo basi, nashauri uwe na utaratibu wa kutofaytisha hela zinazotoka kwenye chanzo kimoja na hela zinazotoka kwenye chanzo kingine.

Na ikiwezekana kabisa uwe na malengo kwamba fedha itakayotoka sehemu fulani, nitaielekeza kwenye kufanyia kazi Jambo fulani wakati fedha ambayo itatoka kwenye chanzo kingine utafanya jambo jingine.

Tatu ni kutoa hela kwenye chanzo kimoja na kuiweka kwenye chanzo kingine.
Ni wazi kuwa pale unapoakzisha chanzo fulani Cha kipato, unakuwabunaweka fedha. Ila inabidi ifikie hatua ambapo wewe utakuwa huweki fedha, badala yake chanzo kiwe kinakupa wewe kipato.

NI VYANZO KIASI UNAPASWA KUWA NAVYO.


Hili nalo neno! Tafiti mbakimbali zimeonesha kuwa vyanzo vinne mpaka vitano, vinatosha sana kukufanya uishi maisha mazuri.

Kumbe basi idadi yako ya kwanza ya vyanzo vyako vya kipato ipiganie iwe nne mpaka saba. Na Hivi viwe vyanzo vya uhakika.


Mpango wako wa kuongeza kipato Cha ziada mwaka 2023 ukoje? Unafanyaje ili kuhakikisha unakuwa na chanzo kingine Cha ziada?

Karibu kwenye Semina ya kufungua mwaka 2023. Semina hii itaendeshwa kwa njia ya mtandao na imelenga kuhakikisha inakupa wewe mbinu za kuongeza kipato chako mara mbili mpaka mara kumi zaidi.

Semina hii itadumu kwa siku 15 kuanzia Januari 15 mpaka tarehe 30.
Kwa siku zote hizo 15 utalipia 15,000/- tu.

Unataka kuongeza kipato chako Mara mbili mpaka Mara kumi zaidi ndani ya mwaka 2023, Basi jiunge kwenye Semina hii.

Karibu sana

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

Godius Rweyongeza ni mwandishi wa vitabu zaidi zaidi ya 20. Na ni mwendeshji wa mtandao wa Songambele. Amekuwa akiandika kwenye huu mtandao huu tangu mwaka 2016. Kitabu chake cha Kutoka Sifuri Mpaka Kileleni kimekuwa #1Best Seller kwa muda sasa kwenye mtandao wa GETVALUE

Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.

Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.

Mtandaoni, vitabu vyake unaweza kuvipata kupitia mtandao wa GETVALUE kwa KUBONYEZA HAPA


2 responses to “Kwa Nini Unahitaji Kuwa Na Vyanzo Vingi Vya Kipato”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X