Nimepata kusoma kitabu cha THE YOUNG INVESTOR (Projects and activities for making your money grow)


Hiki ni kutabu cha uwekezaji ambacho kimeandaliwa maalumu kwa ajili ya watoto, kinalenga kuwafundisha watoto juu ya uwekezaji na namna gani wanaweza kuanza kufanya uwekezaji.

Hata hivyo mtu mzima kama wewe unaweza (na unapaswa) kukisoma kitabu hiki pia. Na kwa kuwa lugha iliyotumika kwenye hiki kitabu ni lugha rahisi kwa ajili ya kuwafanya watoto waelewe, wewe mtu mzima ukisoma kitabu hiki, utakielewa zaidi.

Kitabu ni kidogo tu, kina kurasa kama 124 hivi, hivyo unaweza kukisoma ndani ya wiki moja kikaisha. Binafsi nimekisoma na kukielewa.

Kuhusu mwandishi wa kitabu hiki
Mwandishi wa kitabu hiki ni Katherine R. Bateman. Mwandishi ameandika kitabu hiki kwa ajili ya wajukuu wake. Anasema kwamba alikuwa na shauku kubwa ya kuwafundisha wajukuu wake kuhusu uwekezaji.

Hivyo alianza kukusanya taarifa kwa ajili ya wajukuu wake, kila alipokuwa   anaongea na watu juu ya hilo, jibu alilopata kutoka kwa watu lililuwa kwamba akishaandika kitabu awataarifu wanunue nakala pia.

Hili jambo lilimfanya mwandishi ahakikishe anaandika kitabu kinakamilika.

Sasa hapa ningependa kukwambia yafuatayo ambayo nimejifunza kutoka kwenye kitabu.

1. Kitu cha kwanza ambacho ningependa na wewe uondoke nacho ni kuwa na wewe utapaswa kuandika kitabu. Siyo lazima kiwe cha fedha kama hiki, lakini unaweza kuandika kitabu kinachoendana na ujuzi wako. Nakuhakikishia wanao na wajukuu wako watakipenda kitabu hicho. Kama wewe umekuwa mwanakwaya kwa miaka sasa, ebu hata tuandikie kuhusu safari yako ya kuimba, najua una mengi ya kuandika. Kama bado unakwama uandike nini, hakikisha unapata kitabu changu cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU (kwa saaa softcopy ni 5,000/).

2. Hisa siyo makaratasi tu, na wala siyo cheti unachopata baada ya kununua hisa. Bali ni umililiki wa kampuni.

3. Unapaswa kutawanya uwekezaji wako kwenye maeneo tofautitofauti. Kwenye hisa, hatifungani pamoja na vipande.

4. Kama kuna kampuni unapenda kutumia bidhaa zake, hakikisha unanunua hisa zake pia.

Kitabu kina mambo mengi, binafsi nimeandika machache tu kwa sababu nilitaka niweke kumbukumbu kuwa niliwahi kusoma kitabu hiki. Na njia ya mimi kuweka kumbukumbu ni kuandika makala kama hii hata kama ni fupi

Ili unufaike na kitabu hilo, hakikisha unakisoma mwenyewe.
Kipakue mwenyewe kwa kufuata mwongozo huu hapa

Karibu sana

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.

Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.

Mtandaoni, vitabu vyake unaweza kuvipata kupitia mtandao wa GETVALUE kwa KUBONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X