Baadhi Ya Vyanzo Vya Kipato Ambavyo Unaweza Kuwa Navyo


1. Ajira
Hiki ni chanzo maarufu ambacho wengi huwa wanakuwa nacho. Chanzo hiki huwa kinaingiza kipato (ujira) kila baada ya muda fulani (siku,wiki au mwezi). Kwa MTU yeyote ambaye hana sehemu ya kuanzia hakikisha walau unaanzia kwenye ajira.

Ukipata ajira hakikisha unaifanya kwa uaminifu na kwa kujituma. Maana ajira inaweza kukupelekea wewe kupata vyanzo vingine zaidi.

2. Kitabu
Naamini wewe utakuwa na uzoefu  mkubwa ambao wengine wanatamani kuupata kutoka kwako. Uzoefu huu unaweza kuuweka kwenye kitabu na watu wakasoma hiki kitabu.

Kama wewe umekuwa unafuga ng’ombe kwa miaka kumi sasa, tayari una uzoefu wa kutosha wa kuandika kitabu kuhusu ufugaji wa ng’ombe. Utumie uzoefu huu, kuandika kitabu. Kuna watu watapenda kusoma kitabu chako.

Leo hii unaposoma hapa, Kuna MTU sehemu anajiuliza naweza kuanza kufuga ng’ombe wa kisasa. Nini kinahitajika? Napaswa kuepuka Nini? Napata wapi ndama wa kuanza nao? MTU huyuhuyu anaendelea kujiuliza, hivi ng’ombe huwa wanachanjwa? Kila baada ya muda gani? Kwa Nini?

Na wewe una uzoefu huu, Tena wa miaka mitatu, mitano au kumi na zaidi. Kwa Nini usiandike kitabu?

Naomba unisikilize, kaa chini andika kitabu ili watu waweze kunufaika na uzoefu wako huu.

Japo watu watapaswa kununua kitabu chako ili wanufaike, ila ubora ni kwamba baada ya hawa watu kusoma kitabu chako, watakushukuru sana kwa namna ulivyowasaidia.

Unajiuliza unawezaje kuanza kuandika kitabu? Pata nakala ya kitabu cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU. Nakala laini ni 5,000/- tu. Tuma fedha kwa namba ya simu 0755848391 jina ni GODIUS RWEYONGEZA.

Kitabu ni chanzo cha kipato ambacho unakitengeneza mara moja na kinaendelea kuwepo kwa miaka yote. Watu wanaendelea kununua  kile ulichoandika miaka kadhaa iliyopita.

Mfano ukiandika kitabu mwaka ujao wa 2023 na ukakimaliza na kuanza kukiuza. Kitabu hicho kitaendelea kuwafaa watu hata mwaka miaka kumi, ishirini, hamsini na zaidi.

Kuna mtu atanunua kitabu hichohicho ulichoandika mwaka 2023, atakinunua mwaka 2035. Kazi yako ya Mara moja tu, itakulipa maisha yako yote. Hiki ni chanzo kizuri cha kipato ambacho unapaswa kukitengeneza.

Cha kushangaza utasoma hapa na kutikisa kichwa bila kuchukua hatua ya kuanza kuandika kitabu.

Enewei,
Ngoja mimi nikuache

Ila matokeo yako ya kesho yanaathiriwa na uamuzi unaofanya sasa hivi. Na uamuzi unaofanya Sasa hivi Ni au upate kitabu cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU kwa shilingi 5,000/- au la uache!

Kwa uamuzi wowote ule utakaochukua, fahamu kuwa una madhara kwenye kesho yako. Sasa je, upo tayari kuiharibu kesho yako kwa sababu hutaki kuchukua hatua ya kupata KITABU hiki?

Changamka sasa. Lipia 5,000/-  upate kitabu Cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU, ili ujifunze namna ya kutengeneza mfereji wako mwingine wa kipato.

Katika ulimwengu wa leo unaweza kuandika kitabu na kukiuza kwa njia ya mtandao. Kwa hiyo, ukatoa kitabu kwa gharama ndogo. Kumbe tofauti na wengine wanavyofikiri kuchapa lazima uwe na fedha nyingi, bado kuna uwezekano wa wewe wa kuchapa na kuuza kitabu kwa njia ya mtandao.

3. Kozi
Kama kilivyo kitabu, kozi pia ukiiandaa inadumu kwa muda mrefu. Unaiandaa Mara moja ila inadumu kwa muda mrefu huku ikikuingizia kipato.

Labda unajiuliza Kati ya kitabu na kozi, niandae kipi? Nashauri uandae kitabu kwanza, Kisha uandae kozi.

Nazungumzia uwekezaji kwenye hisa, hatifungani na vipande. Huu ni uwekezaji muhimu sana ambao wewe rafiki yangu unapaswa kuhakikisha kwamba umeufanya.

4. Uwekezaji
Yees, na Mimi ninapozungumzia uwekezaji siongelei Mambo ya Bitcoin, sijui crypto currency au sijui nini?

Ni uwekezaji ambao ni uhakika kuwa unaweza kukuingizia kipato hata Kama umelala? Kama hujawahi kuingiza kipato ukiwa umelala, hakikisha unachukua uamuzi Tena leo, wa kuanza kuwekeza kwenye HISA, hatifungani na vipande.


5.  Biashara
Biashara chanzo kingine Cha kipato ambacho kwenye ulimwengu wa Sasa Ni CHANZO ambacho lazima uwe nacho. Hata kama umeajiriwa, bado unahitaji kuwa na biashara yako ambayo itakuwa unaiendesha kwa pembeni hata kama ni ndogo.

Sote tunajua kuwa mshahara huwa haubadiliki mara kwa mara. Lakini kipato kwenye biashara hakina ukomo. Unaweza kukuza kipato chako kadiri uwezavyo. Hivyo, nakushauri na wewe uhakikishe unakuwa na biashara yako. 

6. Kamisheni
Kamisheni ni kipato unachopata kutokana na mauzo ya vidhaa fulani ambayo siyo yako au kwa kuwaelekeza watu wanunue vidhaa fulani. Hii ni Aina ya kipato ambayo Unaweza kuifanyia kazi pia.

Mfano, mimi Sasa hivi nalipa kamisheni ya asilimia 40 pale unapomleta mteja akanunua Audiobooks au softcopy zangu. Kumbe mteja mfano akinunua Audiobook ya kitabu cha NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA, ambayo kwa Sasa naiuza 10,000/-

Wewe unapata 4000/-. Just kwa kumweleza mteja tu aje kununua kwangu na akanunua.

Kwa ambaye angependa tufanye kazi pamoja kwenye hili, hakikisha tunawasikia kwenye WhatsApp yangu leo.

BONYEZA HAPA 👇🏿 kuchati nami
https://wa.me/message/3PMZSAFONLHAP1

Karibu sana

7. Mrabaha
Mrabaha ni malipo unayopata kutokana na kazi ya sana au kazi ya kubunifu.

Wasanii wa muziki huwa wanalipwa mrabaha kwa kazi zao kutumiwa kwenye vyombo vya habari na maeneo mengine. Mchoraji pia anaweza kupata mrabaha kutokana na kazi yake ya kuchora.

Mwandishi anaweza kupata mrabaha pale kitabu/ kazi yake inapochapwa na kuuzwa. Na kampuni za uchapishaji.

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

Godius Rweyongeza ni mwandishi wa vitabu zaidi zaidi ya 20. Na ni mwendeshji wa mtandao wa Songambele. Amekuwa akiandika kwenye huu mtandao huu tangu mwaka 2016. Kitabu chake cha Kutoka Sifuri Mpaka Kileleni kimekuwa #1Best Seller kwa muda sasa kwenye mtandao wa GETVALUE

Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.

Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.

Mtandaoni, vitabu vyake unaweza kuvipata kupitia mtandao wa GETVALUE kwa KUBONYEZA HAPA


One response to “Baadhi Ya Vyanzo Vya Kipato Ambavyo Unaweza Kuwa Navyo”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X