Viashiria Vinne Vya Uhuru wa kweli. Kama hauna hivi vitu jua huna Uhuru..


Leo Ni tarehe 9 Disemba, ni siku uhuru hapa nchini Tanzania. Sikupanga kuandika chochote kuhusiana na uhuru, ila ngoja niandike haya machache kuhusiana na uhuru wako binafsi.

Watu wengi huwa wanachanganya kuwa kwa kuwa nchi iko huru Basi na wao wako huru. Siyo kweli, Kuna viashiria ambavyo vinaweza kuonesha kuwa wewe uko huru au hauko huru. Vifuatavyo Ni viashiria muhimu vinavyoonesha kuwa wewe uko huru.

Ukiona viashiria hivi vinakupiga chenga, basi pambana ili uweze kupata Uhuru wako

Kiashiria namba moja ni Uhuru wa kazi.
Uhuru wa kazi ni pale Ambapo unakuwa hulazimiki kufanya kazi ili uingize kipato. Lakini pia unakuwa unafanya kazi unayoipenda na siyo kufanya kazi unayolazimishwa kufanya. Labda nikuulize unaipenda kazi unayoifanya?

Uhuru wa kazi haumaanishi kwamba uwe mzembe. Mimi Ni mwumini mzuri Sana wa kufanya kazi kwa bidii. Mara zote na siku zote hakikisha unajituma kwenye Kazi, ila fanya kazi unayoipenda.

Kiashiria namba 2 ni Uhuru wa fedha

Wazungu huwa msemo unaosema fuck you money. F*ck you money ni kiwango Cha fedha ambacho ukiwa nacho hakuna mtu yeyote anaweza kukuzuzua. Hiki ni kiasi Cha pesa ambacho ukiwa nacho hata bosi wako akizingua unaweza kumwambia f*ck you!

Kwa kusema hivi simaanishi uanze kutoa matusi kwa watu, Ila hiki ni kiasi Cha fedha ambacho ukiwa nacho, kinakupa uhuru.

Watu wengi huko makazini hawana Uhuru wa kuongea. Wana hoja nzuri ila wanashindwa kuzitoa kwa sababu wanahofia zinaweza kukataliwa na hivyo wakafukuzwa kazi.

Muda mwingine bosi anazingua au anawalazimisha kufanya vitu kinyime na vile wanavyoamini, lakini bado wanafanya kwa sababu hawana fedha, maana wakimpinga hawama kazi, hivyo hawana hela.

Kama bado hujawa na kiasi cha pesa cha kukufikisha kwenye kiwango cha f*ck you money, jua bado unapaswa kuendelea kupambana ili upate uhuru wako, maana sasa hivi huna uhuru.

Kiashiria namba tatu ni uhuru wa muda. Yaani, kwamba unakuwa na Uhuru wa kupangilia ratiba zako. Una Uhuru wa kwenda popote bila kuathiriwa na kitu chochote.
Je, unao uhuru wa muda?

Kiashirikia namba nne Ni uwezo wa kuingiza fedha hata kama umelala.
Kama huwezi kuingiza fedha hata kama umelala jua bado hujawa na uhuru. Unapaswa kupambana kuhakikisha kwamba unaweza kuingiza fedha hata kama umelala. Inawezekanaje? Ndio inawezekana kupitia uwekezaji na kuwa biashara

Hakikisha umesoma kitabu changu cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE ili ujifunze mbinu za uwekezaji ambazo zitakusaidia wewe kuingiza fedha ukiwa umelala?

Je, ni Uhuru upi ambao hauna?
Hauna Uhuru wa kazi. Basi soma kitabu cha JINSI YA KUONGEZA THAMANI YAKO (softcopy 10,000/-)

Hauna Uhuru wa muda? Soma kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI (Hardcopy 12,000/-) na softcopy 7,000/-

Hauna Uhuru wa kazi? Soma kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO na NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA. Kila kitabu Ni 20,000/-

Hauna Uhuru wa fedha. Soma kitabu cha MAAJABU YA KUWEKA AKIBA na kitabu Cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE 20,000/-

Hivyo, ni vitabu muhimu ambavyo unapaswa kusoma kama unataka kupata Uhuru wa kweli.

Unapenda nikupe ofa siku ya leo ya Uhuru? Ndio inawezekana. Bonyeza hapa
Kisha andika OFA YA UHURU!

Nitakupa ofa ya kitabu unachotaka siku ya leo.

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

Godius Rweyongeza ni mwandishi wa vitabu zaidi zaidi ya 20. Na ni mwendeshji wa mtandao wa Songambele. Amekuwa akiandika kwenye huu mtandao huu tangu mwaka 2016. Kitabu chake cha Kutoka Sifuri Mpaka Kileleni kimekuwa #1Best Seller kwa muda sasa kwenye mtandao wa GETVALUE

Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.

Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.

Mtandaoni, vitabu vyake unaweza kuvipata kupitia mtandao wa GETVALUE kwa KUBONYEZA HAPAOne response to “Viashiria Vinne Vya Uhuru wa kweli. Kama hauna hivi vitu jua huna Uhuru..”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X