/
Mr. Beast ni moja ya watu maarufu sana kwenye mtandao wa youtube. Yeye alianzia chini kabisa kwenye ulimwengu wa youtube, hakuwa na umaarufu wowote kama huu alionao sasa hivi. alianza kurekodi video moja baada ya nyingine,. Nyingi hazikufanya vizuri, lakini jamaa hakukata tamaa aliendelea, baada ya miaka mingi ya kuweka kazi bila ya kukata tamaa, ndipo video zake zilikuja kutambulika na baada ya hapo umaarufu wake umekuwa unaongezeka kila siku na kila kukicha.
Sasa kuna siku aliulizwa, hivi una ushauri gani kuhusu watu ambao ndio kwanza wanaanza kuingia kwenye ulimwengu wa youtube. Alisema kwamba hawa wanapaswa kuendelea kuweka kazi. Yaani, wasitegemee kwamba wanaenda kupata matokeo makubwa kwa haraka na ndani ya siku moja. Hakuna kitu kama hicho. matokeo makubwa yatakuja kweli, ila yanahitaji kwanza muda. Lakini pia yanahitaji mtu uweke kazi.
Siyo mtu unarekodoi video moja na kuweka youtube huku ukitegemea kupata m atokeo na mafanikio makubwa ndani ya hiyo siku. Hakana kitu kama hicho, badala yake unapaswa kuwa na mwendelezo kwenye kile ambacho wewe mwenyewe unafanya, yaani, unapaswa kufanya kitu ulichochagua kila siku bila kuacha na kwa mwendelezo.
Kadiri ya Mr. Beast anasema kwa mtu ambaye anataka kutoboa kwenye ulimwengu wa youtube anapaswa kuwa walau amerekodi video za kuanzia mia moja. hapo sasa ndipo tunaweza kuanza kuongea kuhusu kupata wafuasi. Hapo siyo kwamba huyo mtu katoboa, ila ndio mnaweza kuanza kuongea.
Hee, Na anasema kwamba kwenye kila video ambayo utarekodi unapaswa kuendelea kuiboresha na kuifanya kuwa bora zaidi ya ile ya kwanza. Yaani, siyo unarekodi video nyingi lakini zinakuwa hazina ubora wowote. Hapana, badala yake ni kwamba hizi video unapaswa kuwa unaziongezea ubora kila unaporekodi.
Najua asilimia kubwa ya wasomaji wangu siyo watu wanaotengeneza maudhui ya youtube. Na wala siyo kwamba kwa makala hii basi nawataka waanze kurekodi maudhui kwa ajili ya kuweka youtube.
Bali nataka kila anayesoma ujumbe huu aondoke na kitu kimoja kikubwa. Na kitu hiki ni kwamba, kama unaanzia chini, unapaswa kuweka kazi kwenye kitu ambacho unafanya. siyo unafanya kitu hicho mara moja au mara mbili halafu huoni matokeo unaacha. ACHA utani aisee, endelea kuweka kazi mpaka kieleweke.
Na siyo unafanya kazi kwa maozea,bali kila mara unaboresha na kufanya kazi ambayo ni bora zaidi kuliko mwanzo.
Toa mazoea, fanya kazi tena kwa bidii sana. Tutaongea baadaye
Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.
Godius Rweyongeza ni mwandishi wa vitabu zaidi zaidi ya 20. Na ni mwendeshaji wa mtandao wa Songambele. Amekuwa akiandika kwenye huu mtandao huu tangu mwaka 2016. Kitabu chake cha Kutoka Sifuri Mpaka Kileleni kimekuwa #1Best Seller kwa muda sasa kwenye mtandao wa GETVALUE
Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.
Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.
Mtandaoni, vitabu vyake unaweza kuvipata kupitia mtandao wa GETVALUE kwa KUBONYEZA HAPA