Kama utashindwa kufanya vitu vyote ndani ya mwaka 2023, hakikisha kwamba haushindwi kufanyia kazi hiki kitu kimoja tu


Rafiki yangu, sasa hivi ndio kwanza moto wa mwaka 2023 unakolezwa. Kama bado hujaanza kufanyia kazi malengo yako, kuna nafasi kubwa kuwa unaweza usije ukakamilisha haya malengo yako kama niliyoveleza kwenye makala ya jana.

Siku ya leo ningependa kukwambia kuwa kama mwaka huu tutashindwa kufanyia kazi malengo yako na vitu vingine, basi hakikisha kwamba haushindwi walau kuanzisha biashara mwaka huu.

Kweli. Uanzishaji wa biashara ni moja ya hitaji la muhimu sana, muhimu mno ambalo unapaswa kulifanyia kazi ndani ya mwaka huu mpya wa 2023. Pengine kwa siku umekuwa unajipa sababu na kujiambia kwamba mwaka huu nitaanzisha biashara, ila umekuwa huanzishai hizo biashara.

Kitu kikubw aambacho ninataka kuhakikisha kwamba nimekwakwambia ndani ya huu mwaka mpya ni kuwa biashara ina faida nyingi sana ambazo pengine ulikuwa huzijui, au pengine umekuwa unazijua ila umekuwa unapuuzia. Au pengine siyo tu umekuwa unapuuzia, bali muda mwingine ni  uoga ambao umekuwa unakusumbua.

Ukiwa na biashara, uwezekano wa wewe kulipwa mara mbili mpaka mara tatu au hata mara kumi zaidi ya unavyolipwa sasa hivi upo. Unaweza kulipwa zaidi ya unavyolipwa sasa hivi, endapo utakuwa na biashara kuliko pale ambapo unakuwa hauna biashara kabisa.

Kama umeajiriwa utakubaliana na mimi kuwa mshahara wako huwa una ukomo. Yaani, hata ufanyeje kazi, mshahara wako hauwezi kuongezeka.

Ila kwenye bisahra hali ni tofauti. Kadiri ambavyo unakuwa unaongeza juhudi ndivyo unakuwa unaongeza nafasi yako ya kufanya vizuri zaidi,

Hivyo basi, rafiki yangu kama kuna kitu ambacho unapaswa kufanya ndani ya mwaka huu wa 2023 ni kuhakikisha kwamba umefungua biashara. Rafiki yangu, uwanja sasa upo wazi kwa ajili yako kufanya makubwa ndani ya huu mwaka wa kipekee wa 2023. Hakikisha kwamba mwaka huu haupiti bila ya wewe kuhakikisha umefungua biashara. Kila la kheri

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.

Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X