Kitu kimoja ambacho hupaswi kuacha kufanya hata kama una nguvu ya pesa


umeshapata nakakla zako? Wasiliana na 0755848391 sasa kupata nakala zako. kila nakala bei yake ni 20,000/-
umeshapata nakakla zako? Wasiliana na 0755848391 sasa kupata nakala zako. kila nakala bei yake ni 20,000/-

Rafiki yangu mpendwa, ila shaka unaendela vizuri. Kwa upande mwingine mimi nipo vizuri kabisa. leo nataka tujadiliane kwa pamoja kuhusiana na kitu kimoja ambacho hupaswi kuacha kufanya hata kama una nguvu ya pesa. na kitu hiki ni kujadiliana muuzaji kuhusiana na bei anayokuuzia bidhaa.

Yaani, kiufupi ni kwamba mtu akitaka kukuuzia kitu kwa bei fulani, mara zote jadiliana naye ili uone namna ambavyo anawez akukupunguzia kiasi fulani kwenye hicho kiasi ambacho amekwambia.

Hiki kitu unapaswa kukifanya bila kujali una fedha nyingi kiasi gani.

Mara nyingi mfano mtu akikwambia kwamba anauza bidhaa au kitu fulani kwa 20,000/-. Wewe anza kujadiliana naye kwa kumwambia kwamba una kiasi pungufu, pengine nusu yake tu. komaa hapohapo, na ikiwezekana ongeza kiasi kidogo tu.

Mwisho wa siku utajikuta kwamba unaweza kupata hiyo bidhaa kwa bei nzuri sana.

SIyo kwamba ukifanya hivi ni kiashiria cha umasikini, bali  hiki kitu kinafahamika kama negoatiaon. Na negotiation ni mojawapo ya ujuzi muhimu sana ambao unauhitaji, na unakufaa sana, na utakusogeza mbali sana kimaisha.

Rafiki yangu, huu ujuzi hakikisha kwamba unakuwa nao kwa vyovyote vile. Na utumie popote pale unapokuwa bila ya kurudi nyuma.

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.

Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X