Moja ya dhana ambayo watu wengi tumekuwa hatujifunzi ni kuwa vitu ambavyo ni bora ndivyo ambavyo huwa vinapendwa. Hakuna mtu huwa anapenda kukaa karibu na vitu dhaifu, vitu ambavyo siyo vizuri na vitu ambavyo havivutii.
Ili uweze kunielewa vizuri kwenye hili, nitatolea mfano ambao unaweza kukuudhi kidogo. Hivi eti kwa mfano, unaweza kuchukua chakula chako kizuuuri ambacho umekipika na kikapikika na kwenda kula kwenye dampo? Ji bu lipo wazi kabisa, huwezi kufanya hivyo, kwa nini kwa sababu dampo siyo sehemu bora ambapo unaweza kula chakula chako hicho kitamu ambacho umedhamiria kula.
Hivyo hivyo, kwenye maisha ya kawaida, hakuna mtu ambaye anapenda kujihusisha na vitu vibaya. Na hata mzazi anapokuwa analea watoto wake atawaepusha na watoto wengine ambao wana tabia mbaya.
Lengo la mimi kukuandikia haya yote ni kukujulisha kuwa unapaswa kuwa bora kwenye kile unachofanya. Yaani, kwamba unapaswa kujiwekea viwango vya daraja la kwanza. Viwango vikubwa ambavyo utakuwa unavifanyia kazi na kuvifikia
Ubora wa wewe kujiwekea hivi viwango ni kwamba utavutia kwako watu wengine wa viwango vikubwa pia. Chuma kinanoa chuma. Na vitu vya aina moja mara nyingi huwa vina tabia ya kukaa pamoja.
Hivyo kama viwango vyako ni dhaifu, utajikuta kwamba unapata marafiki na watu ambao pia wana viwango dhaifu. Hiki kitu kitapelekea wewe kuishi maisha ambayo ni dhaifu pia . Sasa mwaka 2023 azimio lako linapaswa kuwa ni moja tu. unapaswa kuazimia kwamba mwaka 2023, ni mwaka wangu wa kufanya kazi zangu kwa viwango vya juu.
Hiki kitu kitakufanya uvutie kwako watu wngine wenye viwango vya juu pia.
Kama unaajiri, hakikisha kwamba unaajiri watu wa viwango vya juu.
Marafiki wako wawe marafii ambao wana viwango vya juu pia.
Rafiki yangu, huu ni mwaka wako ila tu siyo kwamba uishie kusema kwamba huu ni mwaka wangu kwa maneno, bali matendo yako yanapaswa kudhihirisha hilo.
Ukiwa bora watu hawawezi kukupuuza.
Asante sana
Kupata makala zaidi kutoka kwangu, hakikisha kwamba umejaza taarifa zako hapa
Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.
Godius Rweyongeza ni mwandishi wa vitabu zaidi zaidi ya 20. Na ni mwendeshaji wa mtandao wa Songambele. Amekuwa akiandika kwenye huu mtandao huu tangu mwaka 2016. Kitabu chake cha Kutoka Sifuri Mpaka Kileleni kimekuwa #1Best Seller kwa muda sasa kwenye mtandao wa GETVALUE
Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.
Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.
Mtandaoni, vitabu vyake unaweza kuvipata kupitia mtandao wa GETVALUE kwa KUBONYEZA HAPA