Viashiria vitano kuwa umeuanza mwaka mpya kwa kishindo


Rafiki yangu, naomba nichukue nafasi hii kuhakikisha kwamba nakutakia kheri ya mwaka mpya 2023. Kheri ya mwaka mpya rafiki yangu.

Mwaka huu naamini, utakuwa ni mwaka wako wa kipeke na mwaka wako wa kufanya makubwa. mwaka huu nina hakika ni mwaka ambao hautaremb  mwandiko. Na njia bora ya wewe kutoremba mwandiko ni kuhakikisha kwamba unaanza sasa hivi kufanyia kazi malengo yako bila ya kuchelewa. kwenye makala ya leo, ningepend akuingia kwa undani zaidi na kukueleza viashiria vitano vinavyoonesha kwamba kweli mwaka huu 2023 umeuanza kwa kishindo kikubwa kabisa.

Kiashiria cha kwanza ni kuweka malengo.

Kama tayari umeshaweka malengo. Basi hicho ni kiashiria cha kwanza kabisa kwamba mwaka huu umeuanza kwa kishindo kikubwa.

Watu ambao huwa wanaweka malengo ni wachache sana. tafiti zinaonesha kwamba asilimia tatu tu ya watu ndio huwa wanakuwa na malengo. Yaani, malengo ambayo ni SMART. Unajua malengo SMART ni malengo gani.

Neno SMART ni neno la kiingereza ambalo linasimama kwa ajili ya vitu vifuatavyo

  • S=Specific. Yaani, kwamba lengo lako ni lengo ambalo linaeleweka. Yaani, unapoweka lengo, wewe mwenyewe unapaswa kuelewa ni kitu gani unataka. Kinachowakwamisha watu wengi kikiwa kitu cha kwanza ni kuwa wenyewe huwa hawajui ni kitu gani ambacho wao wanataka.

Lengo lako linapaswa kueleza kwa uhakika hasa ni kitu gani ambacho unataka, mpaka rangi ya hicho kitu.

Lengo lako linapaswa kuwa linaeleweka kiasi kwamba akilisoma mtoto wa miaka sita, anapaswa kulielewa na kuweza kumweleza mtoto mwenzake wa miaka sita akaelewa.

  • M= Measurable. Lengo lako linapaswa kuwa linapimika. Ninaposema kwamba lengo linapimika nnamaanisha kwamba unaweza kupima na kuona kama unaelekea kwenye lengo lako au la!

Mwishoni mwa mwaka jana, nilikuwa nikiwasiliana na rafiki zangu wengi, huku nikiwauliza ni nini malengo yao makubwa ndani ya mwaka 2023? Mmoja aliniambia kwamba lengo langu ni kufanya zaidi. Kufanya zaidi maana yake nini?

Kufanya zaidi siyo lengo ambalo linapimika. Kama mwaka jana ulikuwa unakimbia mita 100. Mwaka huu ukikimbia mita 101 si utakuwa umefanya zaidi?

Kama mwaka jana ulikuwa huweki akiba, mwaka huu ukianza kuweka shilingi mia moja si utakuwa umefanya zaidi. lengo lako linapaswa kuwa linapimika.

Kwa mwaka huu wote ninaenda kuweka akiba ya shilingi laki mbili kila siku. Hilo ni lengo linapimika.

Kwa mwaka huu wote ninanenda kuwa naandika makala yenye maneno 1500 kila siku. Hili ni lengo jingine ambalo linapimika.

Kwa mwaka huu wote ninaenda kuwa naongea na wateja hamsini kila siku kwa simu. Hili ni lengo jingine ambalo linapimika.

Siku ambayo unafikia lengo lako unajua. Na siku ambayo unakuwa hujafikia lengo unajua.

Ila ukisema niteboresha biashara yangu. Sasa unaenda kuwa unaboresha nini kwenye biashara yako? Ukiongeza hata mfuko wa pipi mmoja si utasema umeboresha?

Ila ukisema kwamba biashra yangu ina mtaji wa milioni 70. Mwaka huu, ninakuza mtaji wangu mpaka milioni 200 hapo sasa ndio unakuwa umeweka lengo linalopimika? Sijui unanielewa?

  • A= attainable. Moja ya kitu ambacho pengine hukijui ni kwamba watu wengi huwa wanaweka malengo makubwa sanasana kwa mwaka mmoja huku wakiweka malengo madogo ya miaka mingi ijayo. Mtu anataka akamilishe na kufanikisha kila kitu masiahani mwake ndani ya mwaka mmoja. Rafiki yangu, ninachotaka kukwambia ni kwamba, malengo yako ya mwaka mmoja yawe makubwa na ambayo yatakusukuma kufanya vitu zaidi ya vile ulivyokuwa umezoea.
  • R=Relevant., hapa maana yake malengo yako makubwa yanapaswa kuendana na ndoto zako kubwa za mbeleni au kazi au  biashara. Usiweke tu malengo ilimradi umeweka malengo
  • T= Lengo lako pia linapaswa kuwekewa ukomo wa muda. Yaani, lini unataka lengo liwe limekamika. Yaani, hakikisha umeweka lengo lako katika namna ambayo ineonesha lini ungependa kuwa umefikia lengo lako.

Andika kufikia tarehe………..ninamiliki…….

Kama umeuanza mwaka wako kwa kuhakikisha kwamba una malengo ambayo ni SMART, hicho ni kiashiria kuwa umeauanza mwaka wako kwa ushindi

Kishiria cha pili kuw umeuanza mwka wako kwa ushindi ni kuwa umeshaanza kufanyia kazi malengo yako. Rafki yangu, ikumbukwe kwamba kuweka malengo ni kitu kimoja ila kufanyia kazi malengo ni kitu kingine kabisa. hivyo, basi kama unataka kujua kama kweli umeuanza mwaka wako kwa ushindi ni mpaka pale utapokuwa umeweza kuanza kufanyia kazi malengo yako.

Kuweka malengo ni kitu kimoja, ila kufanyia kazi malengo ni kitu kingine.

Na watu wengi huwa wanaweka malengo, ila wachache sana ndio huwa wanachukua hatua ya kuhakikisha kwamnba wamefanyia kazi malengo yao na kuyaleta kwenye uhalisia. Rafiki yangu, usiwe mtu ambaye anaweka malengo tu bila ya kuyafanyia kazi. weka malengo kisha anza kuyafanyia kazi.

Kama ulikuwa hujaanza kufanyia kazi malengo yako anza leo hii. na siyo lazima ufanye kitu kikubwa sana ndani ya siku moja.

Unaweza kuanza kidogokidogo kwa kuchukua hatua ndogondogo ambazo utaanza kufanyia kazi. ndio maana nakushauri sana uweze kusoma kitabu changu cha NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA.

Hiki kitabu kitakufaa sana rafiki yangu

Hiki ni kitabu ambacho kimesaidia wengi ndani ya mwaka 2022. Kitakusaidia na wewe kufanya makubwa ndani ya mwaka 2023.

Pata nakala ya kitabu hiki leo hii.

Gharama ya kitabu ni 20,000/-

Kama upo nje ya mkoa wa Morogoro, utaongeza gharama ya usafiri ili kutumiwa kitabu.

Kiashiria cha tatu kuwa umeuanza mwaka wako kwa ushindi ni  kama unafuatilia maisha yako zaidi ya unavyofuatilia maisha ya watu wengine.

Kuna watu huwa wanapenda kufuatilia maisha ya watu wengine kuliko wanavyokuwa wanafuatilia maisha ya watu wengine. Unawakuta mtandao ni wakiwa wanafuatilia labda maisha ya msanii fulani au mtu fulani. Lakini wanachosahau ni kuwa wao wenyewe wana mambo mengi ya kufuatilia juu yao wenyewe. Hivyo, basi ili mwaka wako uweze kuwa wenye baraka n yingi na mafanikio makubwa unapaswa kuhakikisha kwamba unajifuatilia wewe mwenyewe kuliko ambaavyo unamfuatilia mtu mwingine.

Jenga utaratibu wa kujifuajtilia wewe mwenyewe ndani ya huu mwaka kuliko ambavyo unamfuatilia mtu mwingine.

Kila siku asubuhi weka orodha ya vitu ambavyo unaenda kufanya ndani ya siku husika.

Kisha baadaye jioni, hakikisha kwamba unajifanyia tathmini kuona ni kwa namna gani umeweza kufanyia kazi orodha ya vitu ambavyo ulipanga asubuhi. Kwa kufanya hivyo, utaona wapi umeweza kufanya vizuri na wapi hukuweza kuafanya vizuri, lakini hilo litakupa picha na kukuonesha ni wapi ambapo unapaswa kubadili kwenye maisha yako ili kufanya maisha yako kuwa bora sana.

Kiashiria cha nne kuwa umeuanza mwaka wako kwa kishindo ni kujikukumbusha malengo yako kwa kuyasoma walau mara mbili kila siku.

Unapoweka malengo, unapaswa kujenga utaratibu wa kuyarudia kuyasoma pia kila mara.

Unafanya hivyo kwa lengo la kuifanya akili yako, ijenge ione kwamba inaweza kufikia lengo lako na linawezekana vizuri sana bila ya shida yoyote ile.

Kiashiria cha tano ni kuwa tayari umeshaanza kujifunza kitu kuhusiana na lengo lako. Rafiki yangu, kama kuna kitu muhimu sana ambacho haupaswi kusahau ni kwamba usisahau kujifunza na kujiendeleza zaidi kuhusuaiana na lengo lako.

Kwa mfano, una lengo la kuwekeza kwenye hisa mwaka huu. unapaswa kuanza mara moja kujieleimisha kuhusiana na elimu ya hisa. Na kwa kuanzia unaweza kupata kitabu changu cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE ambacho kitakusaidia sana kwenye hili.

Au pengine una lengo la kuanzisha kilimo cha samaki. Hapa unahitaji pia kuhakikisha kwamba unaaanzakujiendeleza kielimu kuhusiana na elimu ya kilimo na ufugani wa samaki.

Haya ni mambo machache sana ambayo unapaswa kuhakikisha kwamba unayafanyia kazi na kuyuaeta kwenye uhalisia.

Kujifunza ni jambo ambalo haliepukiki hasa kama umeweka malengo makubwa na unataka kufakika mbali ndani ya mwaka 2023. Rafiki yangu, malengo makubwa yanahitaji ujifunze na ufanyie kazi kile unachojifunza.

Kiashiria cha ziada, umebadilli tabia zako. Yaani, kuna tabia ambazo najua unazo. Na tabia hizo haziwezi kukusaidia wewe kufanikisha malengo yako. Rafiki yangu, kama unataka kuhakikisha kwamba umeweza kufanikisha malengo yako ndani ya mwaka 2023, basi hakikisha kwamba unabadili tabia zako. niambie tabia zako, nami nitakwambia kama utawza kufanikisha malengo yako au la!

Una lengo la kupunguza uzito, ila bado hujaacha tabia yako ya kula hovvyohovyo? Una lengo la kuweka akiba ila bado unahonga? Una lengo la kuongeza kisomo ila bado unazembea kusoma.

Una lengo la kuanzisha biashara ila hata hujifunzi kuhusiana na biashara?

Rafiki yangu,  hizi tabia unapaswa kuhakikisha kwamba unaziiishi ndani ya mwaka 2023 ili kupiga hatua. Na kama unavyoona. Wengi walitamanani kusikia nikiwambia kwamba kama ulikseha usiku kuusubiri mwaka mpya, basi umeuanza mwaka wako kwa ushindi.

Au wengine walitaka niwaambie kwamba kama umeuanza mwaka wako kwa kuchati sana hapo umeuanza kwa ushindi. Kiufupi utakuwa umeuanza mwaka wako kwa ushindi kama umefanyia hivyo vitu vitano ambavyo nimekwambia kwenye makala ya leo.

Bila kuongeza la ziada, mimi naishia hapo

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.

Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X