Hii Ndio Njia Pekee Ya Kuhakikisha Kwamba Unapata Upendeleo Popote Pale Utakapoenda


Hii ndio njia pekee ya kuhakikisha kwamba unapata upendeleo popote pale utakapoenda

Sisi binadamu huwa tunapenda sana kuonekana mbele ya watu kama watu wa thamani sana. Tunataka tukikuta sehemu fulani tusianze kupanga foleni, badala yake tupite kwenye hiyo foleni na kuhudumiwa.

Tunapenda tukiwa kazini tupandishwe vyeo.

Tunapenda tukiwa kwenye foleni, gari letu lipishwe lipite haraka ili tuwahi kufika.

Sasa siku ya leo nataka nikuoneshe namna ambavyo unaweza kupata upendeleo sehemu yoyote ile utakapokuwa.

Ndio namaanisha hilo.

Na njia hii ya kupata upendeleo ni wewe kufanya kazi kwa bidii. Rafiki kufanya kazi kwa bidii kutakufanya upendelewe sehemu yoyote ile utakapoenda. Hakuna mwajiri ambaye huwa anapenda kukaa na wafanyakazi wazembe. Ila ukifanya kazi kwa bidii, mwajiri wako atakupendelea.

Hakuna mtu ambaye yuko makini ambaye anapenda kukaa na watu wanazembea kwenye kazi zao.

Hivyo basi, kuanzia leo hii, uamuzi wako uwe mmoja tu, kufanya kazi kwa bidii.

Kufanya kazi kwa bidii kunaweza kukufanya ukae meza moja na wafalme. Na kwa jinsi hiyo utakuwa umesababisha watu wakupendelee.

Kufanya kazi kwa bidii kuutakufanya ulipwe zaidi. hivyo, kwa jinsi hiyo, utakuwa umejipendelea.

Kumbe basi kufanya kazi kwa bidii ni kujipendelea mwenyewe. Maana kabla mtu hajaona juhudi zako na kuzipia zawadi atahitaji kuona utendaji kazi wako.

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.

Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X