Rafiki yangu, kama kuna kitu ambacho utasikia kutoka kwangu amra kwa mara ni kuhusu kuongeza thamani yako.
Nasisitiza hili kwa sababu watu wengi wangependa kupata mafanikio. Ila sasa tatizo ni kwamba hawajui ni kwa namna gani wanaweza kuwa na mafanikio. Moja ya kitu ambacho kinaweza kuwafanya watu wawe wenye mafanikio makubwa ni kwa kuhakikisha kwamba unaongeza thamani yako.
Kuna vitu vingi vya kuangalia tunapokuwa tunazungumzia thamani yako kama wewe. Na moja ya kitu hiki ni kanuni hii rahisi sana ya uchumi. Kanuni ya upatikanaji na uahaba.
Kwenye uchumi kitu chochote ambacho kinapatikana kwa wingi thamani yake huwa inakuwa chini sana ukilinganisha na kitu ambacho ni haba kukipata.
Maji yanapatikana kila sehemu, hivyo thamani ya maji ndogo ukilinganisha na thamani ya dhahabu, ambayo inapatikana sehemu chache.
Sasa wewe kama wewe jukumu lako ni kuhakikisha kwamba unakuwa na kitu ambacho hakuna mtu mwenye nacho. Kadiri ambavyo unnakuwa na kitu ambacho kila mtu anacho, maana yake unakuwa na kitu ambacho hakuna mtu yeyote yule anaweza kufanya. Hiki kitu kinakufanya wewe uwe na thamani kidogo sana. ila ukiwa na ujuzi au kitu ambacho watu wengine hawana, maana yake unakuwa na thamani ambayo watu wngine hawana. Hivyo, thamani yako itakuwa kubwa sana
Huwa napenda sana kutolea mfano wa wanachuo ambao wanasoma kwenye darasa moja na kufundishwa na profesa yuleyule. Ni kitu gani kinapaswa kumfanya mwanafunzi mmoja kulipwa mshahara mkubwa kuliko mwingine,k ni kitu gania ambacho kinapaswa kumfanya mhitimu mmoja kulipwa zaidi ya mwingine.
Kitu kimoja tu kinaweza kufanya hili, na kitu hiki siyo kingine bali ni kuwa mtu mwenye thamani. Hapa kuna vitu vitano ambavyo vinaweza kukuongezea thamani yako kwa harakaharaka.
Kwanza kuwa na ujuzi ambao wengine hawana au hawawezi kuufanya kama ambavyo wewe mwenyewe unaufanya. Yaani, usiwe na ujuzi wa kawaida ambao kila mtu anao, kuwa na ujuzi wa kipekee ambao hakuna mtu mwingine mwenye nao. Na hili linawezekana kama utakuwa tayari kujifunza kwa kina kuhusiana na huo ujuzi na kuhakikisha kwamba unaenda hatua za ziada kuliko wengine ambao wamekuzunguka. Haitoshi tu kujifunza na kuujua ujuzi husika, bali kuufanya kwa vitendo ndio kutakufanya wewe kuwa mtu mwenye thamani kubwa zaidii.
Nataka leo hii ujiulize, hivi mimi nina ujuzi gani ambao watu wngine hawana, ambapu unaweza kunifanya mimi niweze kulipwa zaidi ya ninavyolipwa sasa hivi. Ukishaugundua huo ujuzi, basi hakikisha kwamba unaufanyia kazi li uweze kuwa mtu adimu, mtu ambaye anaweza kulipwa kutokana na thamani yako ambayo unazalisha sokoni.
Pili ni kufanya kazi kwa bidii, hiki ni kitu kingine ambacho kinaenda kukufanya wewe uwe mtu mwenye thamani kubwa sana. najua watu wengine sana wamekuwa wanasema kwamba ooh, unajua unapaswa kufanya kazi kwa akili (work smart) badala ya kufanya kazi kwa bidii. Wewe ufanya vyote viwili. Yaani, fanya kazi kwa akili, na wakati huoho fanya kazi bidii. Jitume sana kwenye kazi zako kiasi kwamba asiwepo mtu mwingine ambaye anajituma na kufanya jkazi kwa bidii kama wewe.
Inawezekana watu wengine wakawa wamekuzidi kipaji, inawezekana wengine wakawa wamekuzidi konekisheni, inawezekana wengine wakakuzidi fedha, ila hakikisha kwamba watu hawakuzidi kwenye kufanya kazi kwa bidii. Kubali watu wakuite majina yoyote mabaya yale hapa duniani, ila usikubali kuitwa mzembe. Kwa vyovyote vile hakikisha kwamba unakuwa mchapakazi wa kweli. Mchapakazi aliyejitoa haswa kuhakikisha kwamba anachapakazi, siyo tu kwa kuongea bali kwa matendo.
Tatu, ni kujifunza.
Hiki ni kitu kingine ambacho unapaswa kukifanyia kazi, hiki kitu kitakufanya uweze kuongeza thamani yako kwa viwango vikubwa sana. na kiwango cha chini kwako ni walau kusoma kitabu kimoja kila wiki. Hiki kitu kitakufanya wewe uweze kuwa mtu ambaye anafanya makubwa sana kuliko watu wengine wanavyokuwa wanatazamia. Utaweza kufanya yale ambayo watu wengine wanaona kama hayawezekani vile ila kwako utakuwa unaona kwamba inawezekana na inawezekana kwelikweli.
Nne, mezwa na kile unachofanya
Kwenye ulimwengu wa leo, ambao ambayo hata siyo ya maana yanachukua sana muda wetu. Unaweza kukuta kwamba mtu anaamka asubuhi na kitu cha kwanza mbacho anafanya ni kuingi amtandaoni ili kuangali ni kitu gani ambacho kinaendelea kwenye hiyo mitandao, na tena kabisa anajiambia kwabma ataingia kidogo tu,ila mwisho wa iku huyu mtu anajikuta katumia saa moja, mawili lau hata matatu.
Na hata muda mwingine wa kazi unakuta kwamba mtu anafanya kazi huku akiwa anachughulia kwenye hii mitandao ya kijamii.
Rafiki yangu unapaswa kumezwa na kile unachofanya, unpaswa kumezwa na hicho unachofanya kiasi kwamba unapokuw aunafanya hicho kitu iwe kama vile duniani hakuna kitu kingine zaidi ya hicho tu. Linaweza kuwa ni zoezi gumu mwanzoni, ila ni zoezi ambalo unapasw akujizoeza kulifanyia kazi.
Kwa kuanzia kuanzia leo hii, muda wa kazi, hakikisha kwamba unazima simu au la unaiweka mbali na eneo ambapo unafanyia kazi au la unaiweka katika mfumo ambapo watu wakipiga hawawezi kukupata. Hiki kitu kitakusaidia sana rafiki yangu kuweza kufanya kazi haswa pale inapokuwa inatakiwa kazi.
Tano, usifanye vitu kwa ukawaida. Badala yake weka kazi na uhakikishe kwamba unafanya kazi kwa namna ambayo ni ya tofauti na wengine. Hakikisha kwamba kazi yoyote ile ambayo imebeab jina lako basi inakuwa ni kazi bora sana kuwahi kutokea.
SOMA ZAIDI: Haya ni mambo ya msingi ambayo unaenda kujifunza kutoka kwenye kitabu cha jinsi ya kuongeza thamani yako
Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.
Godius Rweyongeza ni mwandishi wa vitabu zaidi zaidi ya 20. Na ni mwendeshaji wa mtandao wa Songambele. Amekuwa akiandika kwenye huu mtandao huu tangu mwaka 2016. Kitabu chake cha Kutoka Sifuri Mpaka Kileleni kimekuwa #1Best Seller kwa muda sasa kwenye mtandao wa GETVALUE
Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.
Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.
Mtandaoni, vitabu vyake unaweza kuvipata kupitia mtandao wa GETVALUE kwa KUBONYEZA HAPA