KITABU: JINSI YA KUONGEZA THAMANI YAKO: Njia Za Uhakika Zitakazokufanya Ulipwe Mara Kumi Zaidi ya Unavyolipwa Sasa


Sisi binadamu ni viumbe ambao tunapenda kuthaminiwa, kuheshimiwa na tunataka watu watambue uwepo wetu. Ukienda kwenye mkutano au kwenye sherehe fulani, wakiwatambulisha watu wote halafu wakakuacha wewe bila kukutambulisha, ni wazi utajisikia vibaya na pengine utasema kwamba wamekudharau.

Au ukienda sehemu watu na wote wakapewa vinywaji na chakula, halafu ukasahaulika wewe, ni wazi kuwa wewe mwenyewe utang’aka. Ila upande mwingine wa shilingi, ni kuwa ukienda sehemu watu wakatambua uwepo wako, wakakupa heshima zote. kama ni vinywaji wewe ukapewa kwa kipaumbele, utafahamu kuwa hawa watu wamenithamini, na pengine utataka na wengine wajue hilo.

Thamani ni kitu muhimu sana ambacho unahitaji kuwa nacho.

Kwenye kurasa za kitabu hiki unaenda kujifunza namna ambavyo unaweza kuongeza thamani yako zaidi.

Mbinu unazoenda kujifunza kwenye kitabu hiki zitakusaidia kuongeza thamani yako mara mbili mpaka mara kumi zaidi.

Naomba nieleweke kwamba ninaposema kuongeza thamani yako simaanishi kwamba, utaongeza thamani kwa kuwa mrembo zaidi. Wala simaanishi kwamba utaongeza thamani kwa kupata followers zaidi mtandaoni, na wala simaanishi kwamba unaongeza thamani yako kwa kuwa mrefu, mfupi, mtu wa miraba minne, mweusi, mweupe au maji ya kunde! Endapo hayo yatatokea, basi tutashukuru pia kuwa yametokea.

Bali haswa namaanisha kuongeza thamani yako kwa kulipwa zaidi. Ukitumia mbinu zilizoainishwa kwenye hiki kitabu, utakuwa na uwezo wa kulipwa mara mbili mpaka mara kumi zaidi. Hivi kwa mfano, unaanzaje kuacha kutumia mbinu hizi ili uweze kulipwa zaidi ya unavyolipwa sasa hivi?

Gharama ya kitabu hiki ni 20,000/- kupata nakala yako. Tafadhali wasiliana nami kwa 0755848391 ili niweze kukutumia nakala yako


One response to “KITABU: JINSI YA KUONGEZA THAMANI YAKO: Njia Za Uhakika Zitakazokufanya Ulipwe Mara Kumi Zaidi ya Unavyolipwa Sasa”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X