Rafiki yangu, najua kuna vitu vingi ambavyo unahitaji kufahamu. Ila siyo kila kitu unachokifahamu kina manufaa chanya kwako. kwa mfano unaweza kufahamu kuwa kuna ajali fulani sehemu fulani, ila siyo kwamba hiyo ajali ina manufaa yoyote kwako. au kwa wewe kufahamu kuwa kuna vita sehemu fulani, hilo kwa kupande wako siyo kwamba linakuwa na matokeo chanya ambayo unaweza kuyatumia.
Ila kwa upande mwingine kuna vitu ambavyo ni muhimu kwako kuvifahamu na baada ya kuvifahamu unapaswa kuhakikisha kwamba umetumia maarifa na kila kitu ulichokipata kwa manufaa zaidi. moja ya kitu ambacho wewe unahitaji kuhakikisha kwamba umekifahamu kwa undani zaidi ni THAMANI YAKO.
Thamani ni kitu cha muhimu sana ambacho unahitaji kuhaikisha kwamba umekifanyia kazi, tena unahitaji kuhakikish kwamba unakifanyia kazi sasa hivi rafiki yangu
Ukijua thamani yako, utaokoa mengi sana rafiki yangu.
Thamani yako inakusaidia wewe kupangilia muda na kazi zako ambazo unafanya. hii ndiyo kusema kwamba badala ya kufanya vitu hovyohovyo, unakuwa unafanya vitu kwa ustaarabu na kwa utaratibu mzuri ambao umeupangilia. Kitu ambacho hujakipangilia hukifanyi.
Pili kujua thamani yako kunakusaidia kujua vitu vya kukubali kwenye maisha yako na vitu ambavyo unapaswa kukataa. Siyo kila kitu unaweza kukifanya, kuna baadhi ya vitu unaweza kuvikubali na kuamua kuvifanya kwenye maisha yako, ila kuna baadhi ya vitu unapaswa kuacha kuvifanya ili uwekeze nguvu zako na muda wako kwenye kukuza thamani yako zaidi.
Hii inakusaidia kuwekeza muda wako kwenye sehemu zenye nguvu na kuachana na sehemu ambazo hazina nguvu kwa upande wako.
Rafiki yangu kama kuna sehemu ambapo wewe unapaswa kuwekeza muda wako na nguvu zako basi ni kwenye thamani yako. Hakikisha kwamba unaijua thamani yako kw aundani.
Nimeandaa kitabu kizuri kwa ajili yako kitakachokusaidia wewe kwenye hili. Kitabu kinaitwa JINSI YA KUONGEZA THAMANI YAKO.
Karibu sana uweze kujipatia nakala yako siku ya leo.
Kupata nakala tuwasiliane kwa 0684408755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA