Njia bora ya kumbadili mtu yeyote


Rafiki yangu, watu wengi wamekuwa wanapenda mabadiliko. Wanapenda watu waliowazunguka kwenye maisha yao wabadilike na wafanye vitu kama ambavyo wao wanataka pia.

Nina njia moja ambayo itakupa uhakika wa kubadilika na kufanya chochote kile unachotaka kama ambavyo wewe mwenyewe unataka. Na njia hii ni wewe kuanza kubadilika. Yaani, kama kuna njia bora ya kuwabadili watu ni wewe kubadilika. Ukibadilika wewe basi watu wakinna namna ambavyo umekuwa unafanya na mwisho wa siku watakuwa tayari kuchukua hatua ili kuweza kufnaya kama unavyofanya.

Unataka kuwafanya watu wasome vitabu. Anza wewe kusoma vitabu

Unataka kuwafanya watu waweke akiba. Anza wewe kuweka akiba

Unataka kuwafanya watu wafanye kazi kwa bidii, anza wewe kufanya kazi kwa bidii.

Unataka kuwafanya wtu wawahi kazini, anza wewe kuwahi.

Chochote kile kizuri unachotaka watu wafanye, anza wewe kukifnaya.

Kila la kheri.

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.

Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X