Epuka hiki Kitu kama unataka kufanya makubwa


/

Rafiki yangu, najua unataka kufanya makubwa kwenye maisha yako. Hongera sana kwa kuwa na ndoto kubwa sana.
Ebu kwwanza, kabla sijakwambia kitu cha kuepuka kama unataka kufanya makubwa. Naomba kwanza uandike malengo yako na ndoto zako hizi kubwa chini. Ziandike kabisa, ili ujue ni kitu gani unataka kufanikisha kwenye maisha yako.

Hongera kwa kuweza kufanyia kazi hilo.
Sasa kwa kuwa una malengo na ndoto kubwa hivyo, kuna kitu kimoja ningependa ukifanyia kazi siku ya leo. Na kitu hiki siyo kingine bali ni kuhakikisha kwamba unajituma na unafanya vitu vya tofauti. Huwezi kuendelea kufanya vitu vilevile kila siku huku ukitegemea kupata matokeo ya tofauti.

Ni lazima uwe tayari kujisukuma kidogo, ni lazima uwe tayari kufanya mambo ya tofauti, ili uweze kupata matokeo ya tofauti ambayo hujawahi kuyapata.

Hiki ndicho kitu kikubwa sana ambacho ninataka kukwambia siku ya leo rafiki yangu.

Kifanyie kazi hiki, utanishukuru kesho.

Kila la kheri

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.

Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.

uNGEPENDA KUPATA HIVI VITABU, TWANGA 0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X