Rafiki yangu, umewahi kujiuliza ni kitu gani kinakukwamisha wewe kuweza kufanya makubwa. Kama kuna kitu kinakukwamisha wewe na watu wengine wengi, basi kitu hiki ni kufanya kazi kama vile una muda wote hapa duniani. Yaani, unaanza kufanya jukumu lako bila ya kuwa na lengo wala mwelekeo wowote. Kitu kinachokufanya ufanye jukumu hilo kwa muda mrefu sana kuliko unavyokuwa unatazamia.
Unaweza usijue hili. Kwa sababu kama hauna mpango, utaona uko sahihi kwa kile utakachokuwa unafanya. Ila nikuhakikishie kwamba ukiwa na mpango, rafiki yangu, mambo yako, utayafanya vizuri, kwa kujisukuma na kujituma zaidi.
Ninachotaka ufahamu ni kuwa kama unataka kuutumia muda wako vizuri na kwa manufaa makubwa sana, basi unapaswa kuwa na ukomo kwenye muda wako.
1. kuanzia unapoamka asubuhi, hakikisha kwamba unapangilia siku yako kwa kuweka majukumu yote utakayoyafanya ndani ya hiyo siku. Usikubali kuipitisha siku bila ya wewe kuwa na mpango ambao unaoufanyia kazi ndani ya hiyo siu
2. Muda ambao wewe unautumia kupangilia siku yako au wiki yao, siyo kwamba huo muda unakuwa unaupoteza. Hapana, badala yake huo muda unakuwa unautumia kwa manufaa makubwa. Hivyo, usije kusema kwamba nimepoteza muda kwa kupangilia siku yangu. Badala yake unakuwa umeokoa muda, maana muda ambao hapo baadaye ungekuja kuupoteza utauokoa kwa kufanya majukumu ya maana.
3. Ukishapangilia siku yako, kinachofuata ni wewe kufuata huo mpangilio wako ambao umeuweka kama ulivyo. Kufanya majukumu yako muda ambao unapaswa kuyafanya bila kuacha, kitu hiki kitakufanya uweze kuutumia muda wako kwa manufaa makubwa.
Asante sana, nikutakie siku njema rafiki yangu.
Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.
Godius Rweyongeza ni mwandishi wa vitabu zaidi zaidi ya 20. Na ni mwendeshaji wa mtandao wa Songambele. Amekuwa akiandika kwenye huu mtandao huu tangu mwaka 2016. Kitabu chake cha Kutoka Sifuri Mpaka Kileleni kimekuwa #1Best Seller kwa muda sasa kwenye mtandao wa GETVALUE
Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.
Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap. Mtandaoni, vitabu vyake unaweza kuvipata kupitia mtandao wa GETVALUE kwa KUBONYEZA HAPA