Rafiki yangu mpendwa, salaam. Leo ni siku njema sana. Kwenye andiko hili nataka tuongelee namna ambavyo UMEZALIWA KUTAWALA na jinsi unavyopaswa kufikiri katika namna ya KUTAWALA muda wote
Mtazamo wa uhaba (Scarcity mindsent)
Hii ni dhana ambayo watu wengi wanakuwa nayo. Hiki kitu kinawafanya wengi wafikiri kwamba RASILIMALI na vitu vingine vinapatikana Kwa uhaba hapa duniani. Ila ukweli ni kwamba RASILIMALI na mali nyingine hazipatikani Kwa uhaba wowote ule hapa duniani. Dunia ina utele wa fursa na utele wa RASILIMALI kiasi kwamba pale unapokuwa unafikiria kama RASILIMALI zimeisha ndio kwanza RASILIMALI nyingine zinakuwa Zinakuwa zinazidi kujitokeza
Mfano, tukiangalia upande wa nishati. Kuna kipindi watu walikuwa wanatumia nishati ya makaa ya mawe kwa ajili ya kuendesha shughuli mbalimbali za viwandani na majumbani. Watu wakawa na hofu kuwa makaa ya mawe yataisha na hivyo, dunia itashindwa kuendesha viwanda. Katika nyakati ambapo watu walikuwa wanafikiri kwamba makaa ya mawe yanaenda kuisha, zikagundulika nishati nyingine kama mafuta. Kadiri ambavyo kumekuwa na ongezeko la watu wanaotumia hii nishati, ndivyo ambavyo wengine walianza kuhisi kama hii nishati itaisha na hivyo watu kuikosa kwa ajili ya kuitumia kwenye uzalishaji na shughuli mbalimbali za viwandani na majumbani. Hata hivyo, kinachoonekana sasa hivi ni tofauti kabisa
Leo hii imegundulika kuna vyanzo vingi vya nishati kiasi kwamba mafuta siyo tishio Tena. Tunaweza kupata nishati ya umeme kutoka kwenye maji, upepo mpaka vinyesi. Huku nishati ya jua tu ikiwa na uwezo wa kutoa umeme wa kutosheleza kama itatumika vizuri . Na hasa katika nchi zetu za Afrika ambazo zinapata jua kwa muda mwingi wa mwaka kuliko nchi nyingine.
Kumbe mpaka hapo tunaona wazi kuwa nishati ya mafuta siyo TATIZO Tena. Na Wala hatuwezi kusema kuna uhaba wa nishati kwa sababu labda mafuta yamepungua. Tutasema Kuna uhaba wa nishati pale ambapo tutakuwa tunafikiri kuwa mafuta ndio nishati pekee hapa duniani
Pale ambapo tutakuwa kama mtu ambaye ameshika shoka na kila kitu kwake anakiona kama mti.
Sasa rafiki yangu, ninachotaka ujue ni kuwa dunia haina uhaba wa kitu chochote. Siyo fedha. Siyo kiwango Cha maarifa unachoweza kupata. Labda uhaba pekee uliopo ni ule ambao unaweza kuutengeneza wewe mwenyewe kwenye akili yako.
Kujua hili ni muhimu sana kwako kwa sababu itakusaidia wewe kuweza mara zote kuweka nguvu kwenye kuziangalia fursa na kuzitumia fursa vizuri ili uweze kufanikisha kile unachotaka. Hapa duniani unaweza kupata na kuwa unachotaka. Wewe rafiki yangu. Umezaliwa KUTAWALA. Na unaweza KUTAWALA. Kwenye sura hii nitakuonesha namna unavyoweza kutumia nguvu ya utawala iliyo ndani yako kwa manufaa.
Ninamaanisha nini ninaposema kwamba umezaliwa kutawala..
Watu wengi wanaposikia habari za kutawala basi kinachokuja kwenye fikra zao mara moja ni kuwa lazima uwe na cheo. Kwa hiyo, kuna mtu anaweza kusoma hapa habari za kwamba amezaliwa kutawala, kesho yake akaamka na kwenda na kuchukua fomu ili agombee na kuwa na cheo ili aanze kutaawala.
Kwanza naomba ifahamike kuwa kutawala siyo lazima uwe na cheo kuna tofauti kubwa kati ya kuwa na cheo na kuwa na kuwa kiongozi. Hivi ni vitu viwili tofauti. Asilimia kubwa ya watu tunaowafahamu kama viongozi, siyo viongozi ni watu wenye vyeo. Cheo ni dhamana ambayo unapewa kwa ajili ya kutumikia jambo fulani. Cheo huleta madaraka. Cheo kikiondoka na madaraka nayo huondoka. Hata hivyo, huhitaji kuwa na cheo ili kuwa kiongozi. Kama wewe ni mtu ambaye unapumua, basi ujue kuwa wewe ni kiongozi. Na uongozi unaanzia kwako wewe mwenyewe. Na kwenye mambo yako ambayo unayafanya kila siku.
Cheo kinakupa madaraka ya kuwasimamia watu ili watekeleze majukumu yao lakini ukiwa kiongozi unakuwa na uwezo wa kutekeleza majukumu yako hata bila ya kusimamiwa.
Mfano huhitaji kuwa na cheo ili kuweka malengo yako binafsi na kuyafanyia kazi. Najua watu wengi huwa wanalalamikia serikali kuwa haijafanya hiki na wala haijafanya kile. Lakini watu hao hao ukiwauliza malengo ambayo wanayo wanakuwa hawana hata malengo ambayo wanayafanyia kazi. Huhitaji kuwa na cheo ili uwe na malengo na uyafanyie kazi malengo yako. Huhitaji kuwa na cheo ili uwe na ndoto kubwa. Huhitaji kuwa na cheo ili ujitume kwenye kazi zako. Huhitaji kuwa na cheo ili ujifunze na kusoma kitabu. Huhitaji kuwa na cheo ili ufanye vitu vya tofauti. Unachohitaji ni kuchukua hatua ili kufanyia kazi yale ambayo umeamua kufanya bila ya kurudi nyuma.
Huhitaji kuwa na cheo ili uongeze juhudi kwenye kazi zako. hata kama hauna cheo unapaswa kufanya kazi zako kwa bidii kiasi kwamba hakuna mtu anayeweza kufanya kazi kwa viwango vikubwa kama wewe.
Siku moja nilikuwa nasoma kitabu cha ELON Musk, kitabu kilichoandikwa na Ashlee Vance, kwenye kitabu hiki, mwandishi anasema kwamba, Elon Musk na watu wake kwenye kampuni ya SPACEX wanafanya kazi kwa viwango vikubwa sana kiasi kwamba mtu mmoja kwenye kampuni ya SPACEX ni sawa na watu wawili wa kawaida kwenye makampuni mengine. Ebu pata picha na wewe kwenye kazi zako ukifanya kazi kwa viwango kama hivi hapa. Yaani, kazi yako unayofanya, ikawa ni ya viwango vikubwa kiasi kwamba kazi ambayo unafanya kwa siku moja wewe watu wengine wakaifanya kwa siku mbili mpaka tatu.
Hiki kitu ukikitumia kwenye kazi na shughuli zako ujue unaweza kufanya makubwa sana. KWA HARAKA NAJUA UTANIAMBIA kwamba kitu kama hiki hakiwezekani, utasema kabisa kwamba haiwezekani kufanya kazi ya siku mbili ndani ya siku moja. ila nina uhakika umewahi kufanya kitu kama hiki kwenye maisha yako, ila utakuwa ulifanya hiki kitu wakati uko kwenye msukumo (pressure) mkubwa wa kukamilisha majukumu yako.
Pengine kuna siku ambayo ulikuwa na majukumu ambayo ulipaswa kuwa umeyafanya ndani ya mwezi au wiki husika ila hukufanya hivyo, ni mpaka siku moja hivi ya mwisho ilipofika na kesho yake kazi ikawa inatakiwa, ukaamua kufanya kazi kwa bidii na kujituma sana ndani ya muda mfupi kuhakikisha kwamba unakamilisha kazi na kuifikisha kwa wahusika.
Ndani ya siku moja au mbili za mwisho ukajikuta kwamba umeweza kukamilisha majukumu ambayo hapo mwanzoni yalipaswa kuchukua wiki nzima. Katika mazingira kama haya rafiki yangu hapa ndiyo ulikuwa umefanya kazi ya wiki au wiki moja au mbili mbili ndani ya muda mfupi.
Sasa ebu pata picha ukifanya kazi kila siku kama hivi. Yaani, kila siku ukifanya kazi ambayo watu wengine wanafanya kwa siku mbili wewe ukaifanya kwa siku moja. Ni wazi kuwa utapiga hatua kubwa, matokeo makubwa yanaweza yasionekana mwanzoni, ila ni uhakika kuwa kadiri utakavyoendelae kufanya kazi na kuchapa kazi kwa bidii itafikia hatua ambapo matokeo yatakuwa hayaepukiki.
Unajua ni kitu gani ambacho huwa kinamsukuma mtu kukamilisha kazi kubwa ndani ya siku moja au mbili. Ni kwa sababu huwa kuna deadline. Yaani, siku ya mwisho ya kukamilisha kazi. Hiki ni kitu ambacho na wewe unapaswa kuanza kukitumia kwenye kazi zako kuanzia sasa hivi.
KUMBE KAZI YOYOTE ile unayopapaswa kufanya hakikisha kwamba unajipa siku ya mwisho ya kukamilisha hiyo kazi (yaani, deadline). Hiki kitu ni muhimu sana kwako maana kitakusukuma kwenye kufanyia kazi majukumu yako na kuhakikisha kwamba umejisukuma kuyafanyia kazi kwa viwango vikubwa sana kwa namna ambavyo hakuna mtu mwingine anaweza kufanyia kazi hivyo. Hiki kitu kitakuweka mbele sana zaidi ya mtu mwingine yeyote ambaye wewe unamfahamu
Sasa je, vipi kama utaamua kufanya kazi zako za kila siku kama vile siku hiyo ni siku ya mwisho ya kuwasilisha kazi hiyo? Je, vipi kama utaamua kufanya kazi zako, kama vile hutakuwa na siku nyingine ya kufanya kazi ambayo utafanya kazi yako? Nina uhakika kufanya kazi kwa viwango kama hivyo rafiki yangu kutakufanya kuwa mtawala mkubwa kwenye kazi na shughuli zako ambazo utakuwa unafanya. Mara zote na siku zote hakikisha kwamba unaweka kazi kubwa hivyo. Hiki kitu tu kitakufanya kuwa mtawala mkubwa sana.
SOMA ZAIDI: Vitu Vitano Vitakvyokuwezesha Kupata Maisha Ambayo Umekuwa Unatamani
Moja kati ya watawala ambao waliwahi kutokea alikuwa ni Napoleon Bonaparte, huyu ni mtawala ambaye aliweza kufanya makubwa enzi zake. Lakini kitu kikubwa na cha tofauti sana ambacho huyu mtawala aliweza kufanya kilikuwa ni kufanya kazi kwa bidii na kujituma sana. Unaambiwa Bonaparte alikuwa anafanya kazi hata muda ambao alikuwa anaenda kuoga. Kama alikuwa anaoga na anatokea mtu anamwabia kwamba kuna kitu ambacho unapaswa kusaini, basi alikuwa anatoka mara moja kwa ajili ya kuhakikisha kwamba anasaini kile kitu kisha anaendelea na kuoga. Hiki kitu ni rahisi kusema, na ni rahisi wewe kusoma hapa na kujiambia kwamba nitafanya kazi kwa bidii na nitajituma sana kwenye kazi zangu. Na pengine ndani ya siku mbili au tatu, unaweza kufanya kitu kama hiki lakini baadaye ukajikuta kwamba baada ya siku chache unakwama na kuachana kile ulichokua unapaswa kufanya na kuendela na maisha yako ya kawaida.
Lakini ninachokuandikia hapa unapaswa kuwa ndiyo mwongozo ambao wewe binafsi unaufuata kwenye kazi na kwenye shughuli zako binafsi za kila siku. Yaani, hakikisha kwamba kila siku unaweka kazi kwenye shughuli zako bila ya kuacha. Yaani, hakikisha kwamba, kila siku inakuwa ni siku ambayo unaweka kazi na muda wa kazi kunakuwa hakuna sumbufu wowote ule ambao unakusumbua wewe wala kukurudisha nyuma kwenye kazi au shughuli zako. Rafiki yangu mpendwa. Penda sana kazi kuliko unavyopenda kitu kingine chochote.
Sasa hapa ndipo huwa kinatokea kitu ambacho kinachanganya sana watu. na kitu hiki siyo kingine bali ni kwamba unapaswa kufanya kazi SMART NA SIYO KUFANYA KAZI KWA BIDII. Hiki kitu kinachanganya si ndio?
Yaani, kwamba ufanye kazi SMART au ufanye kazi kwa bidii? Kitu kimoja kikubwa ni kwamba kufanya kazi kwa bidii kunaweza kukutofautisha wewe na watu wengine wote unaowafahamu. Lakini ninachohitaji ufahamu wewe binafsi ni kuwa unapaswa kufanya kazi siyo tu smart,bali unapaswa kuhakikisha kwamba umefanya kazi kwa bidii na SMAET pia kwa wakati mmoja.
Juzi juzi hapa umegunduliwa mtandao wa ChatGPT. Mtandao ambao unaweza kufanya vitu vingi mpaka kuandika. Unaweza kuandika makala, mpaka kitabu! Ni wazi kuwa watu waliotengeneza huu mtandao ni watu ambao wanafanya kazi kwa bidii kubwa sana.
Na hiki ni kitu ambacho hakiwezi kutokea ndani ya siku moja tu bila ya kufanya kazi. Japo watu wengi wanasema kwamba huu mtandao utasaidia kwenye kufanya nyingi. Au kwa lugha nyingine kwamba mtandao huu utafanya kazi SMART, lakini, nina uhakika mkubwa kuwa waliotengeneza hiki kitu ni watu waliokuwa wanafanya kazi kwa bidii kubwa sana. Na pengine walikuwa hawalali. Kumbe kwa mantiki hiyo basi kufanya kazi kwa bdii na kujituma ni kitu ambacho hakiepukiki rafiki yangu. Yaani, kufanya kazi kwa bidii na kutawala ni mapacha wawili ambao wameshikamana.
Soma zaidi: JINSI UBUNIFU UNAVYOWEZA KUKUINUA KWENYE BIASHARA
Dhana ya kutawala inapoanzia Ni Martin Luther King Jr, ambaye aliwahi kusema kwamba, ukiwa unafagia unapaswa kufagia kiasi kwamba
1
JIFUNZE, CHUKUA HATUA
Kupata ebook hii mpaka mwisho utachangia kiasi kidogo cha fedha ambacho ni sawa na shilingi 2,000/ tu
Ukitaka kupata mafunzo ya kina kama haya ambayo yanatolewa kila wiki. Utachangia elfu tano. Bonyeza hapa chini kupata ebook hii mwanzo mpaka mwisho
2
PATA EBOOK YOTE
Changia kiasi cha shilingi 2,000/ tu kupata ebook hii yote. Utanishukuru baada ya kuisoma. Bonyeza hapa chini kuipata
3
WATU WENGI WAMESHAPATA EBOOK HII
Watu wengi wameshapata ebook hii. na wengine zaidi wanazidi kupata ebook hii.
Na wewe chukua hatua uweze namna ulivyozaliwa kutawala
Watu pia wamependa: THE SIMBA MENTALITY