Siku ya leo kuna vitu vitano ambavyo naamini kwamba ukivifanyia kazi, unaenda kuwa na maisha ambayo umekuwa ukiyatamani kwa siku nyingi. Kilichokukwamisha wewe kuweza kupata maisha unayoyataka ni kwa sababu hujafanyia kazi hivi vitu vitano hapa.
Kitu Cha Kwanza Ni Kujua Watu Wanataka Nini. Ukijua watu wanataka nini, wewe pia utaweza kupata kitu chochote kile ambacho unataka. Kivipi unajiuliza, iko hivi, kama kuna kitu ambacho watu wanataka na wewe ukawaletea hicho kitu, ni wazi kuwa hawa watu wantakuwa tayari kukulipia na kwa jinsi hiyo utaweza kutengeneza kipato chako kizuri tu.
Lakini je, unajuaje kitu ambacho watu wanataka.
Hapa utaangalia vitu ambavyo watu wanapenda kufuatilia
Vitu ambavyo watu wanapenda kuongelea mara kwa mara
Matatizo ya watu pia yanaweza kukuonesha vitu ambavyo watu wanataka
Lakini pia kuna vitu ambavyo kwa asili tunataka. Chakula, mavazi na malazi. Na havitabadilika. Kwa hiyo, angalia ni kwa namna gani ambavyo unaweza
Kwa hiyo kazi yako ya kwanza kabisa rafiki yangu ni kuangalia watu walio kuzunguka wanataka nini. Ukishajua kitu ambacho watu wanataka, basi wape hicho kitu, na hao watu watakuwa tayari kukulipa.
- SOMA ZAIDI: Jinsi ya kupata chochote unachotaka
- Ukiweza Kumpa Mtu Kitu Hiki , Basi Utapata Chochote Unachotaka Kutoka Kwake
Pili Ni Kufanya Hicho Kitu Kwa Ubora Na Ubunifu
Kuna kanuni ambayo unaweza ukawa hujawahi kuisikia. Inaitwa copy-cut principle. Kulingana na kanuni hii ni kwamba kwa kitu chochote kile ambacho unafanya. , hata kama umeanza kufanya hicho kitu kikiwa kipya, ndani ya miezi sita, kuna watu watakuwa nao wameanza kufanya hicho kitu. Watakopi unachofanya na wataanza kukifanya wao pia.
Hiki kitu ndiyo kinaitwa copy-cut. Unaweza kuanzisha mgahawa eneo fulani. Ndani ya miezi sita, ukakuta kuna watu watatu au wanne nao wameanzisha migahawa kama wa kwako halafu eneo hilohilo.
Sasa ili kujitofautisha kwenye kile unachofanya unahitaji kuwa mbunifu na kuhakikisha kwamba unafanya unafanya kile unacahofanya kwa ubora
Lakini ubunifuni ni nini? na utauwekaje kwenye biashara? Hii ni mada ndefu ambayo siwezi kuiongelea yote kwenye hii makala ila kwa leo itoshe kusema kwamba ubunifu ni kufanya vitu kwa namna ta tofauti na vile ulivyofanya jana. Na hapa huhitaji kufanya mapinduzi makubwa kwa wakati mmoja. Badala yake unaweza kufanya marekebisho ya kitu kimoja baada ya kingine, baada ya muda biashara yako ikawa inazidi kuboresheka zaidi.
Mfano leo hii unaweza kujiweka kwenye viatu vya mteja wako na kuangalia kama ungekuwa mteja kwenye biashara yako, je, ungependa kupata huduma ambayo inatolewa kwenye biashara yako? Kama huduma hiyo hujaipenda basi unaangalia wapi pa kuboresha ili uweze kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wako.
Lakini pia kesho unaweza kuboresha kipengele cha huduma kwa wateja na kukifanya kuwa bora zaidi.
Kwa vyovyote vile unakuwa hutulii kwenye hali ileile kila siku. Badala yake unakuwa unazidi kukua na kufanya kitu kwa ubora na ufanisi zaidi.
Tatu Ni Kuwa Na Mwendelezo Wa Kile Unchofanya
Watu wengi huwa wanapenda kuanzisha vitu ila wanaishia njiani. Sasa naomba unisikilize kwenye hili, bila kujali kwa sasa unapitia kwenye hali gani. kwa vyovyote vile jitahidi kuendeleza ulichoanzisha bila ya kukoma. Kuna watu wengi huwa wanapenda kuanzisha vitu ila huwa wanaishia njiani. Sikiliza, kitu kimoja cha uhakika ni kwamba ukiweza kuwa na mwendelezo wa kile ulichoanzisha, utaweza kufika mbali.
Haijalishi umeanzia wapi, haijalishi umeanzia kwenye hali ya chini kiasi gani. Bado utaweza kufika mbali na kuona makubwa endapo tu utakuwa na mwendelezo wa kile unachofanya bila ya kuacha.
Nne Ni Kujifanyia Tathimini
Ni muhimu sana uwe unajifanyia tathimini kila mara kuona vitu gani ambavyo umefanya na vimefanya vizuri na vitu gani unafanya ambavyo havijaenda vizuri. Na kwa jinsi hii utaweza kuona wapi labda kuna mwanya ili uweze kuuziba, au labda utaona kwamba kuna vitu ambavyo umekuwa unafanya kwa mazoea, na sasa unahitaji kuviboresha na kuvifanya kwa uzuri zaidi.
Tano, Ukifanya Makosa, Usijishikize Kwenye Makosa Yako. Inuka endelea mbele. Ni kweli huwa tunafanya makosa kwenye vitu ambavyo tunafanya, ila sasa usijishike kwenye makosa yako. Badala yake ukifanya makosa, imuka, kisha songambele ili uweze kufanya makubwa zaidi.
Kwa leo naishia hapa
Nakutakia kila la kheri
Godius Rweyongeza
0755848391