Je, ni kwa namna gani wewe unaitumia simu yako kwa manufaa?


Wakati mwingine ukiambiwa kwamba simu yako ina uwezo mkubwa, unaweza kudhani ni masihala vile. Leo nimechapa mawasiliano (namba za simu) yaliyo kwenye moja ya email yangu. Nimepata karatasi zenye  kurasa 131

Na kila ukurasa umejaa juu mpaka chini.

Nilipobeba karatasi zenye haya mawasiliano mkononi ndiyo nikagundua ni kwa namna gani simu yangu imebebeba vitu vingi sana.

Nikajaribu kufikiria kama hivi vitu vyote vikiwekwa kwenye karatasi au kwenye mfumo wa kushika mkononi, pengine vinaweza visitoshe kwenye nyumba nzima (naweza kuwa nimetia chumvi kidogo hapa).

Mfano email yangu moja ina zaidi ya email elfu ishirini na tatu!

Vitabu zaidi ya elfu moja ambavyo vipo kwenye simu.

Sms za whatsap hata sijui ni ngapi

Sms za kawaida kama zote.

Hivi kama hivi vitu vyote vikichapwa kwenye karatasi kama nilivyofanya kwa namba za simu nitakuwa na karatasi zenye kurasa ngapi?

Hapo sijazungumzia screenshots ambazo huwa nachukua hapa na pale.

Picha za kawaida

Video na ……..

Hiki kitu nataka kikuoneshe thamani ya kifaa kidogo unachobeba mkononi mwako na kwenye mfuko wako leo hii.

Ukihitajika utoe kila kilicho kwenye simu ukibebe, huwezi kubeba vyote, (labda kama wewe ni hawafu mweye nguvu)

Miaka kama mitatu au minne hivi ya nyuma nilikutana na nukuu ambayo imekuwa ikinifanya nijitahidi kuitumia simu yangu kwa uzuri kila mara. Na nukuu hii ilikuwa inasema kwamba simu tunazotumia leo hii, zina uwezo mkubwa kuliko hata kompyuta iliyopeleka mtu mwezini.

Ebu pata picha ya kifaa ulichonacho leo hii. Yaani, kwa kifaa ulichonacho leo hii. Kina uwezo kuliko mtu kompyuta ya mwaka 1969 iliyopeleka mtu mwezini. Kinadharia ni kwamba, ukitaka kutumia kifaa chako hichohicho, unaweza kupeleka watu mwezini.

KUNA WATU WAMEONA FURSA YA KUTUMIA hiki kifaa (simu) vizuri. Na kuna watu ambao wanatumiwa na hiki kifaa.

Wewe uko upande gani?

Siku za nyuma niliwahi kushirikisha kuhusu vijana wa KiNigeria waliotengeneza kwa kutumia simu yao ya iliyoharibika haribika.Je, wewe ni kama hawa vijana wa kiNigeria waliotengeneza tamthiliya kwa kutumia simu? Au wewe ni kijana ambaye muda wote anafuatilia umbea kwenye simu yake.

Una app za umbea kwenye simu yako kuliko ulivyo na app za kujifunza vitu vya maana. Kama wewe ni mmoja wao, badilika.

Tena futa hizo app kabla sijafika hapo sasa hivi, hahaha,

Usiwe na wasiwasi, hapo siji, ila kama unazo kweli, FUTA

Niliwahi pia kushikirisha habari za kijana Khaby Lame ambaye aliachishwa kazi mwaka 2020. Je, wewe ni kama huyu kijana ambaye aliachishwa kazi wakati wa kipindi cha UVIKO-19 akaamua kuitumia simu yake kwa manufaa. Au, kazi yako ni kuwasimanga watu kwa simu yako?

Unakopa mpaka salio ili upate MB, na hakuna chochote cha maana unafanya?

Je, ni kwa namna gani wewe unaitumia simu yako kwa manufaa?

Nasubiri ujumbe wako sasa….

SOMA ZAIDI: Vitu 21 Ambavyo Ni Lazima Kufanya Hata Kama Una Kipaji Kikubwa

Uwe na siku njema

By the way, nimeandika kitabu kinachoitwa ZAMA ZIMEBADILIKA, MAISHA YAMEBADILIKA, AJIRA HATARINI NA WEWE BADILIKA. Hiki kitabu ni softcopy kwa sasa na gharama yake ni 10,000/- tu.

Kupata kitabu hiki, unalipia elfu kumi tu. Namba ya malipo ni 0684408755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA.

Ukishalipia, nitumie ujumbe kwa namba hiyohiyo, ili nikutumie kitabu chako

Uwe na wakati mwema.

MAKALA HII IMEANDIKWA NA

Godius Rweyongeza

Kuwasiliana na Godius Rweyongeza, tuma ujumbe kwenda godiusrweyongeza1@gmail.com

Au 0755848391

Mpaka wakati mwingine

Tchao


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X